HATARI: Tossi, FFU wamfuata Zitto Mererani

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Kuna habari kwamba Mkuu wa Operesheni Maalumu wa Polisi, venance Tossi na maofisa wanne waandamizi wa polisi Wako Mererani katika mkutano wa Zitto. haijafahamika hasa kwanini nguvu kubwa imepelekwa huko. Ofisa mmoja mstaafu wa polisi alisema ni lazima Zitto awe mwangalifu kwani upo uwezekano wa kuandaa ama kuchochea vurugu ili lolote liweze kutokea. Zitto hakwenda huko kuanzisha vurugu na hajawahi kufanya hivyo. Kwa mujibu wa watu walioko Arusha, mada kuu itakua, "CCM loosing touch with Wananchi. CCM from a movement to an electoral machine."
 
Haya ndiyo mambo ya kuzungumzia, hivi Zitto si kafungiwa na Bunge takatifu? Si hoja zao ni za kipuuzi na wananchi wasiziamini? Si CCM tayari wameenda kusafisha sumu ya wapinzani kwa kufafanua jinsi tulivyogawana "kasungura" ka Lowassa. Sasa kinachowatisha hasa ni nini?
 
Haya ndiyo mambo ya kuzungumzia, hivi Zitto si kafungiwa na Bunge takatifu? Si hoja zao ni za kipuuzi na wananchi wasiziamini? Si CCM tayari wameenda kusafisha sumu ya wapinzani kwa kufafanua jinsi tulivyogawana "kasungura" ka Lowassa. Sasa kinachowatisha hasa ni nini?

Mkuu MwKjj, Hapo I beg to differ, haya ndo ya kuzungumzia tu kwasababu ya Zitto. Hata topic zingine pia zina value mkuu kuzizungumzia

Nnavyofahamu mimi Tossi ni Mkuu wa operesheni maalum,sasa asiende Mererani tu kufanya kazi zake kwa schedule zake alizozipanga kwa sababu tu Zitto yuko huko?
 
Mkuu MwKjj, Hapo I beg to differ, haya ndo ya kuzungumzia tu kwasababu ya Zitto. Hata topic zingine pia zina value mkuu kuzizungumzia

Nnavyofahamu mimi Tossi ni Mkuu wa operesheni maalum,sasa asiende Mererani tu kufanya kazi zake kwa schedule zake alizozipanga kwa sababu tu Zitto yuko huko?

kulingana na post ya kwanza kwenye thread hii umeambiwa kuwa Tossi ameenda kwa ajili ya mkutano wa zitto! nadhani swali lako limejibiwa unless kama una taarifa kuwa Tossi alikuwa na ziara ya mererani ya muda mrefu ila "coincidentally" imegongana na ziara ya Zitto!
 
Kwanza hii habari imethibitishwa? Tungepata chanzo chake ingekuwa vema. Tusianze kiushabiki, Mzee Mwanakijiji vipi tena umesahau "hoja hujibiwa kwa hoja?"

Mkuu Halisi au yeyote mwenye data amwage kitu kizima hapa kichambuliwe kinagaubaga.
 
Mkuu MwKjj, Hapo I beg to differ, haya ndo ya kuzungumzia tu kwasababu ya Zitto. Hata topic zingine pia zina value mkuu kuzizungumzia

Nnavyofahamu mimi Tossi ni Mkuu wa operesheni maalum,sasa asiende Mererani tu kufanya kazi zake kwa schedule zake alizozipanga kwa sababu tu Zitto yuko huko?


You can differ all you want.. kuna mambo ya "kuzungumzia" na yapo ya "kuzungumzwa" mimi nimeona haya ndiyo ya kuzungumzia kwa sababu kwanini vyombo vya dola vinamtendea hivi mwananchi? Hivi kuwa mpinzani ni jambo la hatari sana? Je wanataka kutuma ujumbe kwa wabunge wengine kuwa wasishupalie mambo Bungeni maana wakifanya hivyo siyo tu watafungiwa bali pia watajikuta wanawekwa mahali pabaya pa kufuatiliwa na vyombo vya dola?

Tossi ndiyo tunamfahamu na miye ninamfahamu vizuri sana... haendi kule kwa bahati mbaya!! Ila hizi operesheni zinazogongana na Zitto anakokwenda ni operesheni gani hizi?
 
kama hiyo habari ni ya kweli kwa asilimia zote, basi ni hatari kubwa, kwa vile ccm na serikali yake tayari imeshakosa muelekeo, na inaweza kuleta athari kubwa zaidi ya hii kwa wananchi
 
Kwanza hii habari imethibitishwa? Tungepata chanzo chake ingekuwa vema. Tusianze kiushabiki, Mzee Mwanakijiji vipi tena umesahau "hoja hujibiwa kwa hoja?"

Mkuu Halisi au yeyote mwenye data amwage kitu kizima hapa kichambuliwe kinagaubaga.

Mwakilishi, subiri hadi magazeti yaandike kesho! kuna vyanzo lazima vilindwe. Jana nilipowaambia kuwa "Zitto kazuiwa Moshi".. hakuna chombo kingine cha habari, I was the source here.. you can quote me. Vyombo vyetu vya habari vikubwa viko slow kufuatilia habari... ndiyo maana JF is on the cutting edge of breaking news.. and exclusive news..
 
Mwakilishi, subiri hadi magazeti yaandike kesho! kuna vyanzo lazima vilindwe. Jana nilipowaambia kuwa "Zitto kazuiwa Moshi".. hakuna chombo kingine cha habari, I was the source here.. you can quote me. Vyombo vyetu vya habari vikubwa viko slow kufuatilia habari... ndiyo maana JF is on the cutting edge of breaking news.. and exclusive news..

Thats what I am talking about!

JF right now ni kama AP (Associated Press) vile!

Kill me or call me crazy but this is true!
 
Polisi wamzuia Zitto kuhutubia TPC Moshi
* Wasema angefanya mkutano kungetokea fujo
* TPC washangaa mbona hawajazungumza na polisi

* Chadema wadai kuna mkono wa serikali


Na Daniel Mjema, Moshi


JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro jana lilizuia kufanyika kwa mkutano wa hadhara ambao ungehutubiwa na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Zitto Kabwe, katika uwanja wa Limpopo ulioko ndani ya eneo la Kiwanda cha Sukari cha TPC, kwa madai ya kuepusha vurugu ambazo zingetokea kwenye mkutano huo.


Kwa mujibu wa barua ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Moshi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi(SSP), Kibwana Majid, endapo mkutano huo ungefanyika kungeweza kutokea vurugu kati ya menejimenti ya TPC na Chadema.


SSP Majid alisema katika barua hiyo ya jana, Jeshi la Polisi limepata taarifa ya kuwepo kwa matangazo kwa kutumia vipaza sauti juu ya kuwepo kwa mkutano huo ambao ungehutubiwa na Kabwe.


"Baada ya kufuatilia taarifa hizo viongozi wa TPC walinijulisha kwamba uwanja huo uko ndani ya utawala wa TPC na kwamba haukuwa na taarifa ya kufanyika kwa mkutano huo," ilisema barua hiyo.


"Kutokana na sababu hizo na nyinginezo za kiusalama, kwamba kunaweza kutokea vurugu kwa kutoelewana kati ya TPC na Chadema, hivyo ofisi hii inapendekeza kusitishwa kwa mkutano huo katika eneo hilo," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.


Hata hivyo, Afisa Mtendaji wa TPC anayeshughulikia Utawala, Jaffar Ally alipohojiwa na mwandishi wa Mwananchi kwa simu jana, alishangazwa na kauli hiyo ya polisi na kusema TPC hawana mamlaka ya kuzuia mkutano wowote.


"Hapa mbele yangu nina barua ya Chadema ya mkutano ambayo imeandikwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi na sisi tumepewa nakala tu na hatukuwajibu kwa sababu tulijua kibali cha mkutano kinatolewa na Polisi," alisema.


Ally alisema hata Askofu Zakaria Kakobe na viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Mashambani (TPAWU), waliutumia uwanja huo kufanya mikutano akashangaa TPC kuwekewa maneno kuwa wamewakatalia Chadema


"Hebu nipe namba ya hao watu wa Chadema niwasiliane nao ili nijue nini kilitokea kwa sababu hatujafanya kikao chochote na polisi wala Chadema, sasa tungesemaje kutatokea vurugu?" alihoji Afisa huyo.


Kabwe aliliambia Mwananchi kuwa yeye ni mgeni wa Chadema mkoa Kilimanjaro na mkutano huo ulikuwa ni wa kukiimarisha chama na angetumia mkutano huo kuzungumzia mambo muhimu ya maslahi ya nchi.


"Barua hii ya polisi bado hainiingii akilini kwamba Chadema tungegombana na TPC, sisi tunashangaa, kwani TPC ni chama cha siasa? Hapa naona kuna jambo," alisema.


Kwa upande wake, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Akwiline Chuwa alisema sababu zilizotolewa na polisi ni za kisiasa zaidi na kuna kila sababu ya wao kuamini kuwa ni agizo la Serikali.


"Sisi hatujawahi kuwa na ugomvi na TPC na kimsingi walipokuwa na mgogoro na wafanyakazi tulikuwa tunaomba umalizike maana kuna wanachama wetu hapo, sasa leo tunashangaa tunapoambiwa tutapigana na TPC," alisema Chuwa.


Katibu huyo alisema tangu kuwapo kwa kampeni za kujaza nafasi za viti vya udiwani, serikali imekuwa ikitumia nguvu ya ziada kukabiliana na wapinzani, ikiwamo kuitumia vibaya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Moshi.

Hii ya Zitto kuzuiwa kuhutubia Mererani sijaipata, ila hio hapo juu ndio imetangazwa jana.
Labda tujiulize, kwa nini sirikali inakuwa na kiwewe mara isikiapo Zitto atakuwa mahali fulani, hata kama si kwa kazi za kisiasa?
 
Mererani si mbali sana na simu zipo,,, wengi wanaobisha hapa, hawashindwi kupiga simu kwa RPC Manyara, ama hawawezi kukosa mtu wanayemfahamu Mererani ama Arusha.. Hizo tumewapa ni taarifa za awali zaidi baadaye..
 
Wanachofanya ni kuahirisha matatizo. Ni sawa na mgonjwa mwenye majipu, anayaona, lakini anasema "oh, hili si jipu...", linatoka lingine, anasema "hili nalo si jipu..." basi mwili mzima unajaa majipu.

Siku yakija kuiva na kulipuka yenyewe, sijui mgonjwa huyo atakimbilia wapi? Atakuwa na usaha mwili mzima!

Watanzania wameonesha dalili zote za kuchoka, na haya ndiyo majipu yenyewe. Akina Zitto wanapofukuzwa bungeni na kuzuiwa (lakini Sitta alisema anaruhusiwa kufanya kazi zake za kibunge...) kuzungumza hadharani, kwa kisingizio kwamba kwa kufanya hivyo kutatokea vurugu (yale yale ya 1995...), basi, wajue kwamba ndio wanazidi kuwapandisha mori wananchi.

Dawa ni kuwaacha wanaolalamika walalamike, kisha matatizo yao yashughulikiwe. Mkiwakandamiza wananchi kwa muda mrefu sana, yatakuja kutokea yaliyotokea kule Burma... sorry, Myanmar... watu wamesema hata wakiuwawa, hawatoki barabarani... jamani, tusiombe haya yafike huku kwetu!

Wenye kusikia na wasikie.
 
Kweli huko ni sawa na kupaka maji ya kunde katika jipu ili lihame sehemu unayoona ni nyeti kwa jipu kupasukia lakini iwe isiwe jipu kutoka kwake ni kupasuka tu hakuna njia nyingine. Hisia za wananchi zipo pale pale hata kama Zitto atashindwa kuhutubia wananchi, jamani mbona hata sisi mabubu tunazungumza siku hizi.
 
Nakusikia Mkuu Mzee Mwanakijiji,

Ila akina sie wengine tunapenda kupata habari pamoja na vyanzo vyake ili kuweza kufanya analysis bila ya kulalia upande mmoja knowingly, ni hilo tu.

Hiyo strategy ya kutumia vyombo vya dola kumnyamazisha Zitto ita-backfire vibaya sana, kwa kufanya hivyo serikali inawaambia wananchi kuwa huyu bwana anatukosesha usingizi kila ahutubiapo, yaani kwa kifupi wanampigia kampeni bila kujua.
 
Haya ndiyo mambo ya kuzungumzia, hivi Zitto si kafungiwa na Bunge takatifu? Si hoja zao ni za kipuuzi na wananchi wasiziamini? Si CCM tayari wameenda kusafisha sumu ya wapinzani kwa kufafanua jinsi tulivyogawana "kasungura" ka Lowassa. Sasa kinachowatisha hasa ni nini?

watanzania wamekakataa kasungura,watu wamekakataa kabisa,pesa imepotea bure tu,hivi nani huwa anapanga safari za hawa viongozi?
mie nataka hata ndama tu!!
 
Kamanda Tossi, anasema kwamba yuko mkoani Manyara katika operesheni kupambana na MAJAMBAZI katika mikoa ya Manyara na Singida, na kwamba muda huu yuko mpakani mwa Singida na Manyara, wala hana habari na mambo ya siasa. Lakini aliyeko katika eneo la tukio anasema, "Si kweli wapo hapa na ndio kwanza mkutano unamalizika kwa amani, sijui kitakachoendelea baada ya hapa."

Mererani iko mkoa wa Manyara.
 
Thanks Halisi
Napenda kumweleza Mbangaizaji na Mwakilishi kwamba JF imetapakaa .Ndiyo nimeongea na mtu wa Manyara kasema Tossi yupo na alikuwepo muda wote . Tossi kaelekea huko leo akiwa na hao maofisa na kila mmoja amemuona .Sasa anadiriki hata kudanganya mambo yenyewe simu za mkononi ? Mbona wasimtaje Manumba na maofisa wengine toka nje ya Manyara ?
 
Watu wanaogopa hata vivuli vyao. Kama huyo polisi ameenda huko, si aende tu na Zitto aendelee na kazi zake?

Kama huna cha kuficha au kuogopa kwanini iwe jambo polisi kuwepo kwenye mkutano?
 
Mtanzania, kama wapinzani wamejifunza vizuri ni kuwa polisi hawachelewi kutaka "wamalize mkutano" au kuzima mkutano wakiona wao inafaa.. sasa kumpeleka kamanda mzima kama tossi wakati wapo polisi na ma ocd kule ya nini kama siyo lengo kutishia wazungumzaji. Kwenye hili polisi wetu hawana rekodi nzuri..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom