HATARI: Tossi, FFU wamfuata Zitto Mererani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HATARI: Tossi, FFU wamfuata Zitto Mererani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Oct 30, 2007.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna habari kwamba Mkuu wa Operesheni Maalumu wa Polisi, venance Tossi na maofisa wanne waandamizi wa polisi Wako Mererani katika mkutano wa Zitto. haijafahamika hasa kwanini nguvu kubwa imepelekwa huko. Ofisa mmoja mstaafu wa polisi alisema ni lazima Zitto awe mwangalifu kwani upo uwezekano wa kuandaa ama kuchochea vurugu ili lolote liweze kutokea. Zitto hakwenda huko kuanzisha vurugu na hajawahi kufanya hivyo. Kwa mujibu wa watu walioko Arusha, mada kuu itakua, "CCM loosing touch with Wananchi. CCM from a movement to an electoral machine."
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Oct 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Haya ndiyo mambo ya kuzungumzia, hivi Zitto si kafungiwa na Bunge takatifu? Si hoja zao ni za kipuuzi na wananchi wasiziamini? Si CCM tayari wameenda kusafisha sumu ya wapinzani kwa kufafanua jinsi tulivyogawana "kasungura" ka Lowassa. Sasa kinachowatisha hasa ni nini?
   
 3. M

  Mbangaizaji Senior Member

  #3
  Oct 30, 2007
  Joined: Jul 23, 2007
  Messages: 121
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mkuu MwKjj, Hapo I beg to differ, haya ndo ya kuzungumzia tu kwasababu ya Zitto. Hata topic zingine pia zina value mkuu kuzizungumzia

  Nnavyofahamu mimi Tossi ni Mkuu wa operesheni maalum,sasa asiende Mererani tu kufanya kazi zake kwa schedule zake alizozipanga kwa sababu tu Zitto yuko huko?
   
 4. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kulingana na post ya kwanza kwenye thread hii umeambiwa kuwa Tossi ameenda kwa ajili ya mkutano wa zitto! nadhani swali lako limejibiwa unless kama una taarifa kuwa Tossi alikuwa na ziara ya mererani ya muda mrefu ila "coincidentally" imegongana na ziara ya Zitto!
   
 5. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwanza hii habari imethibitishwa? Tungepata chanzo chake ingekuwa vema. Tusianze kiushabiki, Mzee Mwanakijiji vipi tena umesahau "hoja hujibiwa kwa hoja?"

  Mkuu Halisi au yeyote mwenye data amwage kitu kizima hapa kichambuliwe kinagaubaga.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Oct 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  You can differ all you want.. kuna mambo ya "kuzungumzia" na yapo ya "kuzungumzwa" mimi nimeona haya ndiyo ya kuzungumzia kwa sababu kwanini vyombo vya dola vinamtendea hivi mwananchi? Hivi kuwa mpinzani ni jambo la hatari sana? Je wanataka kutuma ujumbe kwa wabunge wengine kuwa wasishupalie mambo Bungeni maana wakifanya hivyo siyo tu watafungiwa bali pia watajikuta wanawekwa mahali pabaya pa kufuatiliwa na vyombo vya dola?

  Tossi ndiyo tunamfahamu na miye ninamfahamu vizuri sana... haendi kule kwa bahati mbaya!! Ila hizi operesheni zinazogongana na Zitto anakokwenda ni operesheni gani hizi?
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2007
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kama hiyo habari ni ya kweli kwa asilimia zote, basi ni hatari kubwa, kwa vile ccm na serikali yake tayari imeshakosa muelekeo, na inaweza kuleta athari kubwa zaidi ya hii kwa wananchi
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mwakilishi, subiri hadi magazeti yaandike kesho! kuna vyanzo lazima vilindwe. Jana nilipowaambia kuwa "Zitto kazuiwa Moshi".. hakuna chombo kingine cha habari, I was the source here.. you can quote me. Vyombo vyetu vya habari vikubwa viko slow kufuatilia habari... ndiyo maana JF is on the cutting edge of breaking news.. and exclusive news..
   
 9. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Thats what I am talking about!

  JF right now ni kama AP (Associated Press) vile!

  Kill me or call me crazy but this is true!
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Hii ya Zitto kuzuiwa kuhutubia Mererani sijaipata, ila hio hapo juu ndio imetangazwa jana.
  Labda tujiulize, kwa nini sirikali inakuwa na kiwewe mara isikiapo Zitto atakuwa mahali fulani, hata kama si kwa kazi za kisiasa?
   
 11. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mererani si mbali sana na simu zipo,,, wengi wanaobisha hapa, hawashindwi kupiga simu kwa RPC Manyara, ama hawawezi kukosa mtu wanayemfahamu Mererani ama Arusha.. Hizo tumewapa ni taarifa za awali zaidi baadaye..
   
 12. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #12
  Oct 30, 2007
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Wanachofanya ni kuahirisha matatizo. Ni sawa na mgonjwa mwenye majipu, anayaona, lakini anasema "oh, hili si jipu...", linatoka lingine, anasema "hili nalo si jipu..." basi mwili mzima unajaa majipu.

  Siku yakija kuiva na kulipuka yenyewe, sijui mgonjwa huyo atakimbilia wapi? Atakuwa na usaha mwili mzima!

  Watanzania wameonesha dalili zote za kuchoka, na haya ndiyo majipu yenyewe. Akina Zitto wanapofukuzwa bungeni na kuzuiwa (lakini Sitta alisema anaruhusiwa kufanya kazi zake za kibunge...) kuzungumza hadharani, kwa kisingizio kwamba kwa kufanya hivyo kutatokea vurugu (yale yale ya 1995...), basi, wajue kwamba ndio wanazidi kuwapandisha mori wananchi.

  Dawa ni kuwaacha wanaolalamika walalamike, kisha matatizo yao yashughulikiwe. Mkiwakandamiza wananchi kwa muda mrefu sana, yatakuja kutokea yaliyotokea kule Burma... sorry, Myanmar... watu wamesema hata wakiuwawa, hawatoki barabarani... jamani, tusiombe haya yafike huku kwetu!

  Wenye kusikia na wasikie.
   
 13. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2007
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kweli huko ni sawa na kupaka maji ya kunde katika jipu ili lihame sehemu unayoona ni nyeti kwa jipu kupasukia lakini iwe isiwe jipu kutoka kwake ni kupasuka tu hakuna njia nyingine. Hisia za wananchi zipo pale pale hata kama Zitto atashindwa kuhutubia wananchi, jamani mbona hata sisi mabubu tunazungumza siku hizi.
   
 14. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nakusikia Mkuu Mzee Mwanakijiji,

  Ila akina sie wengine tunapenda kupata habari pamoja na vyanzo vyake ili kuweza kufanya analysis bila ya kulalia upande mmoja knowingly, ni hilo tu.

  Hiyo strategy ya kutumia vyombo vya dola kumnyamazisha Zitto ita-backfire vibaya sana, kwa kufanya hivyo serikali inawaambia wananchi kuwa huyu bwana anatukosesha usingizi kila ahutubiapo, yaani kwa kifupi wanampigia kampeni bila kujua.
   
 15. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  watanzania wamekakataa kasungura,watu wamekakataa kabisa,pesa imepotea bure tu,hivi nani huwa anapanga safari za hawa viongozi?
  mie nataka hata ndama tu!!
   
 16. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kamanda Tossi, anasema kwamba yuko mkoani Manyara katika operesheni kupambana na MAJAMBAZI katika mikoa ya Manyara na Singida, na kwamba muda huu yuko mpakani mwa Singida na Manyara, wala hana habari na mambo ya siasa. Lakini aliyeko katika eneo la tukio anasema, "Si kweli wapo hapa na ndio kwanza mkutano unamalizika kwa amani, sijui kitakachoendelea baada ya hapa."

  Mererani iko mkoa wa Manyara.
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Thanks Halisi
  Napenda kumweleza Mbangaizaji na Mwakilishi kwamba JF imetapakaa .Ndiyo nimeongea na mtu wa Manyara kasema Tossi yupo na alikuwepo muda wote . Tossi kaelekea huko leo akiwa na hao maofisa na kila mmoja amemuona .Sasa anadiriki hata kudanganya mambo yenyewe simu za mkononi ? Mbona wasimtaje Manumba na maofisa wengine toka nje ya Manyara ?
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Oct 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hilo kweli kwani nilizungumza na Manumba Jumapili na alikuwa sehemu nyinigine kabisa...
   
 19. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Watu wanaogopa hata vivuli vyao. Kama huyo polisi ameenda huko, si aende tu na Zitto aendelee na kazi zake?

  Kama huna cha kuficha au kuogopa kwanini iwe jambo polisi kuwepo kwenye mkutano?
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Oct 30, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mtanzania, kama wapinzani wamejifunza vizuri ni kuwa polisi hawachelewi kutaka "wamalize mkutano" au kuzima mkutano wakiona wao inafaa.. sasa kumpeleka kamanda mzima kama tossi wakati wapo polisi na ma ocd kule ya nini kama siyo lengo kutishia wazungumzaji. Kwenye hili polisi wetu hawana rekodi nzuri..
   
Loading...