Hati ya Mashtaka dhidi ya Freeman Mbowe iliyotumiwa Julai 26, 2021

Niliacha kumkubali Mbowe tangu siku alipobadilisha gia angani in 2015. Lakini huu uovu unaoendelea sasa juu yake haukubaliki aisee. This is unfair and unacceptable
 
Ndio huyu aliyepost. Hapo bado anakazania Lissu atoe ushahidi wa innocence ya Mbowe kwa sababu amepost akisema kuwa Mbowe anaonewa. Go figure.

Amandla...
Huyu hata Lissu akitoa ushahidi anaweza kusema Lissu atoe ushahidi kwamba ametoa ushahidi.

Serikali ikimtuhumu mtu, ina wajibu wa kutoa ushahidi. Aliyetuhumiwa hana wajibu wa kutoa ushahidi kwamba hana kosa.

Hivi hawa watu wanajaribu kujielimisha kidogo tu sheria kabla ya kupost hapa JF?
 
Dah! Kutoka kupanga njama za kuua viongozi wa serikali hadi kulipua mitungi ya gesi!?
Upuuzi huu huwa anaupanga nani lakini? Kweli nimeanzan kuamini njama za kumuua Lissu walizipanga hawa hawa vichwa "think tank" waliondaa hii kesi......!

Watanzania kwa umoja wetu kazi yetu sasa iwe ni kuwatafuta hawa vichwa panzi! Unaweza kuta wapo sehemu nyeti serikalini ambayo maamuzi yao ndio yanaliongoza hili taifa! Hawa ndio wanapitia majina ya teuzi za mawaziri, mabalozi,nk hawa ndio wanajifungia sehemu na kuja na mbinu za kuinua uchumi na kutafuta muafaka wa tatizo la ajira, nk.nk....Jamani tuwatafute ili kunusuru taifa hili!
Diwani na mchengerwa wapuuzi tu
 
Mashtaka ya kipuuzi na ya kutunga, Mbowe kutaka Katiba Mpya sio kupanga kulipua vituo vya mafuta, hii dhulma iko siku mtaulizwa mbele ya safari mmekosa aibu kabisa.
Huenda hata kuteketea kwa solo la Kariakoo, anahusika.
 
Wenye mamlaka kamwe hawajifunzi ya kwamba yupo Mungu aonaye yote haya na ANATAZAMA...!!!
Wakikamatwa akina Mbowe ndio Mungu anatazama, wakikamatwa watu wengine huyo Mungu ghafla anakuwa kipofu, what the f***

Mungu huyo Mungu gani?

Kama ameonewa nendeni Court mkawa_prove wrong halafu huyo anayetuhimiwa ku_finance Ugaidi tuone akiachiwa kesho asubuhi.
 
Hivi kweli toka may 2020 yawepo mashitaka kama haya tena chini ya Magufuli halafu Mbowe ni mmoja wapo halafu Magufuli akae kimya bila kusema? pengine hao vijana walipanga hayo lakini kumuhusisha Mbowe ni uongo ambao itakuwa ngumu kuhuthibitisha kamwe......
Kama Mbowe angekuwa ameyatenda haya Magufuli asingelinyamaza hadi anakufa lazima angelisema kabisa wazi... asingeficha hiii...

Mimi kawakweli sijawai kuwa fan wa Mbowe na nimekuwa nikimtania sana Mbowe humu jf lakini katika maisha yangu ataungeniambia kuwa Mbowe ni mtu muovu au anapanga uovu tena ugaidi kama huu ulioandikwa hapa na DPP kwakweli nisingekuamini na kamwe siwezi kukuamini.......Mbowe awezi fanya haya....... uzuri wakati taarifa zinatoka hizi pale tulipokuwa watu wote sio fan wa Mbowe lakini walikataa kata kata kuamini taarifa hizi na wengi tulisema wazi hakuna ushahidi nitauamini kuwa Mbowe ni gaidi....
Mbowe awezi fanya haya kamwe kamwe...
Hapa wanapoteza muda tuuu
Humjui Mbowe wewe!
Ni rahisi, Kama ulikuwa unawasikiliza vizuri wale waliotoka CHADEMA, ungeng’amua mapema ‘ugaidi’ wa viongozi wa CHADEMA. Angalia tu aina ya viongozi wa CHADEMA!
Watu wanapanga kulipua ofisi zao alafu wanasingizia serikali. Mbona usanii mwingi waliokuwa wanafanya ukichunguza ulikuwa unajulikana! Kujiteka, au wakiitwa polisi wanadanganya wametishiwa kutekwa, na wakikamatwa wanastage kwamba wametekwa. Kumbuka hata usanii wa kuchapa karatasi za kura siku ya uchaguzi!

Fuatilia hata kupotea kwa Ben Saanane kwa vyanzo vya watu wa CHADEMA, kwamba Saanane alimtishia Mbowe kuwa atatoa siri zake zote endapo atamuachisha kazi kama alivyopanga. Jiulize ni siri gani hizo? Alafu baadaye Mbowe anamvuta Saanane karibu na kumpandishia mshahara! Kisha anapewa safari ya kwenda SA kwa kazi maalum, ghafla anapotea! Alafu vijana waliopangwa mitandaoni wanaendeleza propaganda za kupotosha,

Au umesahau Mbowe alivyosingizia kapigwa na kuumizwa na watu wasiojulikana! Na jinsi viongozi wa ngazi za juu wa CHADEMA walivyokuwa wanaigiza kwa waandishi wa habari jinsi Mbowe alivyovamiwa! Kina Msigwa! alafu ukweli unakuja kujulikana in usanii tu!

Kesi hii itawafungua macho waliokuwa hawaijui CHADEMA, kwangu sishangai na najua mengi zaidi yanaweza kujulikana.
 
Mashtaka ya kipuuzi na ya kutunga, Mbowe kutaka Katiba Mpya sio kupanga kulipua vituo vya mafuta, hii dhulma iko siku mtaulizwa mbele ya safari mmekosa aibu kabisa.

kweli kabisa ni ya Kipuuzi na anaonewa lakini tusuburi kesi yenyewe ianze na hata ushahidi uanze kutolewa unaweza kushangaa yanajitokeza mambo ya ajabu ambayo yakawashangaza wengi.
 
ukiangalia makosa yote aliyoshitakiwa nayo ni ya kipindi cha August, 2020, yaani soon before uchaguzi, hivyo kumbe alikuwa ameandaa kufanya ujinga wa kutisha, na mnakumbuka kuna baadhi ya sheli ziliungua kipindi kile, na criminal huwa haifi, hata kama ulifanya kosa miaka 20 iliyopita kama ushahidi upo wanaweza kukunanga hata leo. kwahiyo msimtetee tu, alijiandaa kwa namna yeyote ile mwaka jana achukue nchi hata kwa ugaidi. kasomeni sheria ya ugaidi mtajua elements zake. pia, kudai katiba isiwe kisingizio chenu/kinga, mnaweza kuwa mlifahamika muda mrefu tu wakaamua kuwapuuzia lakini mlipoanza kuleta jeuri serikali imeamua kuleta kibri, ndio dawa yenu.
Unatetea tumbo huna mpya
 
Maslahi gani ya Taifa Mkuu? Kila kesi ikifutwa sababu haina maslahi ya taifa tutabaki na kesi gani mahakamani? Mimi leo hii nikimtandika mke wangu, nikashtakiwa, ninaweza kuargue hiyo kesi haina maslahi ya Taifa. Ishu ya Bwana Mbowe nashauri viachwe vyombo vya sheria vifanye kazi yake. Ila lile wazo la Lissu la kutomwekea mawakili lisifuatwe, anaweza akafungwa na kwa tz yetu hii ilivyo maisha yataendelea na watu watamsahau

Jenerali Ulimwengu - Kesi hii ni medani nyingine ya kufanyia Siasa. Na Mahakama sasa kuwa uwanja mwingine wa kufanyia siasa

Mwandishi mkongwe na wakili wa mahakama kuu Jenerali Ulimwengu amesema tuhuma zinazomkambili mwanasiasa Freeman Mbowe ni muendelezo wa njama za kumtoa ktk reli ya kisiasa mwenyekiti wa CHADEMA

"Tafakuri ya kisiasa ni kuwa mbinu hii mpya ni hatua nyingine ya kujaribu kumtoa Freeman Mbowe katika uwanja wa siasa baada ya mbinu zingine zilizotumika huko nyuma kushindwa kufikia lengo la kumzima kiongozi huyo shupavu wa upinzani nchini Tanzania" anahitimisha maoni yake mwandishi wa habari na mchambuzi wa kisiasa Jenerali Ulimwengu.
 
Usisahau na wa Sabaya umeshaanza kulipwa

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
Hivi wewe hata kwa akili ya kawaida tu huoni Sabaya alikuwa jambazi na alikuwa anasemwa tangu akiwa mkuu wa wilaya. Sabaya alilalamikiwa sana tangu akiwa ofisini haijaanza ghafla. Aliumiza watu wengi na ushahidi hadi wa cctv camera upo mahakamani.

Yaani watu walioumizwa na Sabaya wapo wengi tena siku anefikishwa mahakamani wananchi walikusanyika kumzomea kwa vitendo alivyokuwa anavifanya.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom