Hatari Tandahimba, Polisi wateketeza soko na maduka, Mwema na Makamu wa Raisi Watua

mwanzoni nliwasifia sana hawa jamaa lakini walipoanza kushambulia wafanyakazi wa ngazi za chini kabisa kama walimu nikoana kua hawa watuhawafai kabisa. Inabidi waelimishwe wajue kua adui yao ni yupi kabla hawajaanza kuponda watu.

ni kweli maneno yako ila maandamano ya wakulima yaliisha 11/april salama kabisa! After 2days kukaibuka vurugu za zilizoleta uharibifu wa miundo mbinu na uporaji wa mali za askari na raia pia! (msafara wa mamba..) ni vigumu kuubaini ukweli kwakweli!
 
Mmmh jaman huyu Makamu wa Rais amekuja saa ngapi huko, mbona leo mchana nimemuona akielekea njia ya White Sand"

Aliyekuja ni kamishna wa polisi Paul Chagonja ila sidhani kama kuna jipya atakalolifanya! kwasababu jana wakati akiongea na wananchi baada ya kutembezwa eneo la tukio ametoa kauli za kuwalaumu wananchi kwamba badala kuchoma moto ofisi ya ocd na maduka wangefungua kesi dhidi ya vyama vya ushirika lakn akaahidi kufanya upelelezi na kuubaini ukweli!
 
Ameongea na waathirika wa vipigo na moto? Alisema angeongea nao leo..
 
Wasi wasi wangu ni kwamba je, huo upelelezi utakuwa wa haki kweli kwani yeye mwenyewe tayari ameshaanza kuelekeza lawama kwa wananchi na kuwahusisha na uchomaji huo'
-hivi inawezekanaje mtu anayedai jasho lake halafu mtu huyo huyo akateketeza mali zake kwa moto?
-siku ya tukio hakukuwa na vurugu yoyote, kwanini polisi walizuia watu kuja kuokoa mali zao na kuziacha ziteketee kwa moto?
-jana askari walikuwa na operesheni ya kupiga, kuvunja maduka na kupora mali za raia vijijini, hii maana yake nini?
 
habari ya wewe mkuu! Vp kuhusu kikao cha leo hujapata taarifa bado?

Bado mkuu!

Ila saa 6 hivi,pale uwanjani ilipopaki "chopa",watu wamejaa wanamngoja huyo Kamishna wa Polisi.. Na eneo la tukio la moto pia wamejaa watu..

Ngoja nifuatilie..
 
Hii tetesi hata mm nimeipata kutoka kwa jamaa yangu aliyeko eneo la tukio.yani anasema mji/kamji ka Tandahimba kwa sasa hakuna kitu ni majivu tuu yamesalia
 
Wasi wasi wangu ni kwamba je, huo upelelezi utakuwa wa haki kweli kwani yeye mwenyewe tayari ameshaanza kuelekeza lawama kwa wananchi na kuwahusisha na uchomaji huo'
-hivi inawezekanaje mtu anayedai jasho lake halafu mtu huyo huyo akateketeza mali zake kwa moto?
-siku ya tukio hakukuwa na vurugu yoyote, kwanini polisi walizuia watu kuja kuokoa mali zao na kuziacha ziteketee kwa moto?
-jana askari walikuwa na operesheni ya kupiga, kuvunja maduka na kupora mali za raia vijijini, hii maana yake nini?
Ni kweli mkuu na jambo linaloshangaza kabla ya tukio askari Polisi
walianza kuhamisha Familia zao wakati ilishatangazwa kuwa kuna
amani - Jambo hilo liliwashangaza wananchi - Hii ni kwa mujibu wa
wananchi waliohojiwa na kituo cha TV cha TBC.

WASIWASI WANGU:
Kuna uwezekano wa 98% kuwa Jengo la OCD limechomwa na Polisi
wenyewe ili wapate kisingizio cha kuchoma moto soko na maduka na
kufanya wizi pia - hii ndiyo sababu walihamisha familia mapema.
 
Nasikia ni wananchi wametia moto kisa malimbkizi ya ela yao.
Nilifurai niliposikia hayo yametokea Tandahimba hii inaonesha kuwa nao wameamka kifuatacho ni kuipiga chini CCM.
Haiwezekani korosho kidogo tuu town utasikia buku 2 alfu nyie uko mwapunjwa.
Tia moto mpaka ofisi mnazotumia kufuatilia hayo malipo
 
Moto mkubwa ambao taarifa za awali zinasema umetokana na hitilafu ya umeme katika
ofisi ya upelelezi ya wilaya umeteketeza maduka kadhaa na soko zima la Tandahimba ikiwa
ni pamoja na ofisi hiyo ya upelelezi,
Habari za kuaminika kutoka kwa mashuhuda kadhaa zinadai kuwa moto huo ulianza majira
ya saa moja jioni jana. Jambo la kushangaza ni kitendo cha polisi kununua petroli na kwenda
kumwagia baadhi ya maduka huku wakiwazuia watu waliojaribu kwenda kufanya uokozi wa
mali zao.
HABARI YA UHAKIKA - mtu mmoja ambaye ana duka lake eneo hilo
(Abdalah Abdalah Camumkungu) alienda na gari lake eneo la tukio, hata hivyo alichomolewa
kwenye gari lake na kupata kipigo kikali huku akishuhudia askari wakiteketeza gari lake kwa moto.
Pia INASEMEKANA wananchi kadhaa wamelishuhudia tukio hilo la askari kuchoma moto maduka

Wakati huohuo: Leo Mkuu wa Jeshi la Polisi Saidi Mwema akiongozana na makamu wa Rais Dr.
Bilali wamewasili Tandahimba kwenda kutafuta suluhu ya mgogoro huo.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

kwa kurudiarudia neno 'inasemekana' inaonyesha jinsi usivyo n uhakika na unachokisema. Si kweli kwamba mwema na bilali wako tandahimba. Waliokwenda huko ni afande chagonja na rpc. Hebu tulinde heshima ya jf kwa kusema ukweli jamani!
 
Taarifa za awali tulizozipata wakazi wa Tandahimba zilisema kuwa hao ni
Mwema na Bilali. Hata hivyo kuna kiongozi ambaye hakutambulika ni nani
na aliwahi kurudi, kwa hiyo nafikiri mkuu GAZETI aliripoti kutokana na taarifa
za awali, hata hivyo kiongozi huyo ameondoka bila kufahamika ni nani, pia
inaonyesha kama kuna usiri fulani wa nani na nani waliwasili. Nahisi ni kwa
sababu za kiusalama zaidi kutokana na hali iliyopo.

Yote kwa yote taarifa aliyotoa GAZETI ni sahihi kwa asilimia 90% ingawa kuna
mkanganyiko kidogo wa nani aliwasili kutokana na wakazi wote wa Tandahimba kuwa
na Taarifa hiyo ambayo baadae ilionekana kuwa si sahihi. Hata hivyo hatujafahamu msafara
ule wa Helkopta wale wengine ni kina nani hususani waliowahi kurudi.
 
kwa kurudiarudia neno 'inasemekana' inaonyesha jinsi usivyo n uhakika na unachokisema. Si kweli kwamba mwema na bilali wako tandahimba. Waliokwenda huko ni afande chagonja na rpc. Hebu tulinde heshima ya jf kwa kusema ukweli jamani!
Nashukuru Vijisenti kafafanua hapo juu. INASEMEKANA - ni taarifa ambazo sina
uhakika sana lakini si vibaya kueleza. Niliposema HABARI YA UHAKIKA nina maana
kuwa ni habari ambazo nimethibitisha kwa 100% kutokana na chanzo ambacho
hakina shaka hata kidogo, hata hivyo msingi wa habari yenyewe unaonyesha
ukweli kwa kiasi kikubwa, hakuna haja ya kulaumiana vinginevyo kama ni mwakilishi
wa MAGAMBA ambao wengi wao hawapendi habari hii isikike.
 
kwa kurudiarudia neno 'inasemekana' inaonyesha jinsi usivyo n uhakika na unachokisema. Si kweli kwamba mwema na bilali wako tandahimba. Waliokwenda huko ni afande chagonja na rpc. Hebu tulinde heshima ya jf kwa kusema ukweli jamani!

na wewe pia ni mvivu wa kusoma post, mbona hilo limesha sahihishwa!
 
MAREKEBISHO.
Aliyewasili Tandahimba ni Paul Chagonja KAMISHNA WA OPERESHENI MAALUM na si Mwema
na Shein kama nilivyoeleza awali.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.[/QUOTE]

Chagonja tena ambaye huwa ana majibu kabla ya kufika eneo la tukio, tena majibu ya ki...... Yale ya Songea hatujayasahau.
 
Tandahimba ni mojawapo ya maeneo ambayo ccm inatumia ukilaza wa wananchi kuendeleza utawala wa kiimla. 2015 ndio nafasi yenu kutorudia kosa la kuichagua ccm

penda kuandika vitu kwa evidence co unagubikwa tu na ushabiki wa siasa.
 
Kamanda Chagonja na jopo lake leo wanasikiliza wafanyabiashara waathirika wa mioto na vipigo..

Na yanaandikwa maelezo ya kila mmoja..
 
Back
Top Bottom