HATARI: Tanzania President rejects war, Joyce Banda insists whole lake belongs to Malawi

Mbona nahisi mtu kulishwa maneno. Sijaona direct quotes kuhusu "opposition parties warmongering".
1. Ndugu, JMK hajalishwa maneno. Ndio UPEO wake wa kufikiri. Inasikitisha Rais anapokosa cha kusema na anabaki KUCHEKACHEKA. Leo Lowasa na Membe (ambaye alikuwa naye palepale) anasema ni Wapinzani HAIINGII AKILINI. Labda hapa waandishi wa Malawi hawakumwelewa!
2. Katika UJUMBE wa Lowassa na Membe sikuona mahali popote walipoTANGAZA vita! Hata hivyo, Rais Kikwete angetoa TAMKO kukanusha ama kuwakaripia na kama alihisi kuna upotoshwaji, siyo kusemasema ovyo kama mtu asiyejua kinachoendelea!
3. Kwa ufupi NIMESIKITISHWA na uwezo wa Rais katika nyanja hizi! Inabidi waandishi wa habari wa Tanzania wamwulize kuhusu alichosema Maputo! Sionagi UWEZO wake wa kujenga hoja kutumia data ama habari zililizopo!
4. Asaidiwe!
 
BANDA AMESEMA ZIWA NYASA NI LAO 100% KIKWETE AMESEMA NI LETU KIaSI GANI?
 
kumbe lowassa,membe na sitta ni opposition?sina uhakika kama mkulu alikusudia kulisema hili au lilimtoka bahati mbaya.

Mkuu I wonder, because the ones who gave official strong statements were CCM leaders. Ok letz wait and see.
 
Rais G. Bush na B. Clinton walikua wanaficha udhaifu na skendo zao kwa kuwatwanga Waarabu.

Jamaa aige hii style tuwachape hawa viherehere. Hawawezi kutudharau kiasi hiki.Kwamba ukiwa Liuli au Mbambabay basi kunawa uso tu ziwani mpaka kwa Viza.
 
CHADEMA ni mnyonge wa kila kitu, Madakitari waligoma CCM wakasema ni CDM, kauli za vita zimetolewa na wanamagamba lakini JAKAYA kasema ni CHADEMA. but the reality will stand clear

Ukweli ulio wazi ni kwamba nchi inaongozwa na Chadema. Wapinzani wa CDM ni ccm (Membe, Lowasa nk).

Serikali kivuli iliyoko sasa ni Dhaifu sana.
 
Worry not my fellow Tanzanians....MSIMAMO wa Tanzania UNAJULIKANA..............kama Magamba watatu-let down kwenye mazungumzo.....hiyo itakuwa ni tiketi yao ya kwa heri 2015........Watanzania tutachagua watu walio serious kulinda mipaka yetu halali......na wala sio mipaka ya NDOTO za "Go to hell Land"
 
Commander in Chief DHAIFU..eti mimi kama Jemadari mkuu sijatoa amri kwa majeshi yangu kujiandaa na vita!!!....Sehemu ya nchi yako ambayo inadhaniwa ina utajiri mkubwa inataka kuibwa mchana kweupeeee we unakenuakenua tu na kutoa kauli fyongo zinazowaacha midomo wazi wengi wa Wananchi wako. Ni hatari sana kwa nchi kuwa na kiongozi kama huyu si ajabu yule JB kapata kibri cha hali ya juu na hivyo kutamka kwamba Lake nyasa lote ni la Malawi.

Ukweli ulio wazi ni kwamba nchi inaongozwa na Chadema. Wapinzani wa CDM ni ccm (Membe, Lowasa nk).

Serikali kivuli iliyoko sasa ni Dhaifu sana.
 
Rais wa Malawi anachokifanya ni kununua waandishi wa habari kwa propaganda zake. Kawatoa waanindishi waliokuwa wanamcritise na kuwapa kazi ikulu. Brian Banda sasa hivi ni press secretary wake na amekiacha kipindi chake cha straight talk.
Huyu mama kawatia hasara kubwa sana wawekezaji wa Malawi kwa kuhairisha African Union summit ambayo wawekezaji walijiandaa nayo kwa pesa nyingi. Rais Bingu alijenga Bingu International Conference Center kwa kupokea wageni. Center hiyo mpaka sasa haijafunguliwa kwa sababu wanazi wanataka ibadilishwe kwanza jina la Rais huyo aliyefariki! Next year Malawi watahost SADC summit na hapo ndipo watakapoona kuwa Bingu alifanya jambo la msingi kujenga ile center. Ofcourse wataifungua though haijulikani kama wataibadilisha jina.
Kiujumla, mambo yanayoandikwa kwenye Nyasatimes hayaheshimu professionalism katika uandishi, ni propaganda zaidi in favour of Joyce.
 
Magazeti yetu ya Daily News na Habari leo yako kimya, inabidi tuende kusoma times ya malawi kuelewa kilichojilia.

Magazeti gani yaliyokuwa kimya???
ziwa letu.JPG
agreement1.JPG
agreement.JPG
 
Hivi ni sahihi rais kuongelea mambo ya upinzani hata akiwa nje ya nchi!!!!! Nchi hii bado tuna safari ndefu.
 
Hivi kama Malawi wanaamini wanaimili hilo ziwa kwa 100%...wanatafuta muafaka wa kidiplomasia kwa ajili ya nini??

Sina hakika kama wataridhika na uamuzi ambao utawapa less than 100% ya Ziwa nyasa!!
 
Kati ya magazeti uliyoweka hakuna hata moja linaloeleza kwamba Kikwete ameridhia ziwa nyasa ni mali ya malawi wakati malawi vyombo vya habari vinasema kikwete karidhia.

Kama kikwete hakuridhia kwa nini serikali haikanushi habari hizo za Malawi?

Nipe chombo cha Malawi kilichosema Kikwete karidhia.
 
JK hatakiwi kutoa malalmiko ya wananchi wake kwa huyu Mama kwa kumwambia nani kasema nini? Yeye amwambia hatutaki vita kwani hili swala liko ndani ya uwezo wetu. Tulijadili ili liishe kidiplomasi na yeye yupo tayari kwa hilo. Kisha amwange ushaidi wake wa mipaka. Lakini siyo kulaumu wananchi wake. Tulishasema katika mipaka ya nchi, hakuna CCM wala CDM, ni Tanzania. Kwa maana nyingine CCM na CDM utavipata ndani Tanzania, ukiwa nje, ni Tanzania tu.

Uko sawa Mkuu,
Viongozi wetu badala ya kutenda wamegeuka walalamikaji kama sisi wananchi tusio viongozi.Ndio maana Nape alikuwa analalamika juzi juu ya fedha haramu wakati chama chake ndicho kinachoongoza Nchi.
 
Back
Top Bottom