luambo makiadi
JF-Expert Member
- Nov 28, 2017
- 10,295
- 8,257
Mbeya hoyeee,Nina nyumba hapo japo mm sio Mwenyeji wa huko nimefanya kazi hapo jijini kupo swafiHome Sweet Home
Mbeya ni mti wenye matunda acha upigwe mawe kuna baadhi ya watu wanajikuta tu wanaichukia mbeya ukimuuliza sababu hana au utaskia hamna mall, hamna maghorofa sijui hamna nini muulize babaako anayo iyo shopping mall, au unataka sehemu ya kupigia picha, ivi wanadhani kujenga mall ni kitendo cha kufungua zipu tu na kukojoa.
Mipango ya kujenga green city mall ipo na inaenda kwa hatua iyo rock city mall yenyewe imejengwa lini kama sio juzi tu ndo imezinduliwa.
Mnatakiwa mtambue Mbeya ilijengeka kitambo sana kabla hata aya mambo ya mipango miji hayajaanza watu walikua wanajimegea maeneo mitaa ya mwanjelwa, mabatini, simike na sehemu nyingine ambazo kwa kipindi icho zilikuwa zimechangamka. Saizi hayo maeneo ndiyo yanaonekana ya ovyo na sehemu ambazo zilikuwa zinaonekana mapori mfano New Forest, Iwambi, Isyesye kuna mpangilio mzuri wa majengo kwakua ni maeneo ambayo yamepangiliwa na mipango miji
Tena kuna mwingine utakuta anaishi kwenye nyumba ya udongo mkoani kwake uko afu anaanza kuidiss mby utaskia hamna nyumba nzuri mby. Ivi upo serious kweli?
Vile vile msisahau kuwa hii ni Tanzania tunaposema Mbeya ni jiji kwa level ya nchi yetu ni jiji tena kubwa sana limeiacha mikoa mingine mbali sana sana yani saaana. Sasa wewe unaesema Mbeya sio jiji uje na vigezo vyako vyenye maelezo sahihi kwanini sio jiji.
Mbeya sio kama mikoa mingine ambayo serikali inapeleka projects kubwa kwaajili ya kuiendeleza Bali mbeya inajengwa kwa kiasi kikubwa na wakazi wake.
Itezi ,uyole,Mama John oyeee