Hataki kunipikia, pia hataki tuwe na house girl

caxton

Senior Member
May 8, 2015
145
149
Wandugu nawasalimu,

Huyu fiancee wangu ambae ninaishi nae ni mjamzito, ana mimba ya miezi sita kuelekea saba, hataki kupika chakula anasema hajisikii vizuri hivyo hawezi kupika, house alimfukuza yeye mwenyewe mwanzoni mwa ujauzito kwa madai kuwa ataniiba mimi, kwa kuwa alikua mzuri sana.

Kwa muda mrefu tumekua tukila take away food from outlets, mostly chips kufikia hatua nimeshachoka, juzi nimemuomba aanze kupika akageuka mbogo na kudai nipike mwenyewe kama vipi, wadau huyu ni mchumba tu najibiwa hivyo akiwa mke je?

Nimeanza kupata wazo la kurudi kwa Stella niwe nakula huko kabisa ndipo nirudi home, sijui mlikua mnasemaje?
 
Last edited by a moderator:
Yani mchumba kivipi?? umeruhusiwa kuishi nae na wazazi wake??
 
Mnatakiwa kupata elimu ya ndoa kabla ya kuoana

Huwa kuna mabadiliko yanatokea wakat wa ujauzito na baada ya kujifungua. Hivo bhac unatakiwa kujua.
 
yaani huyo mjamzito ilibidi sana umpikie dagaa kauzu mwanangu hujui tu, ingia jikoni karangiza mkuu
 
Wewe ni mbinafsi, huyo unaemuita mchumba wako ni mjamzito na wafahamu kabisa jinsi mimba zinavyokuaga na complications mfn.kuchukia baadhi ya vitu mfn harufu ya viungo vya chakula,perfumes etc.kakwambia hawezi kupika cause hajisikii vizuri mbioo ushakimbilia Jf kuanzisha uzi, siku akikwambia akikuona anajisikia kichefu chefu si ndo utahamia kwingine na usirudi tena?kama unaweza kupika ukamsaidia kupika japo mara moja moja mtu aliyekubebea kiumbe chako utapungukiwa nini?unafikiri kubeba mimba ni kazi ndogo?haya hamia kwa huyo stella maana umepata kisingizio
 
Hiyo kawaida kwa mjamzito muda mwingine kisirani ni kawaida.pika tu kwani unapungua wapi?
 
Nenda tuu kwa stella but makesure stella asijekuwa nyumba ndogo.
 
Huna mikono?
Kama kipindi cha mpito unamuwaza stella huko mbele si utahamia kabisa???
Huyo mwanamke hajui kama kuna wakina stella? Wanawake kujilegeza tuu. ndio maana bithcomplication zinaongezeka
Ngoja wamsaidie majukum.
 
Huyo mwanamke hajui kama kuna wakina stella? Wanawake kujilegeza tuu. ndio maana bithcomplication zinaongezeka
Ngoja wamsaidie majukum.

Complication kama ipo ipo iwe unejilegeza au umejikaza..... kuna baadhi ya kaka zetu wanahitaji jando walahiiiio

Au anafikiri huyo mwanamke wake hatamaniwi? Tena wajawazito walivyo na joto sasa chaaaaaaaa...
 
Kama kuna ndugu wa karibu wa upande wako ambae yupo yupo tumuombe uishi nae amsaidie kazi ndogo ndogo
 
Complication kama ipo ipo iwe unejilegeza au umejikaza..... kuna baadhi ya kaka zetu wanahitaji jando walahiiiio

Au anafikiri huyo mwanamke wake hatamaniwi? Tena wajawazito walivyo na joto sasa chaaaaaaaa...
Khaaaaa.....kwa vile anatamaniwa ndo alipe kisasi?

Wanawake bwana acheni kujilegeza legeza mbona wazamani walikuwa pamoja na ujauzito wake anapasua kuni, anachota maji n.k siku ya kuzaa inakuwa very simple.

Huyo dawa yake tu jamaaa ale kwa stella. Akirud hom anajifunika shuka paka asubuh
 
Anamimba tena kubwa unataka apike daah yaani nilivosoma hako kichwa cha habari nikajua tatizo mimba msaidie bana acha hixo ww jamaa wakati ashasema hawexi na bado subiri ajifungue sasa mapenzi yote yanahamia kwa dogo
 
Zamani walikuwa hawapati complication?
Takwimu ya Vifo vya ujauzito zamani ilikuwa chini????????

Khaaaaa.....kwa vile anatamaniwa ndo alipe kisasi?

Wanawake bwana acheni kujilegeza legeza mbona wazamani walikuwa pamoja na ujauzito wake anapasua kuni, anachota maji n.k siku ya kuzaa inakuwa very simple.

Huyo dawa yake tu jamaaa ale kwa stella. Akirud hom anajifunika shuka paka asubuh

Aende tu kwa Stella...mkewe ataenda kwa john
 
Zamani walikuwa hawapati complication?
Takwimu ya Vifo vya ujauzito zamani ilikuwa chini????????

Aende tu kwa Stella...mkewe ataenda kwa john
Kwa mazingira ya zamani kutokana na acces ya medical services....

Siku hizi kitakwimu pia, wanaojifungua kwa upareshen imeongezeka, pamoja na sababu nyengine but hii ya mtu akiwa na mimba kujilegeza hataki kujishughulisha na vjikaz vdogo dogo.

Hapo kwa joni, inakuwa ngoma dro
 
Back
Top Bottom