Hatari ya Kufanyika kwa Kosa kubwa la kihistoria: Viongozi CHADEMA kutaneni kwa dharura!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,427
Jamani ! chonde chonde! chonde! Viongozi wa CHADEMA,

  • Naomba kwa heshima kubwa Viongozi wa CHADEMA (waandamizi) wakutane kwa haraka kadiri iwezekanavyo, Waridhiane na kuita vyombo vya habari na kuwaeleza maeneno machache tu "Tumeyamaliza, yaliyopita yamepita, tuko pamoja na tunasonga mbele" au maneno yenye maudhui kama hayo.Ni muhimu kuwaona Mbowe, Dr.Slaa na Zitto wakiwa kwenye press conference kwa pamoja huku wakishikana mikono. Nivyema kufanya hivyo bila kupoteza hata dakika. tafadhali sana!
  • Wafute shutuma zote zinazomkabili Zitto bila masharti. Kuhusu wengine wanaokabiliwa na shutuma watumie busara tu kufikiri ni nini wanaweza kufanya.
  • Chonde chonde tafadhali; fanyeni hivyio ikiwezekana leo.Msisubiri zile siku kumi na nne zifike.Fanyeni hivyo kabla tuhuma hizo 11 hazijavuja kwa wananchi na kujadiliwa. Mkichukulia masikhara, Muda si mrefu linaweza kutokea kosa kubwa sana la kihistoria litakalobadilisha kabisa historia ya chama chetu na kukifanya kionekane kwa sura tofauti kabisa.Chonde chonde viongozi wa chama fanyeni hivyo kukinusuru chama tafadhali.
  • Mtu anaweza kusema hatuwezi kuwachagulia viongozi chakufanya: Tafadhali sana: naomba tusilaumiane, kuzozana au kuendelea kunyosheana vidole katika wakati huu.Tufanye hili kwanza halafu ndo tuendelee na mengine.Ni hatua ya dharura!
Tumieni busara kufikiri hili ninalolisema. Ninyi ndio mmeandika tuhuma 11, zinazowakabili Zitto na wenzake na mnazijua vizuri na mnafahamu mengi. Kadhalika nina uhakika mnapata idea ya ninachokisema.

Nawahakikishieni:
Nina akili timamu wakati huu naandika hapa, nina nia njema na nimefanya utafiti wa kutosha kabla ya kuongea ninachoongea. Ukali wa kichwa cha habari hapo juu ni halisia na sio kuigiza. Tafakarini kwa haraka na kuchukua hatua tafadhali sana sana!
 
Ushauri wako ni mzuri sana ila kumbuka taasisi inapoaamua jambo zito kwa manufaa makubwa huwa imejiridhisha vya kutosha.

wish maamuzi yale yangekuwa ya mtu binafsi ila ni maamuzi ya kamati kuu,pamoja na kwamba inaongozwa na binadamu kama ww ila pia inamisingi yake na taratibu zake ni vzr tuziheshimu.

Since hii platform ina watu wenye hekima bs watakuja na mazuri zaidi ya kuboresha tahadhali yako,kikubwa nikuacha uoga na kuface reality,sisi wanachama tuko tayari kwa lolote litakalotokea kwa hali yoyote ile,ukiyaogopa maisha utakuwa mtumwa
 
Prof. Baregu na mwengine yeyote atakaeweza: jaribuni ku modarate maridhiano hayo kwa weledi na nguvu zenu zote.Tangulizeni nia njema na dhamira ya kufikia muafaka mwema.Nawaombeni sana sana! Mh.Mbowe, Dr.Slaa, Zitto na wengineo, ziwekeni hisia zenu katika lengo na mtizamo wa maridhiano na kusameheana. Tangazeni kusameheana kwa moyo mmoja.Zilazimisheni nafsi zenu kusameheana hata kama hazitaki. Hii ndio njia pekee yenye faida kwa dakika au masaa machache sana yaliyobakia kunusuru hali ya mambo.

Tafadhali sana viongozi! chonde! chonde!
 
Sasa na wewe unatuzingua... hebu nenda zako huko...
 
Ushauri wako ni mzuri sana ila kumbuka taasisi inapoaamua jambo zito kwa manufaa makubwa huwa imejiridhisha vya kutosha.

wish maamuzi yale yangekuwa ya mtu binafsi ila ni maamuzi ya kamati kuu,pamoja na kwamba inaongozwa na binadamu kama ww ila pia inamisingi yake na taratibu zake ni vzr tuziheshimu.

Since hii platform ina watu wenye hekima bs watakuja na mazuri zaidi ya ili kuboresha tahadhali yako,kikubwa nikuacha uonga na kuface lolote litakalotokea kwa hali yoyote ile.
Mkuu tunaheshimu na tutaendelea kuheshimu maamuzi ya kamati kuu. Ni nachokisema sio kuvunja maamuzi ya kamati kuu bali kufikiri tofauti kwa sababu za dharura. Hiyo kamati kuu ikibidi na ihusishwe vile vile. Mkuu kuna mambo mengi nimeyagundua mkuu ila naomba nisiyaweke hapa kwa sababu za kiuadilifu na nikiyaweka hapa yatavuruga maridhiano. Kwa sababu hiyo naomba tu utumie historia yangu kufikiri umuhimu wa ninachokisema.Naomba tu tuaminiane ndugu yangu. Zaidi ya hapo, kama tuko tayari la kutokea litokee basi bwana! dunia yetu chaguo letu.
 
Ushauri wako ni mzuri sana ila kumbuka taasisi inapoaamua jambo zito kwa manufaa makubwa huwa imejiridhisha vya kutosha.

wish maamuzi yale yangekuwa ya mtu binafsi ila ni maamuzi ya kamati kuu,pamoja na kwamba inaongozwa na binadamu kama ww ila pia inamisingi yake na taratibu zake ni vzr tuziheshimu.

Since hii platform ina watu wenye hekima bs watakuja na mazuri zaidi ya kuboresha tahadhali yako,kikubwa nikuacha uoga na kuface reality,sisi wanachama tuko tayari kwa lolote litakalotokea kwa hali yoyote ile,ukiyaogopa maisha utakuwa mtumwa

Nakubaliana na wewe kwa asilimia miamoja, kwani watu wengine wamejaa hofu ambayo haina msingi. Hayo ni maamuzi ya Kamati Kuu, ni maamuzi ya watu wengi na ambao wameaminiwa na wanachama wa CDM kwahiyo sidhani kama kunatatizo lolote.
 
hamna. betlehm yuko sahihi kwa faida ya chama wakae chini tena na wa vunje ukabira kama hawataki watapata pigo
 
Ndugu Mbona unaangaika sana? Hivi unataka CHADEMA iendelee kuwepo ikiwa vipande vipande ili MUNGU saidia 2015 wamechukua nchi waka Iv unje Tanzania Vipandevipande? Hivi huoni hii ni faida kubwa sasa tumewajua walivyo na kama kufa bora wafe sasa kuliko kuja kuiua Tanzania?
 
Sasa na wewe unatuzingua... hebu nenda zako huko...
Mkuu Tuko samahani kama nimekukwaza. Naomba unisamehe halafu nitakuja kukupa habari zinazonisukuma leo hii niseme hivi hapo baadae kidogo.Naomba uniamini.Ila kama nafsi yako inakataa kuniamini basi samahani Ila baada ya muda utakuja kufahamu nilikuwa nasema nini.Elewa wakati fulani, mapenzi au chuki huweza kumziba mtu macho asione ulimwengu katika uhalisia wake. (aone mambo kama alivyo yeye badala ya kuona mambo kama yalivyo)
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Betlehem

Labda nikwambie tu kuwa chadema ni taasisi sio Slaa au mbowe,

Maamuzi yoyote yale ysnafanywa kwamjibu wa katiba na miiko ya chama,

Zitto na wahuni wenzake sio watu wakwanza kuchukuliwa hatu na vyama vya siasa,

Ccm katika kipindi cha miaka nane tu imebadili makatibu zaidi ya wanne ilihali katiba inataka kiongozi wa chama hicho ahudumu kwa miaka kumi.

Chadema ilishafukuza katibu wake "mkuu" lakini hakukuwa na kinachoitwa maridhiano,

Hivi unafanyaje maridhiano kwa maamuzi halali ya chombo halali cha chama?

Haiingii akilini eti katiba iwekwe kando na maneno ya vinywani (vijiweni) yashike hatamu.

Tuache porojo, tusimamie katiba na sheria na tuheshimu maamuzi halali ya mamlaka zetu.
 
Mkuu tunaheshimu na tutaendelea kuheshimu maamuzi ya kamati kuu. Ni nachokisema sio kuvunja maamuzi ya kamati kuu bali kufikiri tofauti kwa sababu za dharura. Hiyo kamati kuu ikibidi na ihusishwe vile vile. Mkuu kuna mambo mengi nimeyagundua mkuu ila naomba nisiyaweke hapa kwa sababu za kiuadilifu na nikiyaweka hapa yatavuruga maridhiano. Kwa sababu hiyo naomba tu utumie historia yangu kufikiri umuhimu wa ninachokisema.Naomba tu tuaminiane ndugu yangu. Zaidi ya hapo, kama tuko tayari la kutokea litokee basi bwana! dunia yetu chaguo letu.

Mkuu kama mbwai acha iwe mbwai,huwezi batilisha uamzi wa kamati kuu kisa kuna baya linataka tokea,chadema sio chama cha upinzani tu bali ni mwalimu wa democrasia hapa nchini.

Kumuogopa mtu mmoja ni ujinga na upumbavu,kuna watu kipindi mwalimu anafariki walisema nchi inakufa leo mbona mimi na ww tuko hapa na nchi iko imara?

tuacheni uoga,tuface challanges ili tuwe imara zaidi.

kama zito alikuwa na nia ya kuiboa cdm bs acha atimizi malengo yake,ila kama hakuwa na nia hyo bs ataisimamisha chadema zaidi ya hapa ilivyo sasa
 
Ndugu Mbona unaangaika sana? Hivi unataka CHADEMA iendelee kuwepo ikiwa vipande vipande ili MUNGU saidia 2015 wamechukua nchi waka Iv unje Tanzania Vipandevipande? Hivi huoni hii ni faida kubwa sasa tumewajua walivyo na kama kufa bora wafe sasa kuliko kuja kuiua Tanzania?
Mkuu tatizo la msingi ndani ya CHADEMA kwa sasa ,ni tatizo la kutengenezwa na sio tatizo halisia.Kuridhiana ndio kujenga, ndio kuunganisha, ndio kupatana na kinyume chake ndio kugawanyika, kugombana kuzozana n.k mkuu kibanga usinisukume nikaongea kitu ambacho sitaki kukiongea. naomba kama unaniamini niamini.Maridhiano kwa sasa ni jambo muhimu kuliko kitu kingine chochote. Zaidi ya hapo kama tunaamua liwalo naliwe, basi dunia yetu, chaguo letu.
 
Mkuu, mbona huonyeshi huo umuhimu wa kukutana kwa dharura? Umepiga lamri ama umeota vibaya nini? Thread imekaa kinajimu najimu hivi... kama walimu aka majini yamepanda kamanda.
Ok mnafiki MM ni wakutoa chamani.

Mtoa hoja katoka mirembe,ila kanuni ya maridhiano ni mkosaji kuomba msamaha. Zitto kajaa jeuri na kiburi,hata wakiridhiana hawataweza kufanya kazi pamoja.Namshauri zitto aende cuf.
 
Jamani ! chonde chonde! chonde! Viongozi wa CHADEMA,

  • Naomba kwa heshima kubwa Viongozi wa CHADEMA (waandamizi) wakutane kwa haraka kadiri iwezekanavyo, Waridhiane na kuita vyombo vya habari na kuwaeleza maeneno machache tu "Tumeyamaliza, yaliyopita yamepita, tuko pamoja na tunasonga mbele" au maneno yenye maudhui kama hayo.Ni muhimu kuwaona Mbowe, Dr.Slaa na Zitto wakiwa kwenye press conference kwa pamoja huku wakishikana mikono. Nivyema kufanya hivyo bila kupoteza hata dakika. tafadhali sana!
  • Wafute shutuma zote zinazomkabili Zitto bila masharti. Kuhusu wengine wanaokabiliwa na shutuma watumie busara tu kufikiri ni nini wanaweza kufanya.
  • Chonde chonde tafadhali; fanyeni hivyio ikiwezekana leo.Msisubiri zile siku kumi na nne zifike.Fanyeni hivyo kabla tuhuma hizo 11 hazijavuja kwa wananchi na kujadiliwa. Mkichukulia masikhara, Muda si mrefu linaweza kutokea kosa kubwa sana la kihistoria litakalobadilisha kabisa historia ya chama chetu na kukifanya kionekane kwa sura tofauti kabisa.Chonde chonde viongozi wa chama fanyeni hivyo kukinusuru chama tafadhali.
  • Mtu anaweza kusema hatuwezi kuwachagulia viongozi chakufanya: Tafadhali sana: naomba tusilaumiane, kuzozana au kuendelea kunyosheana vidole katika wakati huu.Tufanye hili kwanza halafu ndo tuendelee na mengine.Ni hatua ya dharura!

Tumieni busara kufikiri hili ninalolisema. Ninyi ndio mmeandika tuhuma 11, zinazowakabili Zitto na wenzake na mnazijua vizuri na mnafahamu mengi. Kadhalika nina uhakika mnapata idea ya ninachokisema.

Nawahakikishieni: Nina akili timamu wakati huu naandika hapa, nina nia njema na nimefanya utafiti wa kutosha kabla ya kuongea ninachoongea. Ukali wa kichwa cha habari hapo juu ni halisia na sio kuigiza. Tafakarini kwa haraka na kuchukua hatua tafadhali sana sana!
Wewe una akili sana lakini wale ma-F4F hawatakuelewa.
Jana Mnyika kaongea nini sijui, watu wakifikiri atasaidia kutatua tatizo linaloikabili CHADEMA yeye kaongea mambo ya kufikirika ambayo wala hayaingii akilini, kwa kulifikiria jiwe lililo shingoni mwa chama chenu.

Sisi wengine wa buku 7 hatutaki kulumbana na ma F4F bali watu ambao shule imepanda.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom