Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,393
Kama imetokea, ni mara chache sana wanaume wanaonunua miili ya wanawake kuzongwa na jamii. Kama ikitokea ni pale tu mwanaume fulani anaposhindwa kujilinda ipasavyo hadi siri yake ya kwenda kwa makahaba ikatoka.
Kwa kawaida wanawake ndio ambao wanalaumiwa, kutukanwa, kukashifiwa na kupata kila aina ya mzigo unaohusiana na ukahaba. Ni kama vile mwanamke anajiuza na kujinunua mwenyewe au kununuliwa na wanawake wenzake. Mwanaume ambaye bila yeye kwenda kununua mwili wa mwanamke, biashara ya ukahaba haiwezi kuwepo, huwa hatajwi kabisa linapokuja suala la kujadili ukahaba.
Bila shaka ni hali kama hii ambayo inawafanya watu wengi kudhani kwamba wanaume hawahusiki kwenye ukahaba, yaani wanashawishiwa na wanawake ambao kujiuza ndio shughuli yao. Kuvaa nguo fupi na mikao ya kihasara pamoja na vitimbwi vingine vimehesabiwa kwamba, ndivyo vyenye kumshawishi mwanaume kuingia kwenye kununua mwili wa mwanamke.
Inaonekana kama vile mwanaume anasamehewa kwa udhaifu wake wa kushindwa kujizuia anapoona maungo ya siri ya mwanamke, hivyo kosa ni la mwanamke ambaye amemshawishi. Lakini taarifa za kitaalamu zinazohusiana na ukahaba zinaonesha kwamba, hata kama wanawake wangekuwa wanavaa nguo ndefu zinazoburuza chini, ikishabainika kwamba ni makahaba, wanaume watamiminika kuwanunua.
Suala hapa siyo kushawishiwa na wanawake wanaojiuza. Wanawake wanaojiuza hujipitisha na kujinadi mbele ya wanaume kwa kuwahi tu kupata wateja, lakini hata wao wanajua kwamba, hawahitaji kujinadi kwa wanaume……………………….