HATARI: Wahalifu wadaiwa kupewa ulinzi Bahari ya Hindi

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,171
2,000
Taarifa iliyotolewa leo na magazeti, inaeleza kuwa kuna maofisa wa polisi wanashirikiana na matajiri wakubwa wahalifu kuingiza mizingo ya hatari kupitia njia za panya, maeneo ya vukwe za bahari yetu ya hindi, pia wameleza kuwa kazi inafanyika usiku wa manane kwa ulinzi wa polisi. My take: je jeshi letu la polisi limekuwa genge la wahalifu wa nchi hii?
 

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,246
2,000
Baada ya msemo wa 'chukua chako mapema' kushika kasi hapa nchini, baadhi ya mapolisi wamegeuka nunda wala watu.Wanajihusisha na chochote cha kuwaingizia kipato. Mpaka wa Rombo na Kenya una mapolisi wamejipanga huko kusaidia wafanyabiashara kupitisha sukari kwenda nchi za jirani.Hilo usemalo la baharini silishangai sana kwa sababu ndipo mahali tulipo kwenye nchi hii. Kama una uwezo fanya magendo yoyote, mkatie polisi posho kidogo na mambo yako yatakuwa saaafi. Nenda ofisi ya ccm, omba kuwa mwanachama,utapewa kadi kwenye sherehe ambayo Nape atahudhuria na kutoa hotuba ya kusifia ccm.
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
04 DECEMBER 2012

HATARI*Wahalifu wadaiwa kupewa ulinzi Bahari ya Hindi *Polisi lawamani, hofu ya kuingizwa silaha yatanda *Wavuvi wahofia usalama wa maisha yao baharini


Na Waandishi Wetu - MAJIRA

ULIPAJI kodi si jambo la hiari bali ni lazima ili kuchochea maendeleo ya sekta mbalimbali. Taifa ambalo wananchi wake hawalipi kodi, haliwezi kupiga hatua ya maendeleo.

Mamlaka ya Mapato na Tanzania (TRA), ina wajibu mkubwa wa kuhakikisha kila mwananchi anayestahili kulipa kodi anawajibika kufanya hivyo ambapo Jeshi la Polisi, linapaswa kuzuia mianya yote ya ukwepaji kodi inayofanywa na watu wasio waadilifu.

Katika kipindi cha miezi zaidi ya sita, gazeti hili lilifanya uchunguzi wa kina usiku na mchana ili kuangalia ukubwa wa tatizo la ukwepaji kodi katika mizigo inayoingizwa jijini Dar es Salaam kwa njia za panya kupitia Bahari ya Hindi, ikitokea visiwani Zanzibar.

Mizigo hiyo hushushwa katika maeneo ya Msasani na Kawe ambapo kazi ya ushushaji shehena ya mizigo katika bodi iznazomilikiwa na watu binafsi hutumia muda usiozidi dakika saba hadi 10.

IMG_2857.jpgUchunguzi wa gazeti
Uchunguzi uliofanywa na Majira, umebaini wapo baadhi ya askari polisi wasio waadilifu ambao hupokea rushwa kutoka kwa matajiri wa mizigo hiyo ili kuwapa ulinzi.

Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Jeshi la Polisi unapaswa kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini askari wanaofanya vitendo hivyo kinyume na maadili ya kazi zao na kuwachukulia hatua kwani hali hiyo inaweza kusababisha usalama wa nchi kuwa hatarini.

Uingizaji mizigo kwa njia za panya kutoka Zanzibar umekuwa ukifanyika muda mrefu. Boti hizo hupakua mizigo hiyo kuanzia saa nane usiku hadi 11 alfajiri.

Wakazi waishio jirani na maeneo hayo ambao wamezungumza na gazeti hili, walisema wasiwasi wao ni juu ya mizigo inayoingizwa wakiamini pengine baadhi ya matajiri husafirisha silaha ambazo wabebaji si rahisi kuzibaini wanapobeba mizigo hiyo kwa ujira mdogo usioendana na kazi wanayoifanya (kujitoa mhanga).


IMG_2859.jpg
Gazeti hili lilizungumza na mmoja kati ya wabebaji anayeendesha maisha yake kupitia kazi hiyo (jina linahifadhiwa), ambaye alidai uingizwaji mizigo kwa njia za panya umeanza muda mrefu.

"Ngoja niwaeleze ndugu zangu, kazi ya kubeba mizigo haramu inayotoka Zanzibar imeanza kuda mrefu, mimi binafsi naihudumia familia yangu kupitia kazi hii, wapo baadhi ya askari polisi ambao wanatoa ulinzi na kulipwa fedha na matajiri (wahusika wa mizigo).

"Awali baadhi ya boti zilikuwa zikileta mizigo na pale zilipotaka kukamatwa, zililazimika kukimbia majini, sisi tunaamini askari waliokuwa wanataka kuzikamaata walikuwa wageni tofauti na wale wazoefu ambao wamezoea kuchukua rushwa.

"Mizigo inayoletwa na boti hizi haitokei Zanzibar pekee bali hata katika nchi jirani (jina linahifadhiwa)," alidai mbebaji huyo.

Uchunguzi wa gazeti hili ulikwenda sambamba na uchukuaji picha zinazoelezea uhalisia wa biashara hiyo, zikionesha boti moja iliyokuwa na watu zaidi ya 10, ikishusha mizigo iliyofungwa katika viroba na kupakiwa katika gari aina ya Hiace (namba tunazo), ambayo ilikimbia baada ya kuwaona waandishi wetu.

Mvuvi mmoja ambaye alizungumza na gazeti hili (jina tunalo), alisema upo umuhimu mkubwa wa Serikali hasa TRA, kuchukua hatua za haraka kudhibiti hali hiyo kwani kodi inayopotea ni kubwa kulingana na shehena ya mizigo inayoingizwa kila siku.

Alisema zipo tetesi zinazodai kati ya mizigo inayoingizwa ni pamoja na silaha ambazo hutumiwa na wahalifu katika matukio mbalimbali ya uhalifu na mauaji ili kujipatia utajiri wa haraka.

Aliongeza kuwa, wapo baadhi ya wavuvi ambao hivi sasa wameacha kuvua usiku wa kuanzia saa saba wakihofia usalama wa maisha yao kutokana na taarifa walizopata kuwa kati ya mizigo inayoingizwa na boti hizo ni pamoja na silaha za moto.

"Hadi sasa hakuna mvuvi anayeweza kuhoji na kupata majibu ya mara moja juu ya ukweli wa taarifa hizi, hatujui ni aina gani mizigo inayoingizwa na matajiri kwani hata polisi ambao tunawategemea kwa kuzuia uhalifu, wanatoa ushirikiano kwa wahalifu.

"Huu ni mchezo mchafu ambao uongozi wa Jeshi la Polisi haupaswi kuuvumilia, hatujui wahusika wa silaha hizi akina nani na zinakwenda wapi.

"Hivi sasa kumekuwa na matukio ya vurugu mbalimbali nchini hasa zinazochangiwa na imani (dini), hivyo wasiwasi wetu ni kwamba, huenda silaha hizi zikatumika kuchochea mgogoro uliopo," alisema.

Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini hakuna mvuvi au mbebaji mizigo aliyeshuhudia uingizwaji silaha katika mizigo hiyo kwa wale waliohojiwa.

Polisi wazungumza
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema alidai kuwa, yeye binafsi hana taarifa kamili hivyo aliwataka waandishi wafanye mawasiliano na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.

"Taarifa hizi ndio nazisikia kwenu hivyo tutafanya jitihada za haraka kuhakikisha tunafanya uchunguzi wa kina ili wahusika wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria," alisema.

Kamanda Charles Kenyela
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, alisema ni kosa kisheria kwa askari kushiriki vitendo vya uhalifu kulingana na kazi yake.

"Siwezi kuthibitisha suala hilo kama lipo au halipo lakini tutafanya uchunguzi na polisi ambao watabainika kujihusisha na vitendo vya aina hii watachukuliwa hatua iwe mfanmo kwa wengine.

"Bahari ya Hindi inalindwa na Jeshi la Polisi Kitengo cha Majini ambao ambao ndio wanapaswa kufanya doria baharini hivyo ni vizuri nao wakapewa nafasi ya kuzungumzia suala hili," alisema.


Msemaji wa Jeshi la Polisi
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Bi. Advera Senso, alishindwa kuthibitisha madai ya askari kuwapa ulinzi wahalifu wanaokwepa kodi na kusema kuwa, upo umuhimu wa jamii kutoa taarifa za siri kwa uongozi wa jeshi hilo ili wahusika wachukuliwe hatua.

"Mimi sina taarifa na suala hilo ndio kwanza nalisikia, tunawaomba wananchi pindi wanapoona kuna tukio ambalo si zuri, watoe tarifa za siri kwa polisi ili wahusika waweze kukamatwa," alisema.

Mbunge wa Kawe
Gazeti hili pia lilimtafuta Mbunge wa Kawe, Bi. Halima Mdee, ambaye alikiri kupokea taaarifa za kuingizwa mizigo mbalimbali kutokea Zanzibar kwa njia za panya ili kukwepa kodi hasa nyakati za usiku.

Alisema baadhi ya askari wasio wadilifu wamekuwa wakilalamikiwa kwa kushindwa kufanya kazi badala yake wanashiriki kutoa ulinzi kwa matajiri wa mizigo inayoshushwa katika boti hizo.

"Malalamiko haya nimeyapata muda mrefu juu ya polisi wetu kuwapa ulinzi wahalifu wanaoingiza bidhaa mbalimbali kwa njia za panya hivyo kuikosesha Serikali mapato.

"Tatizo jingine ni baadhi ya askari kuwabambikia kesi wananchi, hii ni kero kubwa ambayo uongozi wa Jeshi la Polisi unapaswa kufanya uchunguzi wa haraka," alisema Bi. Mdee.

Hata hivyo, Bi. Mdee alikwenda mbali zaidi na kuuomba uongizi wa jeshi hilo, ufanye mapinduzi ya kuwabadilisha vituo vya kazi askari waliopangiwa kazi jimboni humo pamoja na kuunda kamati ambayo itafuatilia malalamiko ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi.

Diwani Kata ya Kawe
Majira pia lilimtafuta Diwani wa Kata ya Kawe, Bw. Athumani Chipeta, ambaye alidai taarifa za mizigo kuingizwa kwa njia za panja katika eneo la kata yake ndio kwanza anazisikia hivyo aliahidi kuzifanyia kazi kwa kuwasiliana na Mkuu wa Kituo cha Polisi Kawe ili waweze kuchukua hatua.

"Nawashukuru kwa taarifa hizi ingawa ndio kwanza nazisikia hivyo nitakwenda kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Kawe kumweleza ili uchunguzi uanze mara moja kwani wanasababisha Serikali ikose mapato, kama vitendo hivi vinafanyika katika ufukwe wa Kawe basi na ule wa Kunduchi nako si salama," alisema.

Siku mbili baada ya gazeti hili kuzungumza na Bw. Chipeta, alipiga simu katika chumba cha habari na kudai katika uchunguzi ambao ameufanya, baadhi ya polisi wa Kituo cha Kawe walikiri uwepo wa tatizo la bidhaa mbalimbali kuingizwa jijini Dar es Salaam kwa njia za panya katika ufukwe wa Kawe hivyo Serikali
kukosa mapato ambayo yangetokana na kodi.

"Kimsingi nimejaribu kufuatilia ambapo baadhi ya polisi wamekiri kuwepo kwa tatizo la uingizwaji bidhaa linalofanywa na wafanyabiashara hivyo uchunguzi zaidi unafanyika ili kuwabaini wahusika," alisema.

TRA wazungumza
Waandishi wetu walifanya jitihada za kuwasiliana na Kamishna wa Upelelezi wa Kodi, Bw. Lusekelo Mwasyeba, ambaye alisema kuwa haitakuwa jambo la busara kulizungumzia suala hilo.

"Si vizuri kuanza kutoa maelezo yanayohusiana na suala hili kwani tayari tunashirikiana na watu flani hivyo tukitoa taarifa za mambo haya tutaharibu upelelezi," alisema. 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225

Sijali ULIPAJI wa KODI kwa TRA; KINACHONITISHA ni HIZO SILAHA; Kuingia Bara inaogopesha kweli kwa sisi sababu kila MTU sasa ana SILAHA BILA LESENI...

Na Sasa HIVI TUNAVYOCHUKIANA... RAIS WETU huyu wa SASA kaonyesha MATABAKA yetu na kuyataja kiuhalali; Sasa tunajua CHUKI ZETU TUNAPELEKA wapi... ni KUFYATUANA tu KARIBU RWANDA B
 
  • Thanks
Reactions: Paw

Waambi

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
737
0
Polisi ndio wanaongoza kwa uhalifu. Matatizo yetu mengi nchini ni ya kimaadili. Hata ukiongeza mishahara kiasi gani wakorofi hawatoisha.
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
19,775
2,000
Nauliza hivi hizo picha zilizoambatanishwa kwenye habari hizi za post #6 zinaonyesha moja ya matukio ya kuingwa vitu hivyo vya hatari?

Lingine: Je picha hii haijatumika kisiasa kwa kupaka mtubwi huo rangi zinazofanana rangi zitumiwazo na vyama vya CDM na ADC ?

Kama kweli hizo picha post #6 zinahusiana na matukio hayo kwa nini tusianze kuwa chunguza hao wanoonekana kwenye picha?
 

Baba V

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
19,487
2,000
Ndo ubaya w kuwa na mkuu wa nchi anayedhani kuwa kuwa ikulu ni dili na ni sehemu ya kupgia dili
 

katalina

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
262
0
Sasa hapa unachoshangaa nini, mbona wezi wa fedha za EPA walizirudisha wao wenyewe na hakuna kilichofanyika!
 

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,221
1,225
Baada ya msemo wa 'chukua chako mapema' kushika kasi hapa nchini, baadhi ya mapolisi wamegeuka nunda wala watu.Wanajihusisha na chochote cha kuwaingizia kipato. Mpaka wa Rombo na Kenya una mapolisi wamejipanga huko kusaidia wafanyabiashara kupitisha sukari kwenda nchi za jirani.Hilo usemalo la baharini silishangai sana kwa sababu ndipo mahali tulipo kwenye nchi hii. Kama una uwezo fanya magendo yoyote, mkatie polisi posho kidogo na mambo yako yatakuwa saaafi. Nenda ofisi ya ccm, omba kuwa mwanachama,utapewa kadi kwenye sherehe ambayo Nape atahudhuria na kutoa hotuba ya kusifia ccm.
Wana JF,

Huko nyuma me nilisha wahi suggest kuwa kuwepo na Taasisi zingine zinazo anagalia hizi taasisi tulizo nazo kisheria na ziwe na nguvu za kuwachunguza na kufikishwa kwa Pilato. Usalama wa Taifa wenye ndio umeoza kabisaaaaa na hata kama wao USALAMA wana jiaminiu wako gado then wao ndio wanalinda uozo huu kwa kuwa ni kuwalinda wakubwa na wafanya biashara kwa ajili ya njaaa zao KODI zinakwepwa sana na wakubwa na wafanya biashara matokeo yake wafanyakazi wa mashirika ya UMMA na SEKTA BINAFISI na wafanyakazi wa serikali ndio tunao umia na PAYE kila mwezi twalipa kodi bila mjadala je hao wafanya biashara wakubwa inakuwaje Bandarini ndiko nako kuna uozo mtu yaaani vyanzo vyote ni kuwa na mipangilo mibovyu ya kuingiza kodi na ndio maana watu wana kwepa kodi hatuna mfumo halisi wa kukusanaya kodi ni unajengewa mazingira mambovu ili tu utoe hongo na ulipe kodi kidogo kumbe ni ilikuwa ni halali yako ulipe hiyo kodi ndogo.

Dhamana ya viongozi tulio wapa ndio watakapo tupeleka pabaya nchi ikichafuka wala sio UPINZANI ni SERIKALI iliyoko madarakani imeshindwa kabisa kuboresha misfumo yake ya kiutendaji katika kuikwamua nchi hii kutokana na umaskini, ujinga, uchumi mbovu, rushwa iliyo kithiri, mauajia ya raia kutoka kwa askari police haya yote ndio vyazo vya nchi nyingi kupotea kwa amani na haki. Kiongozi yeye aliopo juu ana preach HAKI NA AMANI ukirudi nyuma yake ndio mchafu kupita maelezo sasa hapo mtasema Watanzania ni wabaya au ni viongozi ni wana akili mgando

My Take;
Nchi hii imeshikiliwa na viongozi wasio na uzalendo kabisa na wasio itakia mema AMANI ya nchii na ndio hao hao wanajifanya wahubiri amani na ni wanafiki wakubwa na wahujumu uchumi kwa wananachi wanao waongoza

Police imekuwa ni Branch ndogo ya TRA na sio waongoza usalama au wasiamamia usalama wao ni TAX Collectors tena hawana uoga kabisa na hili liko wazi IGP, JK,PINDA,HOSEA na usalama wa Taifa na raia wote twalijua hili, Ukienda kituo cha Police utawekewa mazingira ya wewe kutoa pesa au ukikutana na askali border au Barabarani kitu cha kwanza tu utajua hawa ni Pesa tu wanataka hakuna kitu na kweli

 

cacico

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
8,364
1,250
yaani sijawahi ona rais cartoon kama huyu wetu!! ni bora kujua unatawaliwa na tom and jerry, maana wamejaa maarifa na ubunifu! kuliko hili janga tulilonalo!
 

filonos

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
647
225
Unauliza wazungu Ndanda?

weee kweli sio Mtanzania UPO INDIA UNAULIZA WAINDI MBONA WWNGI HUKU?? huku ndio kwao na hao hiyo ndio kazi yao WALIOTUMWA KUFANYA usishangae wee ukiona shika njia uende uatpigwa na kitu chenye NCHAKALI IWE TABU KWAKO hayakuhusu Mbuzi hula kwa ulefu wa Kamba yakeeeee!!!!!!!!!!!
 

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,134
2,000
Mbona bandari ya Mbweni hayo ni mambo ya kawaida na polisi wa Wazo ndio mahali pa kula
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom