Hatari ya kuurejesha utumwa na utwana tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatari ya kuurejesha utumwa na utwana tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jambotemuv, Feb 3, 2011.

 1. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Heshma kwenu wachangiaji.
  Wanajamii uarabuni kwa bahati ya miundombinu mizuri ya mawasiliano wameshirikishana nia zao na kusema sasa basi. Hatimaye uma utashinda. Swali labaki. Je? watawala hawa watabadili mioyo?

  Nahisi hapana.
  Wakishafukuzwa kwao wataturudia. Ni kama mashetani wamtokapo mgonjwa. Wakikosa pengine hurudi kwa nguvu zaidi. Waarabu sasa tuwategemee bongo wakiwa na nguvu zaidi kuliko walizokuwa nazo walipotuuza kama watumwa. Miaka ile walitumia vibaraka miongoni mwetu na sasa serikali yetu yaonekana ipo tayari kuwatumikia tena.
  Wafanyayo mafisadi wa DOWNS, EPA, MEREMETA, IPTL etc ni mfano tu wa yajayo.

  Kuyaruhusu haya ni kuwatukana wote walomwaga damu kuupinga udhalimu miaka ile. Ni Kujilaani wenyewe.


  Kuyaazuia tutahitaji zaidi ya mawe na kelele.
  Tutahitaji idadi kubwa ya wazalendo walioelimika kwenye fani mbalimbali.
  Tutahitaji idadi kubwa ya wazalendo wanaomiliki misingi yetu ya uchumi wakilenga kujijenga zaidi hapahapa kwetu na wao.
  Tutahitaji sana utaifa.

  Haya hayapatikani kwa serikali kuwakumbatia mafisadi.
  Hayaji kwa kushusha kiwango cha elimu tufanyavyo sasa.
  Watawala wetu wa sasa yafaa waamke na kuwakabili mafisadi kwa dhati.
  Kuwapigia magoti mafisadi ni kujidanganya.Wakishaukamata uchumi majuto yatakuwa makubwa na kwa marefu.
   
 2. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huu kweli ni ujumbe!!!
   
 3. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ujumbe tumeupata. Naunga mkono hoja zako ila naomba utoe mapendekezo ya nini kifanyike mkuu ili tuyajadili hapa jamvini.
  Karibu tena!
   
 4. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Asante Magafu. Kuuzungumza ujumbe wengi wakaipata picha tunayohofia ni hatua mojawapo. Nahisi viongozi wengi hawatafakari matokeo ya mapuuza wafanyayo sasa. Tuhimize kila mmoja kwa ushawishi wake anapoweza swala la KATIBA libane mianya mingi ihusuyo umiliki wa maliasili zetu na nyanja za uchumi. Kwa hali ya sasa kila kichaa awae madarakani ana nafasi kubwa ya kughilibiwa na kugawa ardhi na mbuga zetu kwa waliotutesa zamani.
  Tuhimize kuachana na usanii kwenye elimu. Badala ya lundo la shule za kata tuimarishe zilizo kamili. Badala ya shule nyingi, mfumo wa usafiri ukiboreshwa ni rahisi na bora zaidi.
  Tuseme na vijana wetu majumbani wautambue ujinga wa sasa na kuuchukia kama tulivyolelewa zamani kuuchukia ukaburu, ubeberu nk.
  Tuwashawishi watoto waitamani elimu na kutumia kila nafasi waionayo sasa kuipata elimu.
   
 5. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Mizizi ya utumwa ipo kichwani kwa mtumwa mwenyewe.
  Watanzania walio wengi hawajui kwamba wanaweza kudhibiti hali zao ngumu za maisha kwa kupambana na ufisadi, viongozi wabovu wasiojali maslahi ya taifa, wageni kuibia nchi n.k.
  Mafisadi ni wachache lakini watetezi wao ni wengi.
  Utumwa wa kifikra bado upo!
   
 6. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Haswaaa. Utumwa wa fikra ndo unawafanya viongozi wetu walokosa utaifa kuwapigia magoti wale wanaotafuta kila njia wazirudie maliasili zetu. Ulemavu wa fikra unawatuma kumilikisha urithi wetu kwa wabaya wetu kwa tamaa za ubinafsi. Ndo maana twahitaji kupanda mbegu za kujitambua kwenye vichwa vya watoto wetu watambue walichoporwa au wanachoweza kuporwa. Zaidi ni kutumia kila upenyo uliopo kuhimiza UKARABATI WA KATIBA.
   
 7. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Umenena! Nimekugongea thanks vile vile:)
   
 8. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watwana muliuzana wenyewe kwa wenyewe kwa wazungu wala waarabu hawahusiki. Mbona hatuoni watu weusi wengi ktk nchi za kiarabu? Mbona marekani kuna watu weusi wengi? Munapotaja uarabu na kuuhusisha na utumwa ni uongo na unafiki. Lengo lenu ni kuupaka matope uislam. Hapa tumeshawajua wanafiki wakubwa nyie
   
 9. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Uislamu umeingiaje hapa?
  Kama na wewe umemaliza walau darasa la saba Tanzania, basi mawili. Shule hiyo hawafundishi historia, au wewe ni uzao wa vibaraka wa waarabu hao.
  Asojua mateso waarabu walowapa watumwa tangu kuwakamata huku, mpaka kuwatumikisha walikouzwa ni nani? Kasome historia utajua pia wanaume walihasiwa ili watumwa wasizaliane. Wanawake walinajisiwa kwa nguvu na leo tunao chotara debe.
  Unyama walofanya waarabu haukuagizwa na uislamu. Tutayalaani milele mauvu yao na hili halitamaanisha kuuchukia uislamu. Sitakushangaa sana kwani wapo hata wanaowachekaga walokufa kwa ajali kadiri watumwavyo na vichwa vyao.
   
 10. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Katika watu wanafiki wakubwa duniani hapa mmojawapo anaitwa Mtabe! Usifikirie ni wewe peke yako ndie mwislamu hapa jamvini. Tupo wengi, lakini kuwa mwislamu si sawa na kuwa mtumwa wa waarabu. Watch your mouth!
   
 11. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Asante Rungu. Nilichagua sana maneno ya kutumia kwa huyu 'Mtabe'. Kawatukana babu zetu kwa yalowakuta. Mateso walopata leo kuyahalalisha kwa kujikomba kwa Waarabu ni aibu mno. Naami ipo siku yatamfika machungu ajutie adabu yake mbaya.
   
 12. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  @ jambo temuv. Nani kakwambia kuwa shule kunafundishwa historia? Kumbe weye unahisi watu hawakusoma kumbe weye ndio hukusoma nimeshakugundua. Maana kama umesoma usingalithubutu kusema eti skuli kunafundishwa historia. Historia gani? Ya kumuabudu nyerere?

  Nimewaambia kua mbona arabuni hatuwaoni hao watu weusi? Wakati wamejaa amerika? Wazungu ndio walio watuma na mababu zenu kwa njaa zao ndio waliowauza wenzao. Hebu angalia utumwa zanzibar ulipigwa marufuku tokea miaka ya 1800s lkn watanganyika mukaendelea kuuzana wenyewe kwa wenyewe mpaka miaka ya 1950s, hapa hujaona tu kua mababu zenu ndio waliowauza wenzao?

  Watumwa waliowakimilikiwa na waarabu walitamani waendelee kubakia utumwani, hata leo hii kuna wazee wa kitwana wanaendelea kuwaheshimu watoto wa kiarabu kwa vile baba zao walikua ni mabwana zao. Munasema nini nyie banaa, sisi tunawaelewa hao waliokua watumwa na wanatwambia kua wanafurahi maisha ya kua mtwana wa mwarabu.

  Tafuteni vitabu vya historia musome musikae na propaganda za nyerere tu, yeye keshakufa au hamuamini?
   
 13. Rungu

  Rungu JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 3,873
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Sasa nimekuelewa kuwa wewe ni mmojawapo wa hao wanaotamani kuendela kubakia utumwani. Ok, huo ni uchaguzi wako lakini usitake kumjumlisha kila mtu. We bwa'mdogo usikfikirie kila mtu ni mjinga, ebo!
   
 14. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35

  Wewe MTABE wa wenzio ndo mkasome. Kukusaidia anzia hapa. Kama unyama wote huu wasema wapo waloutamani, wengi tutakuwa na maswali mengi kukuhusu.

  ARAB SLAVE TRADE | Definitive History of the Arab Slave Trade in Africa
  While Europeans targeted men in West Africa, the 'Arab' trade primarily harvested the women of East Africa to serve as domestic slaves, wet nannies and sex-slaves in the infamous harems.

  This trade trickled over millennia is estimated to have taken more than 10 million African via the Eastern route to India,


  By 1839, slaving became the prime Arab enterprise. The demand for slaves in Arabia, Egypt, Persia and India, but more notability by the Portuguese who occupied Mozambique created a wave of destruction on Eastern Africa. 45,000 slaves were passing through Zanzibar every year.

  To satisfy this demand the Arabs hunted deep into the interiors of Africa, they following ancient trails from Bagamoyo, Kilwa, Tanga, where terror and destruction followed in their wake. The Arab plunders met with savage resistance, which meant that the trade had a very high mortality rate. Many documents speak of the roads littered with the weak and the dying, the abandoned and the maimed, left with yokes around their necks. Many as in the case of Tsavo, Kenya became food for lions. Children who became a burden to the coffle gang were brutally murdered in front of their mothers. Slavery in Zanzibar, 500 Years Later (film)
   
 15. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona unaendelea tu kuleta propaganda, za kwenye vitabu bila kutoa ushahidi wa nani hasa kafanyiwa nini na mwarabu gani. Hujibu hoja ya kwanini leo hatuoni watu weusi wengi arabuni? Kwanini amerika na ulaya kumejaa watu weusi?

  Ishu ya kufanya kazi za ndani kwa akina dada sio ajabu kwani mpaka leo hii wanafanya hapa tanzania tena wenyewe kwa wenyewe na wengine wanaomba mungu wapate nafasi ya kwenda kutumika arabuni. Ok inawezekana kua baadhi ya warabu labda waliwadhalilisha watumwa lkn kama walikuepo ni wachache sana na haifai kuwahusisha waarabu wote,

  mimi naomba mujibu hoja. Hivi tanganyika ilikuwa ikitawaliwa na mkoloni gani? Ambae aliendesha biashara ya utumwa? Utakuta kua mjerumani na muingereza ndio waliotawala tanganyika. Mbona walichelewa kupiga marufuku biashara ya utumwa tanganyika lkn zanzibar ilipigwa marufuku mapema zaidi ya miaka 30 halafu ndio ikapigwa marufuku tanganyika?
   
 16. c

  chamajani JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama ktk chain ya kizazi chako kili-associate na utumwa, then ile dhana ya utumwa itavinjari vizazi hata vizazi vijavyo-huyu mtabe anasumbuliwa na utumwa tu ambao kizazi chake kilikuwa part of! Wee mzanzibara gani hta uislam huujui,kwamba anayechukia/kemea utumwa anauchukia uislam? Plz kasome tena historia ya uislam uone namna waarab walivyokuwa ma-giant wa utumwa!
   
 17. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sasa nina wasiwasi hata kusoma kunakupa shida. Vinginevyo umekusudia tu kutetea uovu. Ulidai tusome vitabu. Tumekuletea yaloandikwa umegeuka wataka ushahidi eti mwarabu yupi alimtumikisha mtumwa yupi. Wengi wao kwa sasa wako jehanam na wengine ahera. Tumekujibu kutoonekana weusi wengi uarabuni ni matokeo ya waaarabu kupendelea watumwa wanawake majumbani mwao ambao pia waliwanajisi kwa starehe zao kimwili mafedhuli hao. Sasa umezuka kusema walikuwa wafanyakazi wa ndani kama walivyo hata kwetu. Wafanyakazi hukamatwa na ndugu zao kuuwawa?
  Ila imeandikwa hata waisraeli walipotakiwa kuondoka utumwani, wapo walitaka kubaki Misri wakijisikia wanathaminika kuliko watumwa wengine. Wapishe wanajamvi wasiopenda ufedhuli wa waarabu kurudi Tanzania wajadili hoja.
   
Loading...