Hatari: Mrembo anyonyoka nywele kwa Kusuka ‘Weave kichwani’

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,481
Nywele.jpg

Msemo wa Kiswahili wa wahenga ‘ukitaka uzuri dhurika‘ unaweza kuwa na maana kubwa katika mkasa huu wa aina yake unaowapa kiashiria ‘chekundu’ warembo duniani kote wanaopenda kuvaa mawigi na kusuka ‘ma-weaving’ kichwani kufunika nywele zao za asili.

Jasmine Collins ametoa taarifa kuhusu msichana wa miaka 23 ambaye amejikuta akinyoyoka nywele kama kifaranga chenye ugonjwa wa kuku, baada ya kutusuka ‘maweaving’ na kusuka mawigi kwa miaka kadhaa na kutozipa nywele zake halisi nafasi nzuri ya kupumua.

Collins amepost picha na video fupi zinazoonesha jinsi ambavyo msichana huyo ameathirika, na kueleza kuwa msichana huyo amemruhusu kupost picha hizo ili kuwasaidia wanawake wengine duniani kuepuka kilichomsibu.

“Ninasema tena, ngoja niwaambia kuwa mimi sio mpinga weaving na mawigi lakini huwezi kuishi nayo kila siku. Wateja wanafukuzia mitindo na wanamitindo wanafukuzia fedha na hakuna mtu anayesikiliza kuhusu umuhimu wa nywele. Hii lazima i-stop,” ameeleza Collins kwenye post yake aliyoiandika kiingereza na video ya msichana huyo.
 
wacha hivyo bwana,siku moja niliingia kwenya gari la matatu kama tunavyozinjua hapa kwetu,kuna dem alikuwa amenyeshewa hiyo weave ya kwake jamani nilishindwa kwani nimeingia kwenywe zizi la kondoo.ufundo kama kakondoo kaliko nyechewa.kwem



kwenye ngeli ya ka.
 
Maskini sorry for her,tujikubali jmn au kubadilisha hairstyles mara kwa mara
 
Serikali ikipige marufu nywele bandia punde tu baada ya kuzima simu zetu next week
 
Wapo wengi hapa Bongo walioathirika sababu ya mambo yaho. Wengi ni vibosire wa maofisini wenye vyeo vikubwa. Ukiwakuta majumbani mwao utakimbia.
 
Wapo wengi hapa Bongo walioathirika sababu ya mambo yaho. Wengi ni vibosire wa maofisini wenye vyeo vikubwa. Ukiwakuta majumbani mwao utakimbia.
Hahahahahahahah...... Umenikumbusha kipindi hicho natumia hayo makitu..... Sitaki tena kuyasikia kwa sasa
 
Back
Top Bottom