HATARI: Naona matukio ya mauaji yakizidi kushika kasi nchini

rajiih

JF-Expert Member
Apr 4, 2019
429
652
Habari wana JF,

Poleni na majukumu ya kazi. Kwa pamoja tuliombeeni Taifa letu ili Amani yetu izidi kudumu daima, Tanzania social media zimekua na report kila leo kuhusiana na MATUKIO ya kikatili hii inaleta picha gani ndani ya Taifa letu tulivu.

Nabaki najiuliza watanzania wamepatwa na nn kiasi kutokugopa kutekeleza MAUAJI tena ya kikatili namna ya kuogopesha nauona msongo wa mawazo ukizorotesha na kuharibu kabisa tabia na mila za Mtanzania.
 
Hao wapenzi wakiuwanagaa nikickia hbr zao walaa sishtuki... Nikisikiagaa ulawiti kwa watoto na ubakaji yaan natamanigi serikalii ikiwakamataga hao wenye hzo kesi wawekee uraian tu wapigwee mawee mpk wafee waachee mambo yakuwajaza uko magerezan maninaaa zaoo...
 
Mwisho wa Dunia unakaribiaa wale wenye roho safi tutaenda mbinguni hao makatili makazi yao jehanamu
 
Juzi nilikuwa eneo fulani Tabora wilaya kama unaenda Mpanda na niliyoyakuta kule hakika Tz yetu imechoka sana na ina hari mbaya.

Nimekuta mauaji ya kutisha, watu wanavamiwa na kuuawa kwa staili ya kuchomwa shingoni. Si watoto, si wanafunzi, si wamama, si vijana wote wanawindwa na wakishauawa wanatupwa vichakani.

Sitaki kuongea sana juu ya niliyoyakuta kule ila najiuliza ni kwanini mauaji ya raia yameongezeka sana hawamu hii.

Ndo tuseme wafanyabishara wanapanga foleni sana kwa akina matunge?

Mitaji imekuwa sana sahivi kila mtu yuko huru kuipata damu ya binadamu mwenzie?

Najiuliza ikija kuwa 2025 wanasiasa nao wakaanza kujisafisha gundu na mikosi yao ni wangapi tutatwaliwa na ni wangapi tutasalimishwa.

Mungu awalinde na maalibino, balaa lao limerudi mtaani. Ilipita miaka kama 6 hivi sikuwahi kuyashuudia haya ila nadhani watu wamekumbuka kwenda kuvuna mazao yao mashambani. Ni hawamu ya kuvuna na kuvunwa
 
Mauwaji ni mengi sana.

Rais anapuyanga tu hataki hata kutengeneza nchi.
Sasa unataka raisi akakamate wanaouana kwa wivu kama kule mwanza?
Ukipita kila kona unakutana na movies za kivita unafikiri unategemea taifa la namna gani hapo
 
Na mauaji mengi yanahusishwa na pale ambapo sisi sote twapapenda
 
Sasa unataka raisi akakamate wanaouana kwa wivu kama kule mwanza?
Ukipita kila kona unakutana na movies za kivita unafikiri unategemea taifa la namna gani hapo
Rais anauwezo wa kuwafanya watu wakabadili mitazamo.

Atumie kila aina ya resources alizo nazo.
 
Rais anauwezo wa kuwafanya watu wakabadili mitazamo.

Atumie kila aina ya resources alizo nazo.
Sasa watu wanauwana chumbani kwa wivu wa mapenzi hizo resource ni zipi za kutumia hapo?
Pia tukumbuke raisi siyo mtu ni taasisi. Pale magogoni sasaiv yupo mtu kwenye ofsi ya raisi anakaimu. Unajua hivyo???
 
Sasa watu wanauwana chumbani kwa wivu wa mapenzi hizo resource ni zipi za kutumia hapo?
Pia tukumbuke raisi siyo mtu ni taasisi. Pale magogoni sasaiv yupo mtu kwenye ofsi ya raisi anakaimu. Unajua hivyo???
Hakuna mtu anakaimu Urais wewe.

Rais anatembea nao mwenyewe.

Hauta kaa ukaona mtu amesaini badara ya Rais. Never.

Kasome tena hiyo course..uliingizwa chaka.

Uishangae kuona Rais ametoa salama/teuzi tokea Omani.
 
Back
Top Bottom