Hatari katika ukweli wa hofu: Kisa cha dereva wa gari la farasi na wageni wa Count Dracula

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,863
2,000
HATARI KATIKA UKWELI WA HOFU: KISA CHA DEREVA WA GARI LA FARASI NA WAGENI WA COUNT DRACULA

Kuna movie ilikuwa maarufu sana katika miaka ya 1960 iliyochezwa na muigizaji ambaye alijipambanua kutoka waigizaji wengine kwa kucheza senema za kutisha akiitwa Christopher Lee.

Senema hii ilikuwa, "Dracula Prince of Darkness," Christopher Lee ndiye aliyecheza hiyo nafasi ya huyo Dracula.

Dracula alikuwa Count, yaani mtu tajiri aliyemiliki kasri na ardhi kubwa.

Dracula alikuwa amekufa miaka mingi lakini katika uhai wake aliishi kwa kunywa damu za watu.

Alipokufa mtumishi wake mtiifu akawa kamuhifadhi katika jumba lake juu milimani akisubiri kumfufua kwa kumpatia damu ya binadamu ambacho ndicho chakula chake kinachoweza kumfufua na kumpa uhai mpya.

Historia hii ya Dracula ilikuwa ikifahamika na wenyeji wote waliokuwa wanaishi chini ya mlima ule kwa hiyo basi walijiweka mbali na jumba lile na ilikuwa mwiko mkubwa kwao hata kutaja jina la Dracula.

Watu hawa wakafanikiwa kujenga ndani ya nafsi zao kuwa jirani sana na kijiji chao juu mlimani alipatapo kuishi Count Cracula mtu aliyekuwa na meno mawili yaliyotokeza nje ya mdomo wake, akitoka ndani mwake usiku wa manane tuu kwa kuwa mwanga wa jua unamdhuru kufikia kumuua.

Lakini wao kwa kuwa walihisi wako salama baada ya kifo chake wakajenga fikra ndani ya nafsi zao kuwa Dracula hakupata kuwepo wala hata rejea tena lau wakijua alihitaji damu tu ya binadamu mmoja kutoka kijijii kwao kufufuka.

Siku moja katika mji ule wakapita wasafiri wawili na wake zao walioharibikiwa na safari kwa kupotelewa na farasi wao ikabidi wakodishe usafiri wa gari la farasi pale kijijini.

Dereva akawachukua hadi kijiji cha pili nje kidogo akawaambia abiria wake kuwa hapo ndiyo mwisho hawezi kwenda zaidi ya hapo.

Pale walipokuwa ilikuwa katikati ya pori na kasri ya Count Dracula juu ya kilima iliyokuwa inapigwa na mwanga wa jua la asubuhi lililokuwa linachoza ilikuwa inaonekana katika ubora wake waziwazi.

Mmoja katika wale abiria akamwambia dereva kuwa wao safari yao inaishia kwenye kasri ile ya Count Dracula na akawa ananyoosha kidole chake cha shahada kuelekea jumba lile.

Dereva wa gari la farasi aliingiwa na hofu akashtuka kusikia kuwa abiria wake walikuwa wanataka wapelekwe kwa Dracula.

Bila hata kugeuza shingo yake kuangalia hiyo nyumba anayoonyeshwa alijibu kwa mkatao, "Hakuna nyumba hapo."

Wale wasafiri wakadhani hajaiona ile nyumba ya Count Dracula wakarudia kusema huku wakilinyooshea kidole lile kasri la Dracula.

Yule dereva akiwa dhahiri amehamaki huku akitetemeka kwa hofu aliwajibu kwa ukali bila kugeuza shingo kuangalia nyumba anayoelekezwa alijibu kwa ukali, "Mimi sioni nyumba yoyote hapo kilimani hakuna nyumba hapo."

Aliwatupia mizigo yao chini akagueza farasi waliokuwa wanakokota gari yake na mbio akarudi mjini.

Screenshot_20210216-183535.jpg
 

ujoka

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
2,244
2,000
Kwenye kazi ya fasihi andishi ,mwandishi humaanisha alichokiandika na zaidi
Hapa nimeelewa alichoandika mzee wetu sasa napambana kuelewa zaidi maana siamini kama mzee saidi leo kaamua kutuhadithia sinema tu ni lazima kuna ujumbe ndani yake ila kidizain nimeweza kumng'amua dracular mnywa damu ambaye wakaz wa kijiji kile wamedharau uwepo wake na atakuja kuwamaliza.
Bado naendelea ku brainstorm
 

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,863
2,000
Kwa sis wa saint kayumba tunapata tabu sana kuelewa makala zako ingawaje zinatuvutia.
Muuza Viatu,
Hapana unaelewa kwa ule uelewa wako na mwingine vilevile kwa uelewa wake.

Huyu dereva yeye ile nyumba anaijua vituko vyake na kaifunza akili yake kufuta kuwa ile nyumba ipo, ina mwenyewe na mwenyewe ni Dracula mtu mbaya.

Hataki kukumbushwa mtu yule Dracula anamuogopa hata kumuwaza ingawa kafa miaka mingi nyuma kiasi alipoonyeshwa nyumba yake akajibu kuwa yeye haoni nyumba hapo.

Sisi sote ni wanafunzi tunajifunza kufikiri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom