Hatari: Mabasi ya Mwendokasi V/s waenda kwa miguu

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,592
29,712
Mradi wa magari ya abiria maarufu Mwendokasi umeleta unafuu mkubwa kwa kwa watumiaji wa public transport. Uhakika wa kuwahi kufika destination umeongeza tija kubwa kwa shughuli za kiuchumi.

Ingawa bado kuna tatizo baya sana la ufinyu wa magari wakati wa peak time yaani asubuhi na jioni watu wanapoenda na kurudi makazini magari mengi yanalazimishwa kupaki au gari inaweza kutoka Kimara kwenda kupaki Jangwani bila hata kuchukua abiria wakati pale kituoni.

Turudi kwenye mada ya uzi huu. Hapo tarehe 17/08/2020 majira ya jioni eneo la Utumishi kulitokea ajali ya kutisha iliyokatisha uhai wa mwananchi mmoja. Eneo hilo hilo mwaka huu watu wameshuhudia ajali iliyosababisha umauti kwa mwanafunzi mmoja na watu wengine wawili. Ajali hizo zote zilitokana na mabasi ya Mwendokasi ambapo eneo hilo kuna alama ya wavuka kwa miguu (zebra crossing).

Sehemu mbalimbali jijini ajali kadhaa zimetokea ambazo zote wahanga ni watembea kwa miguu.

Hii hatari inayotokana na kasi ya magari haya inazidi kuongezeka huku wahanga
Wakiwa ni watembea kwa miguu.

Mamlaka husika iangalie namna ya kudhibiti mwenso au kuajiri madereva watakaofuata sheria za barabarani

IMG-20200817-WA0448.jpg

marehemu Ringo mkazi wa Kigamboni ambaye aligongwa na mwendokasi na kufariki tar 17/08/2020

4eea7c0e186e94ce6f2851e81bd25faf.jpg
pic%2Busafiri.jpg
 
hii ajari nimeishuhudia mwenyewe makosa makubwa yapo kwetu sisi unatembea barabarani unaongea na simu bila taadhali, ila cha kushangazam dreva alipiga hone ina maana alishamwona kuwa hayuko sawa, sasa basi speed ilikuwa kati ya 30-35 lakini breki haikufanya kazi vizuri
 
Ni jambo la kusikitisha sana jinsi mabasi hayo yanavopita kwenye alama za zebra. Alafu kuna mjinga humu kaleta hiyo habari anasema 'chanzo cha ajari kuchati', pumbavu kabisa.

Zebra ni zebra haijalishi mtu anachati au la, basi lilipaswa kusimama.

Pia madereva wengi wanao ujinga wa kupiga honi badala ya kushika breki, honi haisimamishi gari. Ukiona mazingira ya hatari cha kwanza ni breki na sio honi au kujaribu kukwepa.

Nimeumizwa sana na ajari hiyo ambayo ingeweza kabisa kuzuilika. Natumaini sheria itafuata mkondo wake kwa dereva kugonga na kusababisha kifo kwenye zabra.
 
Inauma sana.

Madereva wa mwendokasi hawaheshimu Zebra crossing. Ni bora zikafutwa basi maana hakuna usimamizi wala uwajibikaji
 
hii ajari nimeishuhudia mwenyewe makosa makubwa yapo kwetu sisi unatembea barabarani unaongea na simu bila taadhali, ila cha kushangazam dreva alipiga hone ina maana alishamwona kuwa hayuko sawa, sasa basi speed ilikuwa kati ya 30-35 lakini breki haikufanya kazi vizuri
Dereva angesimama....
 
Ni jambo la kusikitisha sana jinsi mabasi hayo yanavopita kwenye alama za zebra. Alafu kuna mjinga humu kaleta hiyo habari anasema 'chanzo cha ajari kuchati', pumbavu kabisa.

Zebra ni zebra haijalishi mtu anachati au la, basi lilipaswa kusimama.

Pia madereva wengi wanao ujinga wa kupiga honi badala ya kushika breki, honi haisimamishi gari. Ukiona mazingira ya hatari cha kwanza ni breki na sio honi au kujaribu kukwepa.

Nimeumizwa sana na ajari hiyo ambayo ingeweza kabisa kuzuilika. Natumaini sheria itafuata mkondo wake kwa dereva kugonga na kusababisha kifo kwenye zabra.
Umeongea point mkuu Unapofika kwenye zebra mwenye gari inabidi kusimama hata kma hakuna mtu Honi hazisaidii assume kama mtu mwenye matatizo ya usikivu ndo anapita Si Ndo yaleyale tu
 
hii ajari nimeishuhudia mwenyewe makosa makubwa yapo kwetu sisi unatembea barabarani unaongea na simu bila taadhali, ila cha kushangazam dreva alipiga hone ina maana alishamwona kuwa hayuko sawa, sasa basi speed ilikuwa kati ya 30-35 lakini breki haikufanya kazi vizuri
Kuna watu wanamatatizo ya usikivu unafikiri kwa situation kama hiyo honi itakuwa inamsaada gani?
 
Mradi wa magari ya abiria maarufu Mwendokasi umeleta unafuu mkubwa kwa kwa watumiaji wa public transport. Uhakika wa kuwahi kufika destination umeongeza tija kubwa kwa shughuli za kiuchumi.

Ingawa bado kuna tatizo baya sana la ufinyu wa magari wakati wa peak time yaani asubuhi na jioni watu wanapoenda na kurudi makazini magari mengi yanalazimishwa kupaki au gari inaweza kutoka Kimara kwenda kupaki Jangwani bila hata kuchukua abiria wakati pale kituoni.

Turudi kwenye mada ya uzi huu. Hapo tarehe 17/08/2020 majira ya jioni eneo la Utumishi kulitokea ajali ya kutisha iliyokatisha uhai wa mwananchi mmoja. Eneo hilo hilo mwaka huu watu wameshuhudia ajali iliyosababisha umauti kwa mwanafunzi mmoja na watu wengine wawili. Ajali hizo zote zilitokana na mabasi ya Mwendokasi ambapo eneo hilo kuna alama ya wavuka kwa miguu (zebra crossing).

Sehemu mbalimbali jijini ajali kadhaa zimetokea ambazo zote wahanga ni watembea kwa miguu.

Hii hatari inayotokana na kasi ya magari haya inazidi kuongezeka huku wahanga
Wakiwa ni watembea kwa miguu.

Mamlaka husika iangalie namna ya kudhibiti mwenso au kuajiri madereva watakaofuata sheria za barabarani

View attachment 1540930
marehemu Ringo mkazi wa Kigamboni ambaye aligongwa na mwendokasi na kufariki tar 17/08/2020

View attachment 1540921View attachment 1540922
Madereva wengi wa mabasi ya mwendokasi hawana tofauti na dereva wa bodaboda kwa kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi. Wanaongoza kwa kuvuka na taa nyekundu na kutosimama kwenye zebra crossing.

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom