Hatari ya Magari ya Serikali barabarani

wiser1

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
2,471
3,646
Habari wakuu, niende moja kwa moja kwenye hoja yangu.

Kunawakati huwa najiuliza tu, watu wenye magari kwenye misafara Kuna haja gani ya kukimbiza magari namna hiyo? Najiuliza hata mwenye nchi anakimbizwa zaidi ya mwizi, hii nchi ni yake Sasa kwanini kukimbizana mpaka najisemeaga tu kufeni ili wengine wajifunze

Ni aibu kubwa kama nchi, huko mabarabarani wenye serikali yao ndo wanaongoza kwa kuvunja sheria za barabarani

Unaweza uliza ukajibiwa kwasababu za kiusalama, hizo sababu za kiusalama ndo Hadi roho za watu zichomoke jaman?

Huwa nasikitika sana! Kwann magari yanakimbia kiasi hiko? Na uwezo wa barabara zetu unajulikana!

Kero ingine ya misafara,
wasafiri wengine kwenye mabasi, magari binafsi wanasimamishwa kupisha msafara, ambao hata wanakokimbilia hakujulikani na hata kinachofanyika hakionekani, Yani vurugu tu saa nzima watu wako barabarani oooh msafara wa waziri, Mara Rais Mara sijui mkuu wa mkoa, mjue tu kwa speed hizo za magari ipo siku nasema ipo siku hii nchi itaingia kwenye janga kubwa la kihistoria.

Serikali tunaomba mjitafakari km ni sahihi kukimbiza magari yenu kwa speed Ile kubwa na yakutisha lakini pia kusimamisha wasafiri wengine zaidi ya saa nzima kwa kisingizio Cha msafara

Mnatukera Sana sisi wananchi
 
Kutana na msafara wa IGP unavyovunja sheria za usalama barabarani hadi kero!
 
Raisi anatembea na msafara mrefu, ukijumuisha mawaziri, ulinzi, wakuu wa wilaya, mkuu wa mkoa husika, wakurugenzi na wakuu wa idara tofauti tofauti.

Msafara wote huu ukisema utembee taratibu kunaweza kuwa na usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri ambako msafara unapita
 
Just imagine una mgonjwa mahututi ndani ya gari unataka kumuwahisha hospitali harafu ukiwa barabarani unaambiwa kuna msafara wa Mkuu fulani!
Anyway ndiyo changamoto za nchi maskini duniani! Tuzikubali tu.
 
Labda Serikali ingepanga kununua na kutumia zaidi helikopta kwa mizunguko ya ndani ya viongozi wakuu!
 
Back
Top Bottom