HATARI: Tanzania President rejects war, Joyce Banda insists whole lake belongs to Malawi

Usiwe na shaka na uwezo wa mhe Membe.
Nina amini mazungumzo ya ile kamati iliyoundwa kushughulikia mgogoro huu italeta ufumbuzi sahihi.
Nyota ya TZ kwenye anga za kimataifa itazidi kung'ara
Nasubiri mohamed ali wa monduli aseme jeshi la TZ nalo litaunda kikosi maalum(shame on him).
 
Hii habari mbona imekaa kisanii.Sio kila mlionalo kwenye vigazeti vyao uchwara mtatuletea hapa,mengine yanaandikwa kwa ajili ya kuuza Gazeti,eti kikosi cha kulinda mipaka,upuuzi mtupu,hawana jeshi?
 
Naona hayo mazungumzo kama ni kupoteza muda kama Rais wa Malawi amesema hilo ni ziwa lao 100% ni heri tuvuke hatua nyingine kama kwenda mahakama ya kimataifa au na sisi tutangaze mpaka wetu ni katikati na atakayevuka tutamshugulikia.Ile kamati kwa upande wa Malawi haiwezi kwenda kinyume na matamshi ya Rais wetu na bahati nzuri amezungumza lakini huku kwetu tumesikia tamko la mawaziri na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na mambo ya nje ya bunge hatujasikia kauli rasmi ya Rais kama tuna haki ya ziwa au la zaidi ya kusema tutafanya mazungumzo.Alipokutana naye alitakiwa kumwambia waziwazi afute kauli zake au asiendelee kuliongelea hilo swala hadi kamati zilizoundwa zitoe maamuzi
 
Nimeisoma habari. Wala hicho kikosi hakiundwi na serikali ya Malawi. Ni mpuuzi mmoja wa Kimalawi anaishi Amerika anajitafutia umaarufu. Soma maoni ya Wamalawi wenyewe hawamwungi mkono
 
Jamaa alipokutana na hasimu wake akaishia kutabasamu bila kuchukua hatua, unategemea kitakachoendelea ni nini? tushaibiwa tayari!
 
Kama jk alisema kuwa wanaotaka vita ni wapinzani... Kama alisema kweli basi jk ni mwendawazimu!
 
Ingekuwa uswahilini ningesema ndiyo mkome. Nimeandika post zaidi ya 30 na sijabadili msimamo hata dakika moja kwamba Tanzania hatuna hata tone moja la maji ya Ziwa Malawi.

Wapuuzi humu badala ya kufikiri wa kutumia vichwa ikawa kama vichwa tunatumia kwa kufuga nywela kama alivyosema Justice Werema.

Kila aliyetoa ukweli kuhusu hili mkamseama ni mmalawi nikiwemo mimi. Sasa mnaona mnaelekea kushindwa porojo zenu mnaanza kumlalamikia Kikwete.

Narudia, muwe na adabu kwa mambo ambayo ni proffessional. Kwa sababu proffessionaly Tanzania hatuna hata tone moja la Ziwa Malawi na sasa kwa kujiamini nimeshaanza kuongeza kwamba hatupati tone hata moja la Ziwa hilo labda waturuhusu tu kufanya shughuli zetu bila kudai kwamba ni letu.

Sasa nisikie kama mtamuita JK naye ni mmalawi. Hakuna aliye mmalawi hapa baali kuna watu waliokataa kutumuia ubongo wao kujua kwamba Heligoland Treaty haiwezi kuwa revoked na 1982 Sea Convention na hivyo hatuna hata tone moja la ziwa Malawi.

Narudia tena, hili ni fundisho kwamba muwe na adabu proffesionals wanapoongea.

Ziwa Malawi ni la Malawi by 100% na Kikwete asingeweza kuzuia hili. Achilia mbali wapiga porojo na wakurupukaji wa JF.

Ukitaka pitia thread zangu kwa kubonyeza hapa.

Dada unaongea kwa confidence sana, kana kwamba ziwa nyasa ni la wamalawi, kwa nadharia hapo mwanzo malawi ikijulikana "nyasaland" na ziwa lile likiitwa "lake nyasa" walipobadili jina kuwa "malawi" wakalibadili na jina la ziwa kuwa "lake malawi" ujue hizo zote mbinu za kuyumbisha wajuzi wa ukweli. (Hatujawahi fikiria kubadilisha jina la ziwa tanganyika japo jina la nchi yetu tushalibadili [kumbuka jina la ziwa liliwiana na jina la nchi hivyo tungetakiwa "kwa akili za kinyasa" kuendelea kuwianisha hayo majina] tunasisitiza HATUDANGANYIKI)

kama unafanya reference kwenye heligoland treaty, nakukumbusha hiyo treaty iliwahusu wakoloni, Nyasaland na Tanganyika!!

kwa sasa hivyo vitu vitatu havipo kabisa
1) Wakoloni
2) Nyasaland
3) Tanganyika

hiyo treaty imekufa automatically!!!! kwa kukosa pa kusimamia. Kwa maana hiyo basi sheria za kimataifa kuhusu nchi mbili zikikutanishwa na ziwa, mpaka shuruti uwe katikati ya ziwa husika, unajadiliana hili na mtu asiyejua kusoma TU!

Kinyume chake mnapaswa kujiuliza huwa mnatenga fedha nyiiiiingi kwa masula ya kijeshi ili iweje, tena mmejiwekea na kanuni "marufuku kujadili matumizi ya kijeshi"
29deb737-9309-21c4.jpg
 
Haya tumeyapata kwasababu ni mgogoro mkubwa na waandishi wa Malawi wanafuatilia.Ni mangapi atakuwa ameyasema huko Europe na USA ambayo Ikulu hawakuandika.
Kuanzia sasa sitashangaa kusikia alipokuwa Europe alisema, CCM hatupingi "Ucameron" ila wapinzani ndio wamekuwa kikwazo.
 
Unachikisema kinaniingia akilini upande mwingine serikali inakuwa kama inafanya maigizo pengine usikute danganya toto kwa sababu kuuu moja ili waharibu mchakato mzima wa katiba inayoandikwa kwa sasa, Mbili kama mkikumbuka LICHIMOND Ilizuka bungeni kikaanzishwa kikombe Arusha Roliondo Richmond ikazimwa, Tatu pengi inataka kuanzishwa vita kwa masilahi ya walio madalakani kwa mfano Rais akitangaza vita mwaka 2014 mtafanya uchaguzi au???? Naomba jibu wadau nahisi kuna mchezo unataka kufanya ili CCM Ikae madarakani kwa kisingizio cha vita haya ni mawazo yangu binafisi wala cjacopy na kupest I wish good IDD,
 
true brother. You start war you make white man rich as you buy weapons. Lets not be stupid. Malawians and tanzanians in the boarder area are related and speak same languages
Things to remember among us as African countries we are the smooth market of weapon from abroad, so before war we have to think twice the necessity.
 
Ndio hatari ya kuropoka wanafunzi wanapata mimba kutokana na kiherehere chao leo amesahau kama wote waliokuwa wanazungumza na kutoa matamko ya vita ni watu wa chama chake
huyo mama kama ana uhakika ziwa lote ni la Malawi anataka mazungumzo ya nini kwa namna nyingine yeye ndio anachochea vita na hali ya wasiwasi kwa wananchi wanaoishi kando kando ya ziwa na asijifanye anajua historia kwamba Mw.Nyerere alikubali juu ya hiyo mipaka ashukuru swala hili limeibuka wakati ameshafariki kwani angechambuliwa na kimbelembele chake cha kujipendekeza kwa wazungu
nawenyewe atasema ni kiherehere chao kuongelea mambo ya siyowahusu
 
Tusipokuwa makini Pwani yooote itakuwa Zanzibar (Miliki ya sultani), kaskazini yote itakuwa kenya, Kigoma itakuwa sehemu ya burundi, Kagera ni sehemu ya Uganda, Rukwa itakuwa ya wazambia, Mbeya itakuwa ni malawi, Mtwara sehemu ya msumbiji. Wamalawi wamelianzisha hili through Banda, after Banda kwa kuhisi tu dhaifu, tukiuthibitisha udhaifu wetu tutaruhusu kugeuzwa taifa lililojaa waoga a.k.a jinsia ile nyingine. If the one who we expect to stand for the rights of our country is weak, I think its time to opt for negative option.
 
nchi yangu Tanganyika nakuona ukimegwa kidogokidogo, leo wanajimegea wamalawi kesho wakenya na mlima keshekutwa uganda na kagera,wakati huo kwa mbali burundi wanapasha bila kusahau zambia na tunduma. Kali zaidi ni wanauamusho kudai klm 10 kuanzia dar, tanga, pwani na mtwara. Wakati huo tayari waarabu wananchi yao ndani ya Tanganyika.! Baba wa taifa langu mzalendo wa kweli tena mwenye heri nitakulilia daima Mwl.Nyerere.!!! Maana uliitetea Tanganyika kwaa ajili ya vizazi vijavyo bahati mbaya kizazi cha sasa ni kama kimelaaniwa. Mh!! Inatia uchungu.!
 
JK bwana...yaani kunapokua na migogoro ukamuambia atoe kauli kama kiongozi wa nchi LAZIMA AHARIBU tuu
 
huyu JK naye kilaza! Chama gani cha upinzani kimehamasisha vita? Upuuzi huu na inabidi aombe radhi

Mkuu hujui kuwa CCM ndo chama pinzani? Huoni kinavopinga maendeleo na haki za wananchi wake?

KIKWETE IS RIGHT, CCM IS AN OPPOSITION PARTY TO MOST OF TANZANIANS AND RULLING PARTY TO NEC, TISS, POLICE AND OTHER FORCES.
 
Msimamo wa serikali ya malawi kuwa ziwa lote ni la malawi upi msimamo wa serikali ya kikwete?
 
true brother. You start war you make white man rich as you buy weapons. Lets not be stupid. Malawians and tanzanians in the boarder area are related and speak same languages

ni kweli vita ni jambo baya je kwa jina la amani tuwakubalie madai yao wamalawi kuwa ziwa nyasa ni la malawi 100%?
 
Yani bora umegundua mapema sasa Kama mama ajasema 100% ni lake alafu mbayuwayu anaomba huruma ya maongezi tena kwa kutukandia kuwa waliosema wako tayari kwa vita ni wapinzani wakati ni ccm wenyewe huoni alikuwa anaomba kuhurumiwa? Naamini ziwa limetutoka kifuatacho ni kilimanjaro, serengeti na bukoba.... Kweli Hata bibilia iliandikwa dawa au fimbo ya kidume ni kijike tuu. Kawa mpole eti anamuita joice my (sister) (if I make billion dollars a month I will make Tanzanian to be heaven) (mkigoma tuu mmepoteza ajara) (mkiandamana tuu mtagawana majengo ya serikali moi na segerea) (Mimi sio mungu kuwa ntafanya mvua inyeshe) (Hata Mimi sielewi kwanini watanzania ni masikini) (wanafunzi wanapewa mimba kwa ajili ya kiherehere chao) sasa kiongozi mwenye kauli Kama hizi unategemea niñi hapo? Wana ccm walipotangaza vita na Malawi mbona haja kanusha in public hapa tz anakwenda kujitetea kwenye nchi ya adui Kama sio trator huyu? Huyu jamaa hakustahili kuwa Hata balozi wa nyumba kumi ndio maana Nyerere alimkataa akamfariji kwa kumwambia umri wako bado...hivi kwanini Siku moja tusiseme basi Kama Libya na kwingineko? Kuvumilia mpaka tuchakachuliwe tena 2015 alafu tuvumilie tena mpaka 2025 jamani bora nihamie Somalia ambapo kila mtu ni kiongozi wa maisha yake no govt no shit

Hizi quotes za JK zimenivunja mbavu, ahadi nyingi hazitekelezeki, mwenye nchi unasema hujui kwanini wananchi wako ni maskini!
 
Back
Top Bottom