HATARI: First long drive na Familia mwisho wa mwaka

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Kuna ulimbukeni mkubwa wa baadhi ya watu kuendesha umbali mrefu na familia zao kwenye gari ndogo kwenda kusalimia ndugu , jamaa na marafiki huko Mikoani..

Barabarani ajali ni nyingi sana za magari madogo Vs malori au mabasi.. kimsingi gari ndogo zinapigwa sana.

Mtu amenunua gari ndogo mwisho wa mwaka, anaendesha umbali mrefu akiwa amebeba familia yake kwenda Mkoani wakati leseni yenyewe ni ya kununua na pia hajawahi kusafiri (alone) kwa umbali mrefu akiwa anaendesha.

Familia zinapotea, gari zinaharibika, hasara juu ya hasara!

Ni bora ukodi dereva akuendeshe then mkifika anakuachia gari yako, siku ya kurudi unamuita tena. Au unaogopa Kijijini utaonekana hujui gari?

Tuache ushamba, tutamaliza familia zetu. Tusiwe malimbukeni kwa vitu vidogo.
 
Jamani mbona Mimi natoka dar naenda katavi Kwa gari Dogo,
Na ninarudi salama bin salmini? Nafikiria inategemea ntu na ntu
 
Mleta mada unapaswa kufahamu haya, kuhusu watu wanaosafiri na familia zao kipindi hichi kwa kutumia usafiri binafsi (hata kama ni gari ndogo)

1. Wanafanya hayo kupunguza gharama za nauli na usumbufu.

2. Wanajaribu kutumia uhuru wao kufurahia maisha na kufurahi pamoja (Safari ni starehe ikiwa utatumia usafiri binafsi na mkiwa wengi)

3. Wanataka kusafiri kwa uhakika zaidi kwenda na kurudi (Kipindi kama hichi cha sikukuu usafiri wa mabasi umezungukwa na kero, fujo, ujanja ujanja, uhuni na usanii mwingi. Kwa mtu anayesafiri na familia huenda atateseka sana)

4. Mtindo wa kimaisha katika kujionyesha (kule unakokwenda) kuwa wewe sio maskini na unaishi mjini vizuri. (Ni jambo la kawaida kwa binadamu kujivunia na kujisikia kila analipia hatua moja ya kimaisha).

5. Watakuwa na nafasi njema na huru kuutumia huo huo usafiri kwa mizunguko ya ndani ya jamii huko wanakokwenda.
 
Kwanini wasipande ma-bus au Ndege Mtu ana-drive Ist Mwendo wa DAR to Bukoba ,

ujinga ni tatizo mfano huyu Balozi anendesha crown dar to Moshi kwanini hataki kupanda Ndege au bus , Mambo mengine ni akili
 
Kifo huwezi kuzuia lakini usilamishe kifo . Hela ya kupanda bus unayo unapanda tu au Ndege

Wachaga wengi na wahaya wanapata Sana ajali wanagongwa na maroli Makubwa
 
Mleta mada unapaswa kufahamu haya, kuhusu watu wanaosafiri na familia zao kipindi hichi kwa kutumia usafiri binafsi (hata kama ni gari ndogo)

1. Wanafanya hayo kupunguza gharama za nauli na usumbufu.

2. Wanajaribu kutumia uhuru wao kufurahia maisha na kufurahi pamoja (Safari ni starehe ikiwa utatumia usafiri binafsi na mkiwa wengi)

3. Wanataka kusafiri kwa uhakika zaidi kwenda na kurudi (Kipindi kama hichi cha sikukuu usafiri wa mabasi umezungukwa na kero, fujo, ujanja ujanja, uhuni na usanii mwingi. Kwa mtu anayesafiri na familia huenda atateseka sana)

4. Mtindo wa kimaisha katika kujionyesha (kule unakokwenda) kuwa wewe sio maskini na unaishi mjini vizuri. (Ni jambo la kawaida kwa binadamu kujivunia na kujisikia kila analipia hatua moja ya kimaisha).

5. Watakuwa na nafasi njema na huru kuutumia huo huo usafiri kwa mizunguko ya ndani ya jamii huko wanakokwenda.
Hapo kwenye kusave nauli sizani .safari ndefu una weza tumia hela ndefu kuliko ata nauli ambayo mnge tumia kwa bus
 
Lete Maneno.......................
By JK Wa Msoga Chalinze Pwani Tanzania.

Tunawatakia Wote Safari Njema Mnaosafiri Na Gari Binafsi Ama Bus Popote Mnapokwenda Tanzania Na Nje Ya Nchi.

Muhimu Mkafurahie Maisha Mwisho Na Mwanzo Wa Mwaka.

Watu Wasafiri.
 
Kwa safari ndefu ya karibu mfano dar Dodoma au singida, dar iringa, dar mtwara, dar Kilimanjaro/ Arusha ni heri utoke saa 9 usiku, mpaka saa 2 asubuhi utakua umefika robo tatu ya safari yako , hapo unaendesha mdogo mdogo .
 
Actually huwa nikiwa naaanza safari then nikawa nasafiri na familia yangu nzima hata kama ni public transport huwa nabadilika rangi ya ngozi.

Huwa napenda tugawanyike katika makundi maana hizi genes zangu zinaweza kuwa terminated kama mzaha vile.Ushauri wangu hata kama destination ni moja msipande chombo kimoja BABA,MAMA na WATOTO.

Hizo fanyeni kwa safari za hapa mjini mkienda church au mkienda Beach
 
Back
Top Bottom