Hatari ya ukaburu mamboleo.

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
mgogoro wa Zanzibar ulio sababishwa na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka2015,unafungua aina mpya ya ukaburu.naam ni ukaburu kwani hauna tofauti na ubaguzi uliofanywa na makaburu wa Afrika ya kusini.Kikundi cha watu wachache wanaona wanayo haki ya kutawala milele hata kama wameshindwa kwenye sanduku la kura.Ni aina mpya ya ukaburu kwani tunashuhudia sasa mwafrika anahaki ya kuwatala watu walio mkataa.

Watanzania ni lazima tuungane kwa pamoja tukatae aina hii ya ukaburu.wamepora ushindi wa CUF kwa kumtumia Jecha, kesho watapora matokeo ya uchaguzi kwa kutumia mtutu wa bunduki kwa kuwa silaha wanazo.tusikubali.Uamuzi wa walio wengi lazima uheshimiwe.

Leo hii kuna watu wanajinasibu waziwazi kwamba Nchi haitolewi kwa karatasi, sasa tuwaulize wanataka itolewe kwa kutumia nini? demokrasia wameichoka?
 
Back
Top Bottom