Hati ya Mashtaka dhidi ya CAG Assad: Anachomokaje?

Status
Not open for further replies.
rais sometime anajidharirisha sana, tunajua kua haya yote ni maelekezo yake, na spika nae alivyo hana akili anakubali kupelekeshwa kama guta bovu
 
Hivi hayo maagizo anayotoa speaker ni maazimio ya bunge ama ni maazimio ya Ndugai?
Yakiwa ni maazimio ya Ndugai hayana uhalali wa kisheria wala wa kisiasa maana ni bifu binafsi.
Na izingatiwe kuwa hatujaona bunge likitoa hayo yanayosemwa na ndugai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1072282

Magazeti ya leo yamemnukuu Spika wa Bunge, Job Ndugai, akitaja mashtaka yanayomkabili CAG Assad. Ni kama ametaja hati ya mashtaka yenye tuhuma mbili, kama ifuatavyo:

JOB NDUGAI,
SPIKA WA BUNGE,
OFISI YA SPIKA,
DODOMA.

14 APRIL 2019.

PROFESA ASSAD,
CAG WA TANZANIA,
DODOMA.

YAH: WITO WA AMA KUJIUZULU AU KUJIELEZA KWA NINI USIADHIBIWE NA MWAJIRI WAKO

Somo hapo juu lahusika.

Unapatiwa taarifa kwamba, unakabiliwa na tuhuma mbili nzito zifuatazo.

Tuhuma ya kwanza: Huku ukijua kwamba, Bunge ni taasisi inayojumuisha Wabunge, Mawaziri na Rais, ambapo Rais ndiye mwajiri na mteuzi wa CAG; na ukiwa unaelewa kwamba, Hati ya Majukumu ya CAG haisemi kuwa kutathmini utendaji wa taasisi ya Bunge ni kazi mojawapo ya CAG, ulichukua hatua ya kufanya tathmini ya utendaji wa Bunge; na hivyo, kumdharau mteuzi wako kwa kufanya kazi iliyo nje ya majukumu yako uliyokabidhiwa rasmi. Mwenendo huu ni tabia mbaya inayotajwa katika kifungu cha 144(2) cha Katiba ya Tanzania (1977) kinachoongoza ajira yako kama CAG.

Tuhuma ya pili:
Huku ukijua kwamba, wewe sio msemaji wa ofisi inayohusika na kutathmini utendaji wa Bunge; alibeba jukumu la kuitangazia dunia kwamba, Bunge la Tanzania ni dhaifu kwa mujibu wa tathmini yako; na hivyo kutumia utaratibu wa mawasiliano unaolidhalilisha Bunge mbele ya wapiga kura na Jumuiya ya Kimataifa. Mwenendo huu ni tabia mbaya inayotajwa katika kifungu cha 144(2) cha Katiba ya Tanzania (1977) kinachoongoza ajira yako kama CAG.

Wito: Hivyo, ndani ya masaa 48 baada ya kupata barua hii, unatakiwa kujitokeza mbele ya Mteuzi wako na kufanya mojawapo kati ya mawili kwa mdomo na kwa maandishi:

(a) ama kujieleza kwa nini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa sababu ya “tabia mbaya” uliyoionyesha;

(b) au kujiuzulu mara moja kwa sababu ya “tabia mbaya” uliyoionyesha.

Katika kutekeleza wito huu unashauriwa kusoma kwa makini ibara ya 144 ya Katiba ya Tanzania (1977) inayosema yafuatayo:

“144. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake (ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (4) ya ibara hii. (3) (a) Iwapo Rais anaona kwamba suala la kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa, basi … atateua Tume Maalum… (4) Ikiwa Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (3) itamshauri Rais kwamba huyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aondolewe kazini kwa sababu ya kushindwa kufanya kazi kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote au kwa sababu ya tabia mbaya, basi Rais atamwondoa kazini."

Uelewa wangu kama Spika ni kwamba, kulingana na uzito wa kosa ulilolifanya, suala la kukuondoa kazini kwa mujibu wa masharti ya Katiba yetu halihitaji kuchunguzwa, na kwa hiyo hakuna sababu ya Rais kuteua Tume Maalum.

Wako katika ujenzi wa Taifa,

Job Ndugai,
Spika wa Bunge Tanzania.
1072814
 
Umeelewa maelezo yangu?,au ndio mikurupuko
LENGO linajulikana ****** hana nia nzuri kwa MH. ASSAD sababu ASSAD hakubali kupindishwa au kulishwa madhambi kama walivozoeshwa waliomtangulia.
nimekupa shortcut hiyo kuondoa mzizi wa FITINAT
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom