Hati ya Mashtaka dhidi ya Freeman Mbowe iliyotumiwa Julai 26, 2021

chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,064
2,000
Kudai katiba mpya ndo kuwa gaid yana mwisho
ukiangalia makosa yote aliyoshitakiwa nayo ni ya kipindi cha August, 2020, yaani soon before uchaguzi, hivyo kumbe alikuwa ameandaa kufanya ujinga wa kutisha, na mnakumbuka kuna baadhi ya sheli ziliungua kipindi kile, na criminal huwa haifi, hata kama ulifanya kosa miaka 20 iliyopita kama ushahidi upo wanaweza kukunanga hata leo. kwahiyo msimtetee tu, alijiandaa kwa namna yeyote ile mwaka jana achukue nchi hata kwa ugaidi.

Kasomeni sheria ya ugaidi mtajua elements zake. pia, kudai katiba isiwe kisingizio chenu/kinga, mnaweza kuwa mlifahamika muda mrefu tu wakaamua kuwapuuzia lakini mlipoanza kuleta jeuri serikali imeamua kuleta kibri, ndio dawa yenu.
 
Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
7,710
2,000
Cha msingi CDM wasitumie nguvu nyingi sana kwenye kesi hii, bali waendelee na kuelekeza mapambano ya kudai Katiba mpya kwa nguvu zaidi sababu hilo ndilo lengo kuu kwa sasa. Dhumuni la CCM ilikuwa ni kumpiga mchungaji ili kondoo watawanyike na hili wameshalitimiza.

Kwa hiyo waonyesheni CCM kwamba kondoo hawatawanyiki na katiba mpya inaendelea kudaiwa kwa nguvu zote.
Huu ndio ukweli,hapo wasipoe kabisa,huku kesi ya Ugaidi inaunguruma huku makongamano ya katiba yanafanyika,watachanganyikiwa wenyewe
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,901
2,000
Binafsi nikiwa mmoja wa vyombo vya ulinzi na usalama nitamlipia Mbowe 'in kind'.
Hawa watawala dhalimu wanahitaji kufunzwa adabu, huku walipofika sasa ni too much kwa vile wanafahamu wananchi hawana la kuwafanya.

Kama kuwasulubu hawa mashetani wa ccm ndo 'ugaidi' wenyewe basi wajiandae kushuhudia vitendo vya kigaidi visivyo na kikomo kutoka humu humu ndani
Hapana, hayo sasa hayana lazima tena.

Hawa wamekwishaingia ndani ya msitari, hakuna wigo tena wa kufanya kukurukakara za aina hiyo tena.

Mhimu ni kwa CHADEMA kutopoteza lengo tena jinsi watakavyo ihitimisha kazi hii muhimu ya kuliokoa taifa hili.
 
Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
7,710
2,000
Hakyamungu kama haya ndio mashitaka yenyewe ni aibu.
Hakuna kitu cha msingi zaidi ya utoto wa mwanafunzi wa sheria aliyeko mazoezini kuombwa kuandika hat ya mashitaka kwa mara yake ya kwanza .
Aisee dunia hii kuna watu wamejaliwa kutokuwa na mahipa wa aibu.
Na ndio maana walimkwepa kibatala wakakimbilia kumsomea mashtaka kimyakimya,subiri vichekesho vya maswali ya Kibatala mahakamani ndio utajua hao waendesha mashtaka ni vilaza
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,547
2,000
Mtu anayeandika "kama hawana makosa njoo utoe ushahidi" hata haelewi where the burden of proof lays!
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,064
2,000
Any support to a dictatorship enables it to continue its oppression. Any type of sanctions against a dictatorship diminishes its capacity to oppress its own people. Our friends & partners shouldn't be complicit in the oppression of Tanzanians by supporting the Samia dictatorship! https://t.co/FO0yiGkjWV
Aache kulia lia na kututakia vikwazo, vikwazo vikiwekwa wanaoumia ni wananchi, yeye anakunywa bia huko ubelgiji. tena si ajabu hata kusali hasali. ukiangalia hati ya mashtaka, makosa yale yalifanywa soon before general election ya 2020. na kipindi kile kweli kuna baadhi ya sheli na maeneo mengine yalipigwa moto kama mabom hivi. selikali huwa inakuwa na ushahidi wa vitu vingi lakini inaamua kuweka pembeni ili kuangalia kama mkosaji hasa maarufu kama dj, kama ana adabu, wakiona analeta dharau, wanafungua tu file. mwaka jana walipanga kuvuruga kabisa hii nchi alimradi tu wachukue nchi.
 
Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,133
2,000
Binafsi siioni kesi hapo Kwa jinsi TU ya uaandaaji wa charge sheet! DPP amefanya kosa moja kubwa la kiufundi ambalo ndilo lililotumika kuwatoa wale mashekhe wa uamsho nalo ni kushitaki nje ya eneo lilikotokea kosa! Ukisoma charge sheet inaonyesha makosa hayo anayotuhumiwa Mbowe yalifanyika Hai mkia wa Kilimanjaro ambayo Ina mahakama za ngazi zote zenye uwezo wa kusikiliza shauri hilo. Kwanini iletwe kisutu ambayo ni mkoa ambao matukio hayo hayakufanyika? Hii ni kasoro ya wazi ambayo inadhihirisha kuwa hakuna kesi hapo Bali kupotezeana muda TU na kuchafuana! Na mkumbuke kuwa Mbowe alikuwa ana kikao Cha Baraza kui kule Mbeya July 31 ya kuwavurusha wale COVID-19! Kwa vyovyote mihimili yote ilikuwa inakwenda kuaibika hivyo wamemshikilia ili kuikwepa aibu hiyo!
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,377
2,000
Any support to a dictatorship enables it to continue its oppression. Any type of sanctions against a dictatorship diminishes its capacity to oppress its own people. Our friends & partners shouldn't be complicit in the oppression of Tanzanians by supporting the Samia dictatorship! https://t.co/FO0yiGkjWV

Hiyo wala sio kesi bali ni utoto
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
7,236
2,000
Any support to a dictatorship enables it to continue its oppression. Any type of sanctions against a dictatorship diminishes its capacity to oppress its own people. Our friends & partners shouldn't be complicit in the oppression of Tanzanians by supporting the Samia dictatorship! https://t.co/FO0yiGkjWV
Hii inahusiana nini na kichwa chako cha habari?

Amandla...
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
44,377
2,000
Aache kulia lia na kututakia vikwazo, vikwazo vikiwekwa wanaoumia ni wananchi, yeye anakunywa bia huko ubelgiji. tena si ajabu hata kusali hasali. ukiangalia hati ya mashtaka, makosa yale yalifanywa soon before general election ya 2020. na kipindi kile kweli kuna baadhi ya sheli na maeneo mengine yalipigwa moto kama mabom hivi. selikali huwa inakuwa na ushahidi wa vitu vingi lakini inaamua kuweka pembeni ili kuangalia kama mkosaji hasa maarufu kama dj, kama ana adabu, wakiona analeta dharau, wanafungua tu file. mwaka jana walipanga kuvuruga kabisa hii nchi alimradi tu wachukue nchi.

Kweli nimeamini mtu skizeeka akili zinakuwa za kitoto. Kwa jinsi ccm iliyozeeka kwa sasa imejikuta inafanya mambo ya kitoto.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom