Hatari: Wawekezaji kuikimbia Tanzania

barwani

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
238
160
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa ameeleza kunasa mpango wa nchi za Ulaya kuiingiza Tanzania katika orodha ya nchi hatari kwa uwekezaji (Risky investiment destination).

Dk. Slaa ambaye hivi sasa anaishi nchini Canada, ameliambia gazeti la Mtanzania mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa endapo Tanzania itaingia kweli katika orodha hiyo itaathirika hususani katika sekta ya mafuta na gesi biashara na utalii.

Wanajamvi kama mambo yatakua hivi nchi itakua katika hali ngumu sana, tatizo la watanzania tunapenda kuambiwa mambo mazuri tu, mfano ishu ya MCC ni pigo kubwa sana kwa Taifa, ila kwakua watawala wanajua kasumba ya watanzania ni kufarijiwa na kuambiwa mambo matamu, wapo waliowaamini watawala na kuona MCC sio janga.

Si walaumu ila wameaminishwa kupitia lundo la makusanyo ya wakwepa kodi,.Nchi bado haijafikia kua na kiburi cha kutohitaji misaada,takwimu nyingi ni za kupikwa kufurahisha raia.Japo rais anaonekana kupiga kazi ila bado nchi inaendeshwa kiujanja ujanja na sanaa za hapa na pale.
 
Ni kweli ni nchi hatari kwa uwekezaji kwasababu hakuna uwazi ktk mikataba ya uwekezaji.

Tangu uwekezaji umeanza ni watu wachache kupiga dili ikiwemo viongozi wakuu wa nchi na kuwaacha wananchi wake taabani.

Nasikitika sana tumebakia na mashimo wajanja wamepiga hela na kuondoka zao.
 
Hata tulionao wawekezaji wanatuibia tu hawana msaada kwetu.wanatusainisha mikataba mibovu.nafasi nzuri zinachukuliwa na wafanyakazi toka kwao.hawana uchungu na nchi yetu.Taifa litajengwa na sisi wenyewe
 
Mbona kwa boko haramu sio risk kuwekeza kwenye mafuta,? Na wapo huko Abuja wanawekeza
 
Hata tulionao wawekezaji wanatuibia tu hawana msaada kwetu.wanatusainisha mikataba mibovu.nafasi nzuri zinachukuliwa na wafanyakazi toka kwao.hawana uchungu na nchi yetu.Taifa litajengwa na sisi wenyewe
Elimu yetu kupata ajira huko migodini ndogo na tamaa sna watu wanalipwa vizur lkn bado anataka kupiga hela ndo tatizo na anaesoma international school ndo best lawyers na utawala anaesoma engineering ndo mtendaji kazi anajua sema kujieleza kwa lugha ile ya malikia ndo shidah ila tuombe tufike salama
 
Dalili za nchi kuwa hatari kwa wawekezaji zimeisha anza kuonekana hasa kitemdo cha mashirika ya serikali kama TANESCO kutolipia huduma wayopata kutoka kwa wawekezaji kama mikataba yaao ilivyo. Kwa sasa wameshindwa kulipa kabisa madeni ya umeme wanaopata toka Songas Mpaka Songas wamelazimika kuzima mashine zao tatu (UGT 1, 2, 3) hadi walipe na nyingine zaweza kuzima kama wakiendelea kukaidi. Uwenda wawekezaji wengine katika sekta ya gesi wanaweza kufunga valve za gesi hadi walipwe maana na wao wanaidai sana. Halafu prof anawaabia ANESCO wapungeze bei ya umeme wakati wanakabiliwa na madeni makubwa sana. I think we need economics Prof and not a Geology Prof to drive the economy backbone of this country!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sijui kama watu wanaelewa hasa maana ya hii habari.

Wakati wa utawala wa JK, uwekezaji ulipungua sana, na wawekezaji wengi katika sekta ya madini waliondoka. Makampuni karibia 160 yaliyokuwa yanafanya utafiti wa madini Tanzania yalisimamisha shughuli za utafiti. Makampuni hayo hayakuwa yanaingiza faida yoyote maana yalikuwa hayachimbi wala kufanya biashara zaidi ya kufanya utafiti, kazi ambayo ina hatari kubwa (business risk). Unapofanya utafiti katika madini risk ya kupoteza pesa ni 99.90%. Kwa wastani katika vitalu 1000 vya utafiti wa madini ya dhahabu Duniani ni kitalu kimoja tu ndiyo kitakuja kuwa na mgodi mmoja wa dhahabu. Wawekezaji katika vitalu 999 watakuwa wamepoteza hela yao. Ndiyo maana kampuni ndogo haziwezi kufanya utafiti. Tanzania hakuna hata kampuni moja yenye uwezo wa kufanya utafiti wa madini kutokana na hofu ya kupoteza pesa. Katika Afrika ni kampuni za kimataifa za Afrika Kusini na Nigeria ndiyo zinazofanya utafiti wa kiwango fulani.

Makampuni haya zaidi ya 160 ya utafiti yalikuwa yanalipa karibia U$320 milioni kwa mwaka kama malipo ya leseni (application, processing na rental, PAYEE, professional levy, n.k.). Lakini pia yalikuwa yanaajiri si chini ya watanzania wapatao 3,200 ambao mishahara yao ilikuwa kati ya TZS 600,000 - 20,000,000 kwa mwezi. Makampuni haya yalikuwa yamepanga katika majengo mbalimbali ya Watanzania na yakilipa kwa dola, wageni waliokuwa wanakuja kwa program maalum walikuwa wakifikia kwenye mahoteli wakilipa kwa pesa za kigeni. Wageni hawa walikuwa wakitumia ndege kutoka kwao na wawapo ndani ya nchi. Baadhi ya makampuni yalikuwa yakikodi magari ya watanzania na kuwalipa kati ya U$120-180 kwa siku.

Mwaka 2013, kulikuwa na uvamizi mkubwa wa wachimbaji wadogo kwenye maeneo ambayo makampuni haya yalikuwa yamepewa leseni za kufanyia utafiti. Makampuni yalipokuwa yanafanya utafiti, wakigundua tu kuwa kuna dhahabu, wachimbaji wadogo walikuwa wanavamia, wachimbaji wadogo wakishaanza kuchimba walikuwa wakichangishana ili kupata pesa za kwenda kuhonga mamlaka mbalimbali ili wasiondolewe kutoka kwenye maeneo waliyoyavamia. Viongozi wa mikoa, wilaya, Waziri Mkuu na Rais hawakuweza kusimamia sheria, na maeneo mengi makampuni ya kigeni yaliamua kufunga shughuli za utafiti.

Mwaka 2014, taasisi ya biashara ya Australia iliitangaza Tanzania kuwa siyo mahali salama pa kuwekeza mitaji ya nje kwa sababu hakuna Rule of Law, kuna makampuni yaliyowekeza Tanzania yalipoteza pesa nyingi kutokana na thamani ya hisa zao kuanguka kwa kiasi kikubwa katika masoko ya fedha Duniani kwa kuwekeza sehemu hatari. Mpaka sasa ni ngumu sana kupata pesa kutoka masoko ya fedha kama ya Sydney kuja kuwekeza Tanzania. Ikumbukwe kuwa Australia ni kati ya wawekezaji wakubwa kwenye sekta ya madini. Wawekezaji wa mataifa kama Hongkong huwekeza Tanzania kupitia Australia kwa sababu ambazo muda hautoshi kuelezea hapa. Makampuni haya kwa sasa yameelekeza zaidi uwekezaji wao Afrika Magharibi, Amerika Kusini na China.

Nakumbuka nilipokuwa Sydney kwenye conference ya upatikanaji wa mitaji, nikiwa mtu pekee toka Afrika, mmoja wa matajiri wakubwa wa Australia, aliniambia amewahi kufika Tanzania, amewahi kuetembela Serengeti, amewekeza tanzania, na akaongeza kusema, 'Tanzania is a good country, we may consider getting back to Tanzania after 2015 election, believing you guys will bring a capable government'.

Watanzania tusidanganyane, tunahitaji uwekezaji mkubwa kutoka kwa watu wenye mitaji mikubwa toka mataifa mbalimbali. China tunayoisifia, kwa miaka mingi ilipojifungia imefurukuta bila mafanikio. Mwishoni ikayakaribisha makampuni makubwa ya Amerika, Kanada na Australia, ndipo uchumi wao ulipoanza kupata afya, leo wachina wanatudanganya kuwa uchumi wetu unaweza kukua haraka kwa kuwaruhusu wao waje kuwekeza kwetu. China mpaka leo hii haiwezi kuchimba gas kutoka kwenye maji ya kina kirefu, China haina uwezo wa kutengeneza mitambo ya kuchimbia gas kwenye maji ya kina kirefu. Nchi pekee yenye uwezo wa kutengeneza mitambo hiyo ni Marekani. nchi pekee zenye uwezo wa kuchimba gas kwenye bahari ya kina kirefu, zaidi ya Marekani ni Sweden na Norway.

Watanzania tukitaka kujitegemea na kupata maendeleo tuutafute ukweli na uhalisia, tusidanganywe kwa ngonjera na nadharia. Wachina wanataka kujifunzia kwetu. Wachina wamepiga hatua lakini kwenye high tech bado sana japo wapo kwenye njia ya kuelekea huko.
 
Mkuu Msambichaka Mkinga kidogo umeelezea kaundani fulani hivi, je umewahi kuandika report ya kidocument kama ulivyooelezea na kuwapelekea wahusika?
 
Tatizo ninaloliona kwa wananchi wengi wa Tanzania ni kutaka maendeleo ya kweli bila kuumia walau kidogo lakini ukweli utabaki palepale kuwa hakuna mapinduzi ya kimaendeleo yafanyikayo bila kuwagharimu wananchi kwa namna yoyote ile .....

Tanzania ilikuwa ni nchi ya deal na dumping economy hivyo, uzibaji wa mianya ya uozo huo lazma kuna impacts zitokee kama upungufu wa bidhaa na ajira kwa wachuuzi wake lakini huu ni mpango mahususi wa kulinda masoko kwa bidhaa za ndani ambapo inaweza kusaidia kufufua viwanda , ajira na hata uanzishwaji wa viwanda vipya kutokana na uhakika wa soko kama chanzo cha faida....

Uwajibikaji na uwazi utasaidia kuondoa mlolongo katika ufanyaji kazi na hivyo kufanikisha mvuto kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi...

Tukubali kuvaa kaniki ili tutengeneze nguo zetu wenyewe na kuacha kuwa taifa LA mitumba

**** TANZANIA KWANZA ****
 
Mkuu Msambichaka Mkinga kidogo umeelezea kaundani fulani hivi, je umewahi kuandika report ya kidocument kama ulivyooelezea na kuwapelekea wahusika?

UKIWAPA RIPOTI HII, KESI YA UCHOCHEZI INAKUHUSU.... SEGEREA BILA DHAMANA....
 
Nafarijika kusoma vitu vya wenye akili kama Msambichaka Mkinga. Tumaini langu ni kuwa wanaohusia wakisoma vitu hivi wana take note. Tanzania imejaa maneno ya uvumi, songi songi na umbea. Ukweli unaotokana na utafiti ni mdogo sana. Asante sana Msambi.
 
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa ameeleza kunasa mpango wa nchi za Ulaya kuiingiza Tanzania katika orodha ya nchi hatari kwa uwekezaji (Risky investiment destination).

Dk. Slaa ambaye hivi sasa anaishi nchini Canada, ameliambia gazeti la Mtanzania mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa endapo Tanzania itaingia kweli katika orodha hiyo itaathirika hususani katika sekta ya mafuta na gesi biashara na utalii.

Wanajamvi kama mambo yatakua hivi nchi itakua katika hali ngumu sana, tatizo la watanzania tunapenda kuambiwa mambo mazuri tu, mfano ishu ya MCC ni pigo kubwa sana kwa Taifa, ila kwakua watawala wanajua kasumba ya watanzania ni kufarijiwa na kuambiwa mambo matamu, wapo waliowaamini watawala na kuona MCC sio janga.

Si walaumu ila wameaminishwa kupitia lundo la makusanyo ya wakwepa kodi,.Nchi bado haijafikia kua na kiburi cha kutohitaji misaada,takwimu nyingi ni za kupikwa kufurahisha raia.Japo rais anaonekana kupiga kazi ila bado nchi inaendeshwa kiujanja ujanja na sanaa za hapa na pale.
Amesema sababu ni nini za kuiweka Tz kwenye risky investiment destination?
 
Sio kwel bana...em achen ku2tsha,hao wawekezaj wenyewe wana njaa hawanauwezo wa kuzgomea fursa!!
 
Back
Top Bottom