Hati ya muungano wa tanganyika na zanzibar ya mwaka 1964 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hati ya muungano wa tanganyika na zanzibar ya mwaka 1964

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Emashilla, May 31, 2012.

 1. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waliokuwepo au wanaojua vizuri kuhusu muungano wa nchi hizi mbili, wanatueleza ya kuwa hati ya muungano ya mwaka 1964 na hii inayotumika katika katiba ya mwaka 1977 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umekosa sifa za kuleta muungano imarai. Sababu mojawapo ni kuinyima nchi ya Zanzibar au kuipunguzia nguvu ya dola katika serikali ya Muungano. Pia, Zanzibar kwa sasa hainufaiki na muungano huu kama vile ilivyokuwa hapo awali. Je!Serikali au Chama Cha Mapinduzi haioni kuwa vurugu za hivi sasa huko Zanzibar zinatokana na kero kama hizi katika muungano?
  Lakini naona iko haja ya kuruhusu mjadala wa kitaifa kuhusu muungano ambao una sura isiyoeleweka kwa walio wengi. CCM, naishauri irudi nyuma kidogo na kufungua mijadala ya wazi ili kuondoa kero katika muungano. Nadhani kuendelea kuiweka Zanzibar katika mazingira ya kunufaika kwa bajeti zinazoonekana kama ni mbili haitoi sura nzuri kwa uhai wa muungano wetu mzuri. Je! Wana-jamii mna maoni gani kwa suala hili la kubadilishwa kwa hati ya muunagnao na vurugu za huko visiwani?
   
 2. t

  tricky Member

  #2
  Apr 12, 2014
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  naomba kujua ni kitu gani kitatokea katika hiki kinachoitwa muungano wa tanganyika na zanzibar endapo itafahamika kwamba hati ya muungano ipo ila si halali ama haipo kabisa,.je muungano ndo basi tena ama bunge maalumu la katiba litachukua hatua gani?
   
 3. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2014
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,081
  Trophy Points: 280
  Mungu apishe mbali, isiwe hivyo; mbona hatari! Ikithibitika hivyo, maana yake muungano uliopo ni batili na kwa miaka yote 50 ya wimbo wa muungano tulikuwa tunacheza kiduku. Kwa hakika ninaweza kuona hatari kubwa mbele. Na ndipo hapo ninapoilaumu CCM kwamba kama wanajua hizo hati hazipo au kama zipo ni batili the best they could do ni ku-support mapendekezo ya Tume ya Warioba fasta yaani wakubaliane na mawazo ya Serikali 3 na mchezo ungekuwa umekwisha sidhani kama kungekuwa na ambaye angehoji hati za muungano kwa nguvu kivile.

  Bahati mbaya ndio hivyo tena, CCM, kutokana pengine na kiburi tu, wanashindwa kuchangisha karata zao vizuri ili kuuwa masoo mengine yasiyo na mpango. Angalia wanavyozidi kumwaibisha Mwl. mchana kweupe kutokana na misimamo yao ya kihafidhina; Mwl. anaaibika ujue! Wananchi wamerahisishia kazi lakini jamaa wanaonekana kuwa kichwa ngumu. Wakati, ukuta.
   
 4. t

  tricky Member

  #4
  Apr 12, 2014
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  shukrani mkuu..dudus.
  vp unaweza nipa tena somo kuhusu contect ya hati ya muungano..
   
 5. Alex Manonga

  Alex Manonga Verified User

  #5
  Apr 12, 2014
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Naona watanzania tunaelekea kuchanganyikiwa. Japo najua hati ya Muungano ipo lakini uhalali wa Muungano huu hautokani na vipande vya karatasi vyenye saini ya Nyerere na Karume pekee, uhalali wa kisheria. Mtu yeyote duniani atakayeukana Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo baada ya miaka 50 ya uwepo wake kwa sababu hakuona karatasi yenye wino wa Nyerere na Karume atakuwa mwendawazimu. Kama wino ungekuwa kitu cha maana leo Crimea isingeondoka Ukraine kujiunga na Urusi, majimbo ya Marekani yaliyoingizwa kwenye Muungano ama kwa kununuliwa kama suti au kwa mtutu wa bunduki yangejitoa kwenye union. Yapo mambo mazito na maana zaidi ya vipande vya karatasi, damu mojawapo, at least on our case.

  Mtu anayetetea muundo wa serikali tatu kwa hoja ya ubatili wa Muungano kutokana madai ya kutokuwepo kwa hati anataka kutuambia msingi wa uhalali wa serikali tatu itakuwa kitu gani kama tayari msingi anaona unakosa uhalali? Hawa wanataka kuvunja Muungano kwa kisingizio cha muundo wa serikali.

  Muungano ulishatokea, upo, hauna matatizo, sisi tuna matatizo. Tujirekebishe na tusonge mbele. Makosa ya wazee wetu tuwaachie wanahistoria. Tukianza kuhoji uhalali wa kisheria hata Tanganyika mnayoidai haitakuwa na uhalali kwa baadhi ya watu maana wakoloni wa kijerumani hakuwauliza wanyamwezi kama walitaka kuwa sehemu ya Tanganyika, wahehe kadhalika hawakuulizwa, maana walikuwa na falme zao lakini bila kuwauliza wakoloni walijifungia huko Berlin na kuamua wanyamwezi, wahehe, wabarbaig, wachaga nk wawe kwenye kipande cha ardhi katika bara la Afrika wakaibatiza jina Tanganyika. Hawa nao wakianza kudai mtawakataa kwa hoja gani? Utakatifu wa Tanganyika ambao haupo kwa Tanzania ni kitu gani? Kwamba Tanganyika tuliachiwa na wakoloni na Tanzania imeundwa na waafrika? Wazungu hawakosei, waafrika wanakosea, siyo? Huu uroho wa madaraka hautatutoka siku tutakapopata serikali ya Tanganyika!

  Katika taifa lolote, hata marekani, kuna mambo ni taboo. Hayahojiwi, kwa kuwa mkianza hakuna mwisho.
   
 6. h

  hagaimwakilembe Member

  #6
  Apr 12, 2014
  Joined: Mar 31, 2014
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa ni huu mkataba wa muungano aka Hati na kwa kuwa watawala wamezoea uongo usio na mfano bhasi ndo maana tumefikia hapa lakini wangekuwa wanaregurate mambo ata watu wasingekuwa ma shahuku ya kutaka kujua hati ya muungano hipo wap na inasema nn lakini kwa uongo wao ulio pindukia sasa unakaribia mwisho.
   
 7. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2014
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kumbe huelewi hata thamani ya maandishi? Katika mbwiga wa karne na wewe umo! Nikuulize swali, kwanini ukinunua kitu unapewa au unatakiwa udai risiti. Kitu si unacho risiti ya nini? Risiti ni karatasi yenye maandishi. Ukipata jibu, nenda kakojoe ukalale.
   
 8. Alex Manonga

  Alex Manonga Verified User

  #8
  Apr 13, 2014
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sikusema maandishi hayana thamani, nimesema si msingi pekee wa uhalali wa Muungano wetu. Msingi wa Muungano wetu ni damu zaidi na utamaduni kuliko makaratasi yanayoitwa hati. Mbona hamdai udongo uliochanganywa mkatawanye mpate ya Tanganyika na Zanzibar? Endeleeni kupiga porojo Muungano mtauacha!
   
 9. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2014
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,155
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Kwa akili yako unadhani udongo uliochanganywa ni Tanganyika na Zanzibar!? Kwa hiyo leo ukichukua udongo wa Marekani ukachanganya na udongo wa Tanzania utakuwa umetengeneza muungano wa Marekani na Tanzania!? Acheni Tanganyika yetu irudi tumechoka na porojo zenu zisizo namashiko
  MUNGU IBARIKI TANGANYIKA
   
 10. m

  matawi JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2014
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ni cheti cha ndoa, hukijui?nenda ofisi ya dc wakuonyeshe
   
 11. m

  maswitule JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2014
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,385
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Enyi wenzangu wa Tanzania, hakuna hata binadamu mmoja iwe wa Zanzibar au wa Tanganyika anayepinga suala na Muungano kilichopo ni Muundo wake, wengi ambao ni wananchi wakiwemo hata wa CCM wanataka serikali tatu, ila tunashangaa kikwete na Kingunge Ngumbale Mwiru wanataka serikali Mbili ziendelee eti kwa hofu ya JK ya muungano kuvunjika mikononi mwake. Kile watu wa TZ wamekipenda na kienziwe mbona matokeo ya Ubunge Chalinze na ya Urais 2010 vilikubaliwa JK?
   
 12. t

  tricky Member

  #12
  Apr 13, 2014
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  gamba on work..ndo uwezo wako ulipoishia..
   
 13. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2014
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,804
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
  japo throne hiyo hati ....
   
 14. OMJ

  OMJ JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2014
  Joined: Apr 24, 2013
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ina maana bado Tanzania haijapata Uhuru, na kwa upande wa muundo wa muungano. Mbona ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar? na kama ni muungano huo kuanzia siku ya muungano hadi leo tulikuwa na sura hii:
  1. Serikali ya Zanzibar
  2. Serikali ya Tanganyika/Tanzania-kwa sasa
  3. Serikali ya Muungano wa Tanzania -kwa sasa
   
Loading...