hatari iliyoko kwenye kivuko cha feery!!!

B.O.G

Senior Member
Feb 17, 2011
144
40
Kivuko cha fery huwa kina beba waenda kwa miguu, baisikeli, magari na kadhalika.chakushangaza ni kwamba unakuta watu wamejazana pamoja na magari na wakati huohuo waendao kwa magari walio wengi wakiisha ingiza magari yao kwenye chombo hawazimi engine za magari yao, wao ni kujifungia humo kwenye magari yao yenye full Ac maana wana aleji na harufu ya soko la samaki,huku sisi akina kabwlela tukibugia moshi wa magari yao. Hivyo naomba wewe unayeingiza gari lako kwenye ferry ulizime mara moja na wahusika wajaribu kuliangalia hilo.
 
Mara nyingi huwa naona walizi wakiwafuata Madereva na kuwaambia wazime gari zao, Ningependekeza waandike Ujumbe kwenye zile ticket za magari kwa maandishi makubwa kuwa uwapo ndani ya ferry ni lazima kuzima gari na likikutwa liko on wakati ferry inatembea kuwe na faini.
 
Back
Top Bottom