HATARI: Wanafunzi shule ya msingi Ukombozi wakiziba paa la darasa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Hii ni hatari kwa wanafunzi kufanya kazi ya kuziba paa la shule wakati hii kazi inatakiwa kufanywa na mafundi wenye utaalam katika kazi hii.

Ikitokea watoto hawa wamedondoka katika paa hili lenye bati zenye kutu nani wa kulaumiwa..? Watoto wenyewe sioni wakiwa wamezingatia suala la usalama, wamejipandia tu kwenye paa.

Tuwaache watoto wasome, walimu kuzibiwa mianya yenu ya michango ya wizi wizi isiwe chanzo cha kunyanyasa wanafunzi.

SWALI: Suala la ukarabati wa shule za UMMA ni jukumu la nani?

Ukombozi.png

13165884_775861525848605_8440964223660371016_n.jpg
 
khaaaaa wakiumia hapa nani anawajibika? wakifa utasikia bahati mbaya, aisee hasira zimenikaba ghafla sana..............
 
Hii ni hatari kwa wanafunzi kufanya kazi ya kuziba paa la shule wakati hii kazi inatakiwa kufanywa na mafundi wenye utaalam katika kazi hii.

Ikitokea watoto hawa wamedondoka katika paa hili lenye bati zenye kutu nani wa kulaumiwa..? Watoto wenyewe sioni wakiwa wamezingatia suala la usalama, wamejipandia tu kwenye paa.

Tuwaache watoto wasome, walimu kuzibiwa mianya yenu ya michango ya wizi wizi isiwe chanzo cha kunyanyasa wanafunzi.

SWALI: Suala la ukarabati wa shule za UMMA ni jukumu la nani?

View attachment 344993

View attachment 344994
Mbaya sana ebu niambie hiyo shule ya Ukombozi iko eneo gani Temeke nikawashughulikie?
 
Ukombozi ya Singida mjini au ya wapi mwandishi? Kamilisha habari tufahamu maana zipo Ukombozi nyingi.
 
Mleta mada baada ya kuwaona hao watoto wapo kwenye hatari ulichukua hatua gani ili kuwanusuru na hatari ambayo ingeweza kuwagharimu maisha yao? Au uliwapiga picha tu na kukimbilia JF kuanzisha uzi?

Sijakulaumu kuanzisha huu uzi ila ninachouliza ulichukua hatua gani kuwanusuru hao watoto kabla ya kuja JF na huu uzi?
 
Ndio vizuri wanajifunza stadi za kazi, sio wanamaliza chuo wanazunguka miaka 2 na bahasha wanatafuta ajira. Wakitoka hapo ni kujiajili tu good.
 
Back
Top Bottom