Hatari ya Saratani ya Shingo ya Kizazi kwa Wanawake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
1633156235931.png

Mratibu wa huduma ya afya ya uzazi ya baba, mama na mtoto mkoa wa Mtwara Bi Rosalia Arope amefafanua kuwa katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu, akina mama 7,783 walichunguzwa na 100 walibainika kuwa na viashiria vya saratani na baada kufanyiwa uchunguzi zaidi 16 walingundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi huku 43 wakionyesha kuwa na dalili kubwa za ugonjwa huo hatari.

Amefafanua kuwa wanawake walio kwenye hatari zaidi ni wale wenye wapenzi zaidi ya mmoja kutokana na virusi vinavyosababisha saratani ya shingo ya kizazi kubebwa na wanaume, kundi lingine ni wale walioanza tendo la kujamiana wakiwa na umri mdogo, walio zaa wakiwa na umri mdogo, walioathirika na magonjwa ya ngono, Watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa kama Ukimwi, wanao zaa mara kwa mara, uzito mkubwa na kutofanya mazoezi na dalili zake zinaweza kujionyesha kuanzia miaka 10 hadi 15.

Arope anasema kwa kuwa saratani ya mlango wa kizazi ni hatari na miongoni mwa ugonjwa ambao unaondoa maisha ya wanawake wengi hapa nchini ni vyema wanawake wakajijengea utaratibu wa kufanya vipimo ambavyo ni bure katika hatua za mwanzo na kudai idadi kubwa wanaojitokeza kufanya kipimo hiko wanakuwa tayari wameshaathirika.

Malengo ya mkoa kwa mwaka ni kuwachunguza akina mama 117,000 yani sawa na akina 9789 kila mwezi lakini mkoa unashindwa kufikia lengo kutokana na mwamko mdogo wa wanajitokeza kupima na kufikia angalau asilimia 13 ya maadhimio.

DW, imefika katika hospitali ya wilaya ya Mtwara na kuzungumza na Hawa Malindi ambaye ni kaimu mratibu wa huduma za afya kituoni hapo, anaeleza katika halmashauri yao tatizo ni kubwa na katika kipindi cha mwezi januari hadi juni akina mama 2,309 walichunguzwa na 30 walibainika na viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi katika awamu ya kwanza.
 
Back
Top Bottom