Hataki niangalie wanawake wanaojidhalilisha kuvaa nusu uchi

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,062
103,260
images.jpeg

Mwanamke anayejidhalilisha kwa kuvaa vibaya

Napotoka na shemeji yenu nakuwa siko huru kabisa. Ukiwa naye kwenye party au event fulani ni hatari zaidi hataki kabisa niangalie pembeni.

Nimeshamwambia napoangalia wanawake wapembeni yetu sio kwamba nawatamani isipokuwa nawashangaa walivyovaa nusu uchi,nawashangaa wanavyojidhalilisha

Ieleweke sio kila mwanaume anapotazama wanawake wanaopita machoni mwake basi anatamaa lah hasha,wengine tunakua wakushangaa mambo yanayoendelea duniani
 
Kwa nini mnawahukumu kwamba wanajidhalillisha? Pengine huo ni utamadduni wa kwao!
 
usimuone mjinga kukwambia hvyo kuna wanawake wamejaliwa kuliko yeye anaogopa ataibiwa maana wapo walio mzidi viwango.
 
View attachment 752299
Mwanamke anayejidhalilisha kwa kuvaa vibaya

Napotoka na shemeji yenu nakuwa siko huru kabisa. Ukiwa naye kwenye party au event fulani ni hatari zaidi hataki kabisa niangalie pembeni.

Nimeshamwambia napoangalia wanawake wapembeni yetu sio kwamba nawatamani isipokuwa nawashangaa walivyovaa nusu uchi,nawashangaa wanavyojidhalilisha

Ieleweke sio kila mwanaume anapotazama wanawake wanaopita machoni mwake basi anatamaa lah hasha,wengine tunakua wakushangaa mambo yanayoendelea duniani
Na je, unaweza kugeuka ikiwa unapishana na Mwanamke mchafu aliyevaa kandambili na kanga iliyochanika?
 
Labda uvaaji wake ni upi??

1.Kama anavaa nguo za staha na heshima za kufunika mwili wake.....
Heshimu hisia zake labda ikiwa nawe unataka awe uchi kama hao wengine.

2.Kama uvaaji wake ni wa kufanana na hao (wa uchi)....
Ni wivu tu ndiyo unamsumbua kuhisi labda wanapendeza zaidi kumshinda yeye na ndiyo maana macho yanakutoka.

Ama huwenda ulimwambia unapenda anapojistiri vyema naye akakusikiliza kisha unamgeuka kwa kuwakodolea wengine badala yake na amevaa ulivyotaka wewe.... Huoni unamkosea mkuu?
 
"Eyes are never quiet"
Jaribu kuepuka dhambi na ushukuru upo na huyo anaekuchunga na tamaa zako
 
Back
Top Bottom