Hata waongeze mwezi mzima zoezi la sensa halitafanikiwa 100%

Aaron

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,019
4,693
Kwa wale mnaofatilia vyombo vya habari na jinsi hali halisi ilivyo kwa zoezi la sensa linaloendelea ni kwamba halitafanikiwa kwa 100%.

Changamoto ambazo serikali imeshindwa kukabiliana nazo ni pamoja na.

1.swala la uislamu ambalo kwa takwimu mpaka sasa zaidi ya kaya 2000 kwa jiji la Dar es salaam zimegoma kuhesabiwa..je, kwa mikoa mingine itakuwaje

2. Serikali kushindwa kuwalipa wenyeviti wa mitaa. Sababu hii ndiyo tishio kubwa hata ukiachana na swala la uislamu kwani viongozi hawa wa mitaa ndiyo wanajua kaya walizonazo hivyo kutowashilikisha hasa kwa kuwapa chochote zoezi hili hata uongezwe mwezi mbele halitofanikisha lolote.

3. Hali mbaya ya uchumi wa mtanzania ni mbaya hivyo waliokata tamaa na maisha hawaoni umuhimu wa kuhesabiwa.
 
Lakini ukisikia usaniii ndio huuuuu, ijumaa walisema wamefanikiwa 80%, inamaana hizi siku mbili watakuwa wamepata angalau 10% na kufikia 90%.....sasa wanaongeza wiko nzima kwa hiyo 10% au taarifa yao ya awali ilikuwa ya kupika?
 
Naomba kujuzwa, je? Hawa makarani wameongezwa na tena posho? Kwa hzo cku 7

kiongozi wao jana kasema watalipwa kulingana na mkataba.. Sijui mkataba wao unasemaje..mwenye kujua atujuze
 
Failed exercise,wanajaribu kufunika kombe mwanaharam apite,hata bila waislam kugoma zoez limekwama kwa maandaliz mabovu kila kitu ndani ya utawala huu hakiendi vizuri sijui kwa nini
 
Mimi mpaka sasa sijahesabiwa. Mwenyekti wa mtaa (ccm) anakaa mita 100 na balozi (ccm) anakaa mita nyingine kama 50 toka kwa m/kiti wa mtaa.

Juzi nimempa m/kiti lift akasema anafuatilia mishe mishe zake sensa sio ishu kwake. Aksema akirudi "angeniftafuta", pata picha! Hajanitafuta na tuliacha geti wazi ili sio tu wapige kengele bali waingie uani kabisa lakini mpaka muda huu hakuna dalili za kuhesabiwa.

Hapa ni mjini hali iko hivyo je huko vijijini? Hapa watu wawajibishwe kwa fedhaha na hasara hii kubwa. Lazima tubadilike
 
Wegine Hatukumbuki hata jana tulikula nini,tutakumbuka vipi nani alilala 26 Agosti.
 
Naomba maswali yangu yajibiwe na wahusika:

1) Je, fedha iliyotengwa kwa ajili ya sare za makarani imeenda wapi?

2) Madodoso mbona hayatoshi?
 
Kiongozi wao, huyo kamishna wa sensa, naona sasa ameamua kutumia nguvu na ubabe, hawana tena uwezo wa kutumia busara na hekima, kushawishi watu, kwa matatizo yaliyoasisiwa na brother.

Kama hata hili, la wazi kabisa, wanashindwa na kuamua kutumia nguvu, mengine wataweza?
 
Wikipedia wanasema failed Government sasa naona imeamua kuwatoa kafara makarani kwa siku7 bila malipo kwa uzembe uliosababishwa na JK na wahujumu wenzake...

iweje leo uwaambie watu wafanye kazi bila malipo angali ww ndo kikwazo wa zoezi?kinachofuata ni kuharibu morali ya kazi na kuharibu kabisa maana yote ya sensa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom