Hati chafu isiwe kigezo cha mateso ya watumishi manispaa ya Kigoma/Ujiji

Haludzedzele

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,468
528
Tangu kupatikana kwa hati chafu katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji imekuwa kama ni fimbo kwa Watumishi wengi hasa kada ya Elimu kwa Walimu as if huo uzembe umefanywa na watumishi wa kada hii kwani kwasasa pamekuwa hakuna lolote linaloendelea kwa watumishi hasa Walimu,

Hakuna pesa za nauli tangu 2016 hakuna upandishwaji wa madaraja tangu 2011 kiukweli jambo hili limekuwa kadhia kubwa sana na linaporosha sana morali ya kazi kwani kibaya zaidi ni Manispaa hii tu ambayo haipandishi watu madaraja wala kutoa pesa za nauli mbona mikoa mingine haifanyi hivyo na kama kweli serikali haijaruhusu upandishwaji wa madaraja ni kigoma tuu?

Mbona sehemu zingine wanapandishwa kama wanafanya kazi kwa mazoea basi mamlaka husika iangalie Kigoma kwa jicho la tatu kwani uzembe wa watu wachache isiwe mateso hata kwa watu wasio husika na uzembe huo.

Kiukweli hali hii inasikitisha na inakatisha tamaa sana kama mnapita pita humu viongozi wetu Mbunge Zitto pia Waziri Ndalichako jaribuni kulifikisha hili Utumishi liangaliwe kwa mustakabali wa Watumishi na Elimu kiujumla katika mkoa wetu!

Nawasilisha
 
Write your reply...nauli pesa zinaletwa karibu Council zote ,kutakiwa na shida ya utawala del wenu na ded
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom