Hatari: Katibu Mwenezi CHADEMA Handeni Atishiwa Kuuawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatari: Katibu Mwenezi CHADEMA Handeni Atishiwa Kuuawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamende, Jul 21, 2012.

 1. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya wa Handeni mkoani Tanga Ndugu Omari Gomangilo ametishiwa kuuawa na Mhe. Diwani wa kata ya Komkonga (CCM) Mhe. Ramadhani Kisatu baada ya Mwenezi huyo kutoa mchango wake katika mkutano kwamba haoni sababu ya wananchi kuchangishwa kwa ajili ya huduma za hosipitali wakati hakuna dawa wala vipimo vinavyofanyika hosipitalini hapo.

  Akiwa amekwishatoa kauli hiyo iliyoshangiliwa sana na wananchi wa mji mdogo wa Kabuku, Mwenyekiti wa UWT aliyekuwepo eneo hilo alimwita Mhe. Kisatu ambaye alifika mara moja na kuanza kumtishia Gomangilo.

  Kisatu kwa kujiamini alimfokea Gomangilo kwa kumwambia kwamba atamfanya kitu mbaya maana kwanza ana hela na anaweza kumficha asionekane milele. Gomangilo alipomuuliza kama atamfanyia kama walivyomfanyia Dr. Ulimboka alimjibu "Nitakachokufanya wazazi wako hawatakaa wakuone tena" Hainichukui muda kukupoteza jumla mimi" alimalizia.

  Gomangilo kuona yamekuwa makubwa akaenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Kabuku ambako muda mfupi madiwani 6 wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Handeni walifika na kumsihi wakayamalize nje ya polisi. Hata hivyo Goma alikataa na ndipo polisi walipomuweka ndani Mhe. Kisatu na kumlazimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Handeni kumwekea dhamana hadi Jumatatu kesi hiyo itakapopelekwa mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa.

  uchunguzi wa kina umebainisha kwamba Uongozi wa CCM mkoa wa Tanga una ugomvi wa muda mrefu na bwana Omari Gomangilo ambaye amjiunga na CHADEMA baada ya kujivua gamba akiwa kiongozi wa UV-CCM hapo hapo Handeni na anaijua sana CCM. Uongozi wa CCM umekuwa ukifanya bidii kumtisha na kumfanya apunguze kasi lakini ameshindikana.
  Taarifa nyingine zimetua mezani kwangu kwamba mwezi Februari mwaka huu Mwigulu Nchemba alipita Komkonga akiwa njiani kwenda Arumeru, ambako alikutana na Mhe. Diwani Ramadhani Kisatu ambapo pamoja na majukumu mengine mipango ya kuzima moto wa CHADEMA ilipangwa.

  Wananchi wanasema kuwa kabla Kisatu hajakutana na Mwigulu mwezi Februari alikuwa mtu mpole na mkarimu sana. Lakini baada ya tu ya mwezi Fubruari amebadilika na kuwa mtu mwenye majivuno, anayejiamini kupia kiasi, mwenye matishio na mkatili sana.

  Wanajamvi hadi ninaleta ujumbe huu viongozi wa CHADEMA wilaya ya Handeni walikuwa kwenye kikao wakipanga namna ya kuhakikisha usalama wa Katibu Mwenezi wao na wao wenyewe.
  Ninaona sasa kwamba kila apitapo Mwigulu anaacha hofu kubwa kwa maisha ya watu na anavuruga sana utengemano na udugu katika jamii.
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kama hata Handeni CDM wanakimbiza basi ukombozi kweli uko mlangoni.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Hivi Mwigulu amekuwa tishio kiasi hicho? Wakati anaenda Arumeru alipitia Pwani, Tanga, Kilimanjaro na mwisho Arusha. Mbona huko kwingine sijasikia watu wakiwa wababe na wakatili baada ya Mwigulu kupita.

  Tanzania sasa fashion ni kutishiwa kuuawa. Bahati nzuri JF watu wengi tunatimia majina fake vinginevyo tungesikia kila mtu ametishiwa kuuawa. Ukitaka umaarufu tu basi sema umetishiwa kuuawa.
   
 4. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Huyu Nchemba asubiri dawa yake hapo 2016, tutakapo mshughulikia na ubunge tutauchukuwa 2015
   
 5. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwigulu ni Janga la Taifa!!.
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Wala sio janga la Taifa, ila ni upumbavu na ushamba ndio unaomsumbua huyu Kijana hana lolote la kuogopewa sema watu wanamlea, bado hajakutana na watu wanoamua kufanya kweli.
   
 7. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  haya sasa onother new movie begines from here......
   
 8. B

  Bob G JF Bronze Member

  #8
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mi sitaki ni amini moja kwa moja kwamba ccm sasa ni chama cha majmbazi ambacho sasa ni tishio kwa uhai wa Mtanzania mzalendo. Nasema siasa za vitisho hazina nafasi kwa sasa hata mahakama zetu tusipoziamini tutakwenda Mahakama za kimataifa zilizoundwa maalumu kwa viongozi vibaka wa kiafrika na Dhaifu
   
 9. only83

  only83 JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mwigulu ni freemason, na lile li skafu la bendera ya taifa uwa simuelewi kabisa ule sio uzalendo ni kamati ya ufundi.
   
 10. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,674
  Likes Received: 17,728
  Trophy Points: 280
  Kuhusu Mwigulu kutajwa hapo jibu lenu lipo kenye ''Signature'' yangu hapo chini
   
 11. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,674
  Likes Received: 17,728
  Trophy Points: 280
  Na Dr. Mkumbo kasema atamnywesha kwa lazima hiyo dawa......tutamnywesha ngao huyu domo
   
 12. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Liwalo na liwe,naam "liwe na liwalo".Ni upepo tu utapita.
   
 13. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Nimesikia kuwa kesho Diwani huyo fedhuli atafikishwa Mahakamani Kabuku, kwakuwa suala lenyewe sio jepesi kama linavyoonekana kwa juu. Huyu Katibu Mwenezi wa CDM wa Wilaya hiyo, kabla alikuwa ni M/kti wa UVCCM wa Wilaya hiyo, pia alikuwa ni Mkufunzi wa Makambi ya Vijana kama lile kambi la Ulemo kule Singida, alidhulumiwa ndio akahamia CDM, tangu amehamia CDM amehamasisha vijana wengi kuhama nae, na hivi sasa kwa kushirikiana na Makamanda wenzake wamekwisha weka uongozi kwenye kata zote za wilaya hiyo na hivi sasa yuko kwenye mchakato wa kuhakikisha vijiji na vitongoji vyote vya wilaya hiyo vinakuwa na viongozi wa uhakika. Aidha, wakati wa uchaguzi mdogo wa Arumeru, Wilayani Muheza pia kulikuwa na chaguzi ndogo za serikali za vijiji, CDM ilisimamisha wagombea katika vijiji 10 na kushinda 7, kampeni hiyo ilisimamiwa na Kamanda huyo. CCM ilishawahi kumbambikia kesi ya mauaji kama walivojaribu kumfanyia Waitara na Mnyika kule Singida lakini ikashindikana, taarifa zaidi zinasema kuwa Mwigulu alipopita maeneo ya Kabuku alikutana na Diwani huyo ambae anaishi Kata moja na Kamanda Gomangilo, na wamekuwa na mawasiliano ya moja kwa moja mara kwa mara. Diwani huyo amesikika akijitapa kuwa ameshapata maelekezo kutoka kwa Mwigulu kuwa asimcheleweshe sana Gomangilo, auawe kwa njia yoyote na muuaji atalindwa na CCM. Mipango ilishapangwa lakini Diwani huyo kwa hasira zake aliteleza na kuropoka kwa kujiamini mbele ya Gomangilo, ndipo sasa suala hilo likafikishwa Polisi, ambao nao kwa kuwa walishapata tetesi za mpango huo wakaona waoshe mikono na wapeleke Mahakamani licha ya shinikizo kubwa la kundi kubwa la viongozi wa CCM hadi wa Mkoa waliofika hapo kujaribu kuzuia. Kesho hapo Mahakamani, kama Kamanda Gomangilo ataachwa peke yake, atasukwasukwa sana na kukatishwa tamaa ili asiendelee na kesi, kwani imekaa vibaya na ushahidi ni mzito.
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Muhingo Rweyemamu at work -- paying tribute to his appointing authority!
   
 15. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Chadema imeenea Tanzania na pia nje kama hewa, huwezi kuizuia.
   
 16. C

  C-Amor Member

  #16
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  acheni kutuboa na upuuzi wenu wa siasa.
   
 17. M

  MgungaMiba JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 28, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 80
  Muhingo Rweyemamu? The new Handeni Dc? Duh!
   
Loading...