Hati ya Mashtaka dhidi ya Freeman Mbowe iliyotumiwa Julai 26, 2021

Mashtaka ya kipuuzi na ya kutunga, Mbowe kutaka Katiba Mpya sio kupanga kulipua vituo vya mafuta, hii dhulma iko siku mtaulizwa mbele ya safari mmekosa aibu kabisa.
Mama alifikiria akirembua hovyohovyo atapendwa,kumbe watu wanamuona kilaza mla urojo
 
mashtaka ambayo siyo ya kipuuzi yangekuwaje, weka mfano wake. cdm mbona mnapungukiwaga akili naman hiyo? mashtaka mazito kama hayo unasema ya kipuuzi? jeuri imewafikisha wapi hadi sasa? segerea.
Unaliwa mzutii na wanaccm wenzako
 
Humjui Mbowe wewe!
Ni rahisi, Kama ulikuwa unawasikiliza vizuri wale waliotoka CHADEMA, ungeng’amua mapema ‘ugaidi’ wa viongozi wa CHADEMA. Angalia tu aina ya viongozi wa CHADEMA!
Watu wanapanga kulipua ofisi zao alafu wanasingizia serikali. Mbona usanii mwingi waliokuwa wanafanya ukichunguza ulikuwa unajulikana! Kujiteka, au wakiitwa polisi wanadanganya wametishiwa kutekwa, na wakikamatwa wanastage kwamba wametekwa. Kumbuka hata usanii wa kuchapa karatasi za kura siku ya uchaguzi!

Fuatilia hata kupotea kwa Ben Saanane kwa vyanzo vya watu wa CHADEMA, kwamba Saanane alimtishia Mbowe kuwa atatoa siri zake zote endapo atamuachisha kazi kama alivyopanga. Jiulize ni siri gani hizo? Alafu baadaye Mbowe anamvuta Saanane karibu na kumpandishia mshahara! Kisha anapewa safari ya kwenda SA kwa kazi maalum, ghafla anapotea! Alafu vijana waliopangwa mitandaoni wanaendeleza propaganda za kupotosha,

Au umesahau Mbowe alivyosingizia kapigwa na kuumizwa na watu wasiojulikana! Na jinsi viongozi wa ngazi za juu wa CHADEMA walivyokuwa wanaigiza kwa waandishi wa habari jinsi Mbowe alivyovamiwa! Kina Msigwa! alafu ukweli unakuja kujulikana in usanii tu!

Kesi hii itawafungua macho waliokuwa hawaijui CHADEMA, kwangu sishangai na najua mengi zaidi yanaweza kujulikana.
Ushuzi

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Mashtaka ya kipuuzi na ya kutunga, Mbowe kutaka Katiba Mpya sio kupanga kulipua vituo vya mafuta, hii dhulma iko siku mtaulizwa mbele ya safari mmekosa aibu kabisa.
Mungu hadhihakiwi Mwendazake aliwafanyiwa Watu haya haya lakini Mungu akatenda Miujiza juu yake Endeleeni kuwaonea Wapinzani Malipo MUNGU wa YAKOBO ATAWALIPA
 
JE WENYE NCHI WANANCHI ?


  • Hati ya mashtaka mbovu
  • Kwanini Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu haiwezi kukataa hati ya kutajwa kesi
  • Nini mantiki ya DPP kutumia hati ya mashtaka yenye mapungufu kupeleka kesi mahakamani
  • Mbinu za kuchelewesha kesi kwa mgongo wa kutumia hati ya mashtaka mbovu
  • DPP anapotayarisha hati ya mashtaka anatakiwa toka mwanzo aoneshe kutenda haki
  • Katiba Mpya irejeshe mamlaka kwa wananchi
  • Katiba ya kupewa ambayo haijapiganiwa na wananchi serikali huidharau na kuikiuka kwa file inaonekana ni kama hisani kwani haikupiganiwa na wananchi bali 'wananchi wamepewa'
  • N.k n.k
Source : DarMpya TV
 
31 Julai 2021

HATI YA MASHITAKA DHIDI YA WANACHADEMA WALIOKAMATWA MWANZA INASEMA 'WAMEKULA NJAMA KUBWA'


Chadema Media TV
 
31 Julai 2021

HAYA NDIO MAAMUZI MAGUMU YA CHADEMA SAKATA LA KESI YA UGAIDI YA MBOWE, '' RAIS SAMIA AMEVUKA MIPAKA'



Source: DARMPYA TV
 
HAYA NDIO MAAMUZI MAGUMU YA CHADEMA SAKATA LA KESI YA UGAIDI YA MBOWE, '' RAIS SAMIA AMEVUKA MIPAKA'
Kama kuna watu wamemhimiza afanye haya, watu hao wamempotosha vibaya sana.

Lakini hii inaonyesha kwamba huyu mama hana msimamo thabiti na wala hana chochote anachokiamini.

Itakuwaje awe amesahau yale yote mazuri aliyokuwa ameahidi kuyafanya, na kuanza kutekeleza mengine, halafu kwa muda mfupi tu wa wiki kadhaa awe amesahau kila kitu juu yake, na kurudi kule kule alikokuwa amekwenda mtangulizi wake?

Huyu mama ni mbabaishaji, hana lolote huyu!
 
Ukiwa mpinzani machachari katika nchi zetu hizi zenye demokrasia bandia,ni sawa na kujitoa mhanga.
 
JE WENYE NCHI WANANCHI ?


  • Hati ya mashtaka mbovu
  • Kwanini Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu haiwezi kukataa hati ya kutajwa kesi
  • Nini mantiki ya DPP kutumia hati ya mashtaka yenye mapungufu kupeleka kesi mahakamani
  • Mbinu za kuchelewesha kesi kwa mgongo wa kutumia hati ya mashtaka mbovu
  • DPP anapotayarisha hati ya mashtaka anatakiwa toka mwanzo aoneshe kutenda haki
  • Katiba Mpya irejeshe mamlaka kwa wananchi
  • Katiba ya kupewa ambayo haijapiganiwa na wananchi serikali huidharau na kuikiuka kwa file inaonekana ni kama hisani kwani haikupiganiwa na wananchi bali 'wananchi wamepewa'
  • N.k n.k
Source : DarMpya TV

Fatma karuma amesoma uingereza, na amefanya kazi uingereza, hajui laws and procedures nyingi sana zinazo apply kwenye Tanzania legal system. anapotosha watu kwamba ile hati ni defective, hajui maana ya defective charge, na ni mweupe kweney criminal. kwenu ninyi mnaomfuatilia huyu mwanaharakati, jueni kwamba sheria ninazokubali kwamba amebobea ni za makampuni, biashara na arbitration etc, ila kwenye ulingo wa criminal ni mweupe halafu huwa hajui hata anachoongea. na hajawahi shika kesi yeyote ya criminal katika mahakama za Tanzania, kama ipo itaje hapa. aliwahi kumwakilisha nani? na alishinda?
 
kweli kabisa ni ya Kipuuzi na anaonewa lakini tusuburi kesi yenyewe ianze na hata ushahidi uanze kutolewa unaweza kushangaa yanajitokeza mambo ya ajabu ambayo yakawashangaza wengi.
mnavyoendelea kusubiri, ndoo inazidi kujaa kule segerea.
 
Jenerali Ulimwengu - Kesi hii ni medani nyingine ya kufanyia Siasa. Na Mahakama sasa kuwa uwanja mwingine wa kufanyia siasa

Mwandishi mkongwe na wakili wa mahakama kuu Jenerali Ulimwengu amesema tuhuma zinazomkambili mwanasiasa Freeman Mbowe ni muendelezo wa njama za kumtoa ktk reli ya kisiasa mwenyekiti wa CHADEMA

"Tafakuri ya kisiasa ni kuwa mbinu hii mpya ni hatua nyingine ya kujaribu kumtoa Freeman Mbowe katika uwanja wa siasa baada ya mbinu zingine zilizotumika huko nyuma kushindwa kufikia lengo la kumzima kiongozi huyo shupavu wa upinzani nchini Tanzania" anahitimisha maoni yake mwandishi wa habari na mchambuzi wa kisiasa Jenerali Ulimwengu.

huyu mnyarwanda naye ana lipo la kuisaidia TAnzania?
 
Aishi ni hotel ya nani
Ni Hotel ya Familia ya Mbowe. Iko Machame Hai District not Moshi District kama Hati ya Mashtaka inavyosomeka. Hivi hata kosa dogo hivyo wameshindwa kulitambua kabla ya kutoa hiyo hati? ''blowing fuel stations'' hiki ni Kibeberu cha wapi? ATTACKING, EXPLODING, BLASTING,

Located just in 15-min ride from the most popular trailhead to Kilimanjaro National Park, Aishi Machame Hotel is an ideal choice for those looking for peace and calm and creature comforts away from the city bustle.
The hotel is situated at the foothills of the Mount Kilimanjaro. The ambiance here is unique – surrounded by the African wilderness, this place is a real hideaway from bustling civilization and a perfect place to unwind. Aishi Machame Hotel features cosy garden view rooms, a swimming pool with a lounge zone, bar, restaurant and free Wi-Fi.
 
na kwa wanaomfahamu DJ, wanajua kabisa kwamba alifanya makisa hayo na alikuwa akiratibu. nyie wengine pigeni kelele lakini kelele zenu haziwezi kumtoa chura pangoni.
Na nyie acheni kelele basi,
HEBU pelekeni haraka huo ushahidi na hivyo vielelezo mlivyonavyo mkawasaidie mapolisi wenu ambao bado wanahanjahanja na kuendelea kuvunja maofisi ya CHADEMA na vituko vingine, ili kutafuta cha kuokoteza.
 
Back
Top Bottom