Hatari ya kiongozi wa mhimili bunge kuwa rubber stamp wa mhimili serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatari ya kiongozi wa mhimili bunge kuwa rubber stamp wa mhimili serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Jul 1, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hali ya nchi ni tete,ni tete kwa kuwa tu mhimili wa bunge umeshindwa kuisimamia serikali kama katiba inavyozungumza kwenye ibara ya 63 (2) inayosema bunge ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka,kwa niaba ya wananchi,kuisimamia na kuishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu ya katiba hii. Leo hii bunge hili lililopewa meno kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano linakiuka kwa makusudi majukumu yake kwa kuwa tu kiongozi wa bunge ambaye ni Spika ana toka chama tawala cha CCM.Bunge hili limekuwa chombo cha kukandamiza demokrasia kwa vyama vyenye wabunge wachache bungeni. Ukiwa na bunge kama hili,ufisadi ndani ya serikali hutamalaki na bunge kugeuzwa sehemu ya mipasho ama kupoteza dira na mwelekeo wa bunge.Tumeona mambo mengi yanayotokea ndani ya mjengo huo kiasi cha kupelekea serikali kuwasahau wapiga kura wake kwa kuwa tu kuna watu wamejazana ndani ya bunge kwa maslahi ya kupitisha bajeti za kifisadi na mambo ovyo ovyo yasiyo na tija kwa wananchi. Kuna tofauti gani kati ya bunge letu na ze comedy,japokuwa ze comedy kazi yao ni kutufurahisha na kutuburudisha.Inawezekanaje kwa bunge makini na wabunge wake kuunga hoja asilimia mia moja,lakini ndani ya mchango wake unaikataa bajeti.Ukifika wakati wa kupiga kura kupitisha bajeti hiyo kinachongaliwa maslahi ya chama. Niliwahi kusema ni bora wananchi tutafute kanuni ambayo itatuwezesha kupiga kura ya kutokuwa na imani na bunge hili kwa kushindwa kutuwakilisha vema kwa maslahi ya taifa letu.Leo hii waziri mkuu ana thubutu kusema wameshazungumza na mihimili mingine,mahakama na bunge.Nini maana ya mazungumzo hayokama si serikali kutoa maagizo na kuingilia madaraka ya mihimili inayojitegemea . Hali kama hii inaleta picha halisi ni jinsi gani serikali inatumia mihimili hii katika kubaka demokrasia.Uzembe unaonyeshwa na bunge ni chanzo kikubwa cha kuwa na serikali dhaifu isiyo jali hali za wananchi wake.Hali hii imesababisha serikali kutokuwa makini pamoja na interejensia yake kupitia vyombo vyake vya usalama kushindwa kudhibiti matukio ya uvunjifu wa amani ndani ya taifa letu. Tusitegemee hata siku moja bunge hili la CCM litakuja kusimamisha shilingi kwa maslahi ya wananchi na bunge kuvunjwa ili kuitisha uchaguzi.Hali kama hii ndiyo inapelekea wabunge toka CCM kuwa mavuvuzela ndani ya bunge kwa kuhofia kutokurudi au kushughulikiana ndani ya chama. Ukweli utabaki kuwa ukweli,ila cha msingi tusifanye makosa kewnye kutoa maoni yatakayo pelekea kupata katiba yenye meno na itayotanguliza Tanzania na wananchi wake kwanza.Bunge hili chofu linaingia kwenye Guinness book of record kwa kuwa bunge lililoshindwa kuisimamia serikali na linaloridhia uuzwaji wa taifa letu kwa gharama ya bure.Ni heri na Sultani Mangungo amabye hakuwa na elimu kuliko bunge letu lilivyo kwa sasa. Napenda kuwakaribisha wana JF tushirikiane kuangalia ni sheria ipi au kanuni itakayo tuwezesha kupiga kura ya kutokuwa na imani na bunge hili.Mungu inusuru Tanzania yetu.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ah stori za bungen kwa sasa zinatia kinyaaaa,,,bora stori za kahawa k'koo ,,,,tuendelee kuangalia euro
   
 3. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  bunge kule wanapiga story tu ukiangalia unasikia kinyaa hamna wanachofanya zaidi ya kula kodi zetu kila siku mambo ni yaleyale kama ahadi za jk eti mtu mwenye akili hawezi akatoa ahadi asitimize.....
  mpaka sasa italy wameshafungwa bao 4
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Stori nzuri ya bungeni ni ile ya bajeti ya upinzani yenye income "0".

  Zitto kawatia mkenge au ma software aliyoweka Josephine pale ofisini hayaoneshi mapato?
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Anne Makinda ameharibu bunge vibaya sana. Na kama wabunge wa CCM wangekuwa na busara kidogo tu wangekaa chini na kurekebisha mambo kabla ya kiama kuwafikia 2015. Kosa kubwa na ambalo historia haitamsamehe Makinda ni kugeuza bunge, chombo cha wawakilishi wa wanachi kuwa sehemu ya serikali! Hili ni kosa la kihistoria. Anatumia nguvu kubwa sana kuziba wabunge mdomo.

  Kwa bahati mbaya amejiaminisha kuwa anaweza kuficha huu mkakati hasi wa kubaka demokrasia kwa kutumia kanuni za bunge! Kila leo amekuwa anarudia rudia kanuni za bunge, hivi ni yeye tu ndiye anayezielewa? Kma hii si kukejeli wabunge na kuwa-treat kama watoto ni nini? Na iwaje matumizi ya hizo kanuni yawe very subjective?

  Pili, Spika haonekani kuwa na ubunifu wowote unaweza kulifanya bunge liendane na fikra na matarajio ya watanzania wa sasa. CCM walifanya makosa kuangalia sifa ya jinsia kama kigezo, lakini wako hatarini kuzama kutokana na madhaifu yanayojitokeza sasa hivi kwenye uendeshwaji wa vikao vya bunge. Hii itakuwa gharama kubwa sana kwa wabunge wa CCM na hata ilivyo sasa mambo ni magumu kwao huku uraiani. Lakini wanastahili kwa lolote maana ndio wanampa mapembe huyu mama sasa ngoja awachimbie kaburi.

  Tatu, Bunge linatizamwa na watu wengi wakiwemo watoto wa shule hivyo ni vema wabunge wa CCM wakajua wanayo responsibility ya kutotoa maana potofu juu namna ya kuchangia hoja. Mbunge anasema anaunga mkono hoja 100% baada ya hapo anaanza kukosoa! Huu ni udhaifu wa elimu. Huwezi, kwa mfano, sema kuwa nyumba imekamilika kwa 100% hapo hapo ukasema kuna vyumba viwili bado vina havina madirisha, au hakuja sink jikoni! Au CCM wana tafsiri nyingine ya 100%? Inakuwaje wabunge zaidi ya 200, tena wengine wana degree daraja la kwanza wanashindwa kuona huu 'primitive' wa kuchangia hoja? Aibu sana.

  Kwa maoni yangu wabunge wa CCM ambao ndio majority wakae chini na kuja na plan juu na namna bora ya kuendesha vikao vya bunge before it is too late. Na pia wahakikishe mtindo wa kuficha report za kamati za bunge kama ambavyo Spika amefanya kwa kamati ya huduma za jamii unaachwa mara moja. Watanzania wa sasa hawataki mzaha, hawana muda wa kuendekeza maujanjajanja kwa kisingizio chochote kile, na kwa hakika hawana tena subira kwenye kufanya maamuzi. Lakini wakiacha hali ikaendelea kama ilivyo watazama. Jenista Mhagama ana afadhali sana pengine wanaweza kuchukua notes kwake. Lakini Spika, naibu wake na yuke Mabumba kuna mambo mengi ya kurekebisha. Uchaguzi ni wenu CCM.
   
 6. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tutaendelea kuendeleza CCM utopia hata kwa mambo ya msingi,tunazungumzia bunge zembe mwingine ana sema bajeti ya upinzani lete thread tuchangie,CDM Wapinzani hawana serikali,hawa kusanyi kodi ndio maana hata incom ipo 0% tatizo liko wapi?
   
Loading...