Hata wanaoitabiria CCM kifo wakifa CCM haitapona (MAKALA) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata wanaoitabiria CCM kifo wakifa CCM haitapona (MAKALA)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ndiyomkuusana, Sep 26, 2012.

 1. ndiyomkuusana

  ndiyomkuusana JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Na Juvenalis Ngowi

  INGAWA dini zetu karibu zote hutufunza kwamba kuna maisha baada ya maisha ya ulimwengu huu, tena wengi tunaamini ni maisha mazuri na bora kabisa, bado ni muhali kukuta watu wakiombea hata maadui wao kifo. Kifo kimeendela kuwa jinamizi kwa wanadamu.

  Ni katika kutambua hilo ndiyo maana Kionambali anashtushwa sana kusikia Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisema kwamba wale wanaosema CCM itakufa, watakufa na kuiacha CCM. Hii ni dua isiyo sahihi kutoka katika kinywa cha rais wa nchi.

  Kifo cha CCM kinachotabiriwa ni tofauti kabisa na kifo cha wanadamu. Tunaoitabiria CCM kifo tunatabiri kuanguka kwake na kupotea katika utawala wa taifa hili. Na historia ni mwalimu asiyedanganya. Ziko wapi dola za Rumi zilizotawala karibu miaka elfu moja? Zilianguka na kusambaratika. Sasa zinasomwa katika historia.

  Yuko wapi Dk. Hastings Kamuzu Banda wa Malawi aliyejitangaza rais wa maisha? Alikufa na kuzikwa bila madaraka yoyote. Iko wapi KANU ya Kenya? Hii ni mifano michache sana ambayo inatosha tu kuthibitisha kwamba kufa kwa taasisi au kupotea kwa taasisi ni ukweli wa kihistoria, si dhana ya waandishi wala wanasiasa.

  Lakini ukiacha ukweli huu wa kihistoria ambao utaikuta taasisi yoyote ile, bado kuna ishara za wazi kwamba sasa CCM inafika ukingoni katika kuendelea kutawala nchi yetu, kwa kutumia mihula miwili ya kwake mwenyewe kupima namna inavyofanya kwenye siasa za nchi hii.
  Mwaka 2005, Rais JKikwete alishinda uchaguzi kwa asilimia 80.28. Ushindi wa dhoruba. Mwaka 2010, matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi yanaonyesha Kikwete alishinda kwa asilimia 61.17. Hili ni kama poromoko la asilimia 20. Huwezi kuona mporomoko huo kwa kipindi cha miaka mitano na bado usipate wazo la CCM kuanguka?

  Lakini tutazame zaidi. Nguvu iliyotumika kupata hizo asilimia 61.17 si haba. Tuliona namna CCM ilivyobebwa na serikali katika mbio hizo za urais. Kuna kila sababu ya kuamini kwamba kama uwanja wa mapambano ungekuwa sawa, bila shaka kura za mgombea wa CCM zingepungua sana.

  Na ikumbukwe, Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa akigombea akiwa pia ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huwezi kupuuza jambo hili. Kuna mazingira ambapo inakuwa vigumu kujua Kikwete anazungumza jambo katika nafsi ipi. Anazungumza kama rais au kama mgombea?

  Maana alikuwa na nafsi zote hizi mbili wakati wote wa kampeni za pili. Ni ngumu kukataa kwamba hili halikuipa CCM faida ya ziada katika kampeni na hivyo anguko la CCM kimsingi ni kubwa kuliko asilimia 20 ukilinganisha na miaka mitano iliyokuwa imetangulia.

  Jambo jingine ambalo liliipa CCM ahueni katika uchaguzi wa mwaka 2010 ni ukweli kwamba CCM iliendeleza ule utamaduni wa kumwachia rais aliyepo amalizie mihula yake miwili. Maana yake ni nini? Maana yake CCM haikuwa na mparanganyiko katika kukimbilia Ikulu katika uchaguzi uliopita. Walikuwa na mgombea ambaye tayari alishapatikana miaka mitano nyuma. Ilikuwa kama vile wanahuisha tu mkataba wake wa kukaa Ikulu. Katika hili udhaifu wa CCM haukuonekana bayana.

  Ulijificha nyuma ya kanuni ya mazoea. Hali halisi sivyo ilivyo kwa sasa. Kwa sasa tayari tunafahamu na hakuna kificho kwamba CCM imegawanyika kwa misingi ya tamaa ya wanaotaka kuingia Ikulu. Wanapingana wenyewe kwa wenyewe.

  Wanatuhumiana wenyewe kwa wenyewe na imefika mahali wanasema wao wenyewe kwamba "patachimbika". Huu ni ushahidi wa CCM iliyochoka na inayopumulia mashine. Kwa nini isife katika mazingira haya ya kugombana ili kunyakua madaraka?

  Na katika mpambano huu wa madaraka tayari CCM wameanza kujibagua wenyewe kwa wenyewe. Sasa kuna magamba wanayotaka kuyavua na bahati mbaya inasemwa mengine yamevuka hadi kiunoni kisha yakakwama. Huu si ushahidi wa kifo cha CCM? CCM ilianza kufa pale ilipoua Azimio la Arusha.

  Ni ngumu kutuaminisha kwamba CCM inaweza kudumu nje ya misingi ya uasisi wake. CCM ya wakulima na wafanyakazi haiwezi kucheza ngoma ya kibepari halafu ikabaki salama. Itakufa kwa sababu imeua mizizi yake. Huu si utabiri wa mwandishi ni ukweli wa kimantiki.

  Bado tunafahamu kwamba kwa kiais kikubwa ushindi wa CCM mwaka 2005 ulitokana na nguvu ya mtandao. Nguvu hiyo kwa sasa haipo na hata wanapozungumza hadithi za magamba wenye akili tunafahamu hao wanaoitwa magamba ni akina nani. Na ndiyo maana baadhi yetu tulidiridiki kusema hakuna mwenye ubavu wa kuyavua hayo magamba maana kuvua gamba ni kujimaliza.

  Hii nguvu ya mtandao sio ya kubeza, lakini bahati mbaya haipo tena. Tuliwahi kusikia kwamba ilifika mahali kukawepo mtandao maslahi na mtandao matumaini. Wapo majeruhi wa mtandao ndani ya CCM na wapo walionufaika. Maana yake ni kwamba ndani ya CCM kuna upinzani mkubwa wa ndani kwa ndani na kwa wanaofuatilia matamshi ya watu wa aina ya Samuel Sitta unaweza kujua kabisa kwamba hali si shwari. Huu ni ushahidi mwingine wa CCM kufikia mwisho wa zama zao katika kutawala.

  Kuna jambo jingine ambalo CCM labda hawajaliona na hivyo kuwabeza wale wanaosema kwamba chama hicho kinafikia mwisho wa kutamba katika siasa za nchi yetu.

  Kabla ya Dk. Willibrod Slaa kutangazwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA, chama hicho pamoja na kwamba hakikuwa hoi sana, lakini hakikuwa kimetoa changamoto na kuwa kikubwa kama ilivyotokea baada ya mwanasiasa huyo kutangaza na hatimaye kugombea urais wa Tanzania.

  Pamoja na madhaifu ya CCM niliyoyajadili hapo, ukweli ni kwamba CHADEMA wamejipambanua kama chama kinachotoa mtikisiko mkubwa kwa CCM. Kwa maneno mengine CHADEMA wanaonekana kuisindikiza CCM katika kaburi lake la kisiasa. Na CCM wanafahamu hili bali hawaamini kinachotokea.

  Hakuna ubishi kwamba baada ya uchaguzi wa 2010, wananchi wamepata hamasa kubwa sana ya kujiunga na kuukubali upinzani hapa nchini. Hata idadi ya wabunge wa upinzani inadhihirisha ukweli huu.

  Ugumu wa CCM katika kampeni za Igunga na Arumeru Mashariki ni uthibitisho wa nguvu waliyo nayo wapinzani katika siasa za leo na kudumaa kwa CCM katika siasa hizo hizo.

  Jambo moja tu linaloweza kuweza kurefusha kidogo maisha ya kisiasa ya CCM ni kurudisha matumaini ya watu waliokata tamaa. Maisha ni magumu. Kama hawataweza kupunguza ugumu huu wa maisha, hakika CCM inatakiwa kusema buriani na kupisha wengine wachukue uongozi wa taifa hili.

  Ni kweli kwamba hatuna mkataba na Mungu kuhusu maisha yetu na hivyo ni kweli kwamba inawezekana baadhi yetu tukavuta pumzi ya mwisho kabla CCM haijafa kama alivyotabiri rais Kikwete, lakini vifo vyetu havina maana CCM itadumu. Nauona mwisho wake bila kujali mimi niko hai au mfu!

   
 2. ndiyomkuusana

  ndiyomkuusana JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Na Edson Kamukara | Tanzania Daima | 26, Sept 2012

  MWENYEKITI wa Chama Cha Mpinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, bado haamini kama chama anachokiongoza kimekufa. Badala yake ametoa tambo kuwa wale wote wanaokichulia kifo, watakufa wao kabla ya chama.

  Kikwete anapima uhai wa CCM kwa kuangalia wingi wa wanachama wanaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama bila kujali kama wana sifa stahiki au hapana.

  Kauli hii ya mwenyekiti ni nzito yenye kuhitaji ushupavu katika kuitamka hasa unapozungumzia na kusifu kitu dhaifu ukiamini kuwa bado kiko imara.

  Pengine nikuulize wewe unayesoma makala hii, hivi ni kweli Rais Kikwete hajui kuwa CCM imekufa siku nyingi hasa baada ya yeye kuchukua wadhifa wa mwenyekiti?

  Nauliza hivyo kutokana na utata wa kauli ya Rais Kikwete. Huyu anajaribu kujipa matumaini ambayo hayapo tena. Kama ni kupima uhai wa CCM kwa sasa ni sawa na mgonjwa aliyeko mahututi ICU akipumulia mashini yaani nusu mfu.

  Kwanini Kikwete anasema CCM haitakufa wakati imekuta tayari. Hivi anaweza kuifananisha miiko ya chama kwa sasa na ili ya miaka kadhaa iliyopita. Kweli anaamini anaongoza chama cha wakulima na wafanyakazi wanyonge?

  CCM aliyorithishwa Kikwete ilikuwa ya wafanyabiashara, mafisadi na uongozi wa kupokezana kifamilia? Kama si hivyo kwanini mwenyekiti huyo amediriki kuwahadaa wajumbe wa Kamati Kuu kuwa chama hicho hakitakufa, anataka kife mara ngapi?

  Rais amesahau kuwa hata dhana ya kujitakasa upya aliyoiasisi mwaka jana ya kujivua gamba imeshindikana kutekelezeka kwa sababu mafisadi aliyokuwa amewalenga kuwang'oa wamejijengea mizizi kwenye chama kuliko yeye.

  Jamani mwenyekiti huyu anataka tumpe mifano gani zaidi ili atambue kuwa CCM anayoiongoza imekufa, haina dira, mwelekeo na sasa imeishia kudandia hoja za wapinzani ndani na nje ya Bunge ikijitapa kuwa zimeasisiwa kwao?

  CCM ya leo ambayo Kikwete bado haamini kama imekufa, ina muundo wa viongozi wasiyo na dira ya kuwaunganisha wanachama bali kutengeneza makundi ya uchaguzi ujao.

  Wakati wa CCM hai, viongozi wake waliikwepa sana rushwa, walijali uzalendo na maadili ya taifa, hawakupena madaraka kifamilia, uwazi ulitawala hasa kwenye chaguzi za ndani na michango ya kuendesha chama. Rais Kikwete anataka kutuambia kuwa CCM ya sasa iko hivyo?

  Leo CCM ambayo mwenyekiti wake haamini kama imekufa, mkewe anagombea ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) kupitia Lindi na mwanaye anagombea kupitia wilayani Bagamoyo. Hivi ni kweli familia nzima ina wito wa siasa na lazima wote waingie huko?

  Pengine Rais Kikwete haamini kifo cha CCM kwa vile anaiona bado iko madarakani. Lakini hakika hicho si kipimo kwani hata uchaguzi ujao wanaweza kushinda. Swali la msingi hapa ni wamefikaje uongozini, wana mipango endelevu, uwezo wa kusimamia sera na ilani yao?

  Tangu mwaka 2005 kwenye uchaguzi mkuu, aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania, akatangaza kutengeneza ajira zaidi ya milioni mbili. Leo maisha ya Watanzania ni magumu kuliko alivyoipokea nchi kutoka kwa mtangulizi wake, Benjamin Mkapa. Sasa hapa Kikwete anataka CCM ife mara ngapi?

  CCM iliyoaminiwa na kuahidi kupambana na rushwa, uhalifu, dawa za kulevya, umasikini, kuinua wakulima, kusomesha wanafunzi kwa kuboresha sekta ya elimu, afya, maji safi na salama mjini na vijijini halafu ikashindwa, Kikwete atasemaje haijafa?

  Mwenyekiti wa CCM anataka maono gani kujua anaongoza chama mfu ikiwa hata uwezo wa wabunge wake bungeni umekuwa na shaka, kutokana na kupitisha kila kitu kwa makofi na vigelegele halafu baadaye wanajuta?

  Kama kweli CCM ingekuwa hai kama anavyoamini Rais Kikwete, leo isingekuwa na makundi ya wabunge hadi ya mawaziri wanaosutana hadharani kwa tuhuma tofauti kwa sababu tu ya kupigania urais mwaka 2015.

  CCM ingekuwa hai isingesita kuwachukulia hatua mawaziri na wanachama wake wanaotuhumiwa kwa rushwa na ufisadi, isingehonga mahindi kwenye kampeni za uchagzu mdogo kama ilivyofanya Igunga, Katibu Mkuu wake na baadhi ya mawaziri wasingewatisha wapiga kura.

  Rais Kikwete anajua wazi kuwa kwa sasa ili uweze kuwavuta wananchi kuhudhuria mkutano wa CCM lazima ukodi wanamuziki au vikundi vya uchekeshaji kwaajili ya kutumbuiza, vinginevyo ni aibu tupu.

  CCM kama ingekuwa imara inatenda yale iliyoahidi bila shaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, asingezomewa mkoani Mwanza, badala yake angesomewa risala za pongezi na kupigiwa makofi. Tafakari!
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Wakati Mwigulu Mchemba yupo CCM haiwezi kufa
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  It is called myopic arrogance.
   
 5. S

  SUPERXAVERY Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hizo ni ndoto za mchana kweupe, endelea kuota kichaa wangu.
   
 6. S

  SUPERXAVERY Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM ni chama kisicho na ubaguzi, wewe unataka watu wenye sifa gani wagombee uongozi?
  Wachaga?
  Wambulu?
  Wachungaji?
  Au
  Wameru?

  Sisi tunaamini kila mtanzania anayo haki ya kuchagua kiongozi na kuchaguliwa kuwa kiongozi na kuongoza wengine.

  Nasikia kwenu CDM, mtu asiyetimiza sifa hizo muhimu haaminiki, ni mamluki.
   
 7. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Binafsi nilichomwelewa kikwete kwenye ile kauli yake ni kuwa alikuwa anajitutumua tu maana anaijua hali halisi ya siasa za Tanzania kwa sasa. Kifo cha ccm kipo palepale tu, ila wao hawawezi kukubali hadharani, tunachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuendelea kuwaelimisha wananchi waelimike ili 2015 wajitokeze kwa wingi kupigilia msumali kwenye jeneza la hiki chama kilichogeuka na kuwa cha kidhalimu waziwazi.
   
 8. ng'wanankamba

  ng'wanankamba JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Anajua sana kuwa CCM imeshakufa ila anajifanya hajui. Inaitwa kuishi kwa matumaini.
   
 9. m

  majebere JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  CCM itaanguka baada ya kupatikana mpinzani wa kweli, lakini kwa sasa hakuna mpinzani na ndio maana JK anaamini kuwa CCM itaendelea kutawala.Makundi yataendelea kuwepo pale anatafutwa mgombea mpya wa urais, kama mnakumbuka hata kabla ya Mkapa kupitishwa kulikuwa na mvurugano,walikuwepo wengi walio pinga Mkapa kuwa mgombea lakini alipita kwa nguvu ya Nyerere.
   
 10. m

  majebere JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Haya makundi tunayo yaona sasa yatakuwepo mpaka pale mgombea atakapo patikana, Jina likitoka tu basi wote wataelekeza nguvu zao kumsupport huyo. Viongozi wote wa CCM wanajua wazi kuwa kifo cha CCM ndio kifo chao wao na ushindi wa CCM ndio usalama wao kwahiyo baada ya mgombea kupatikana wao watapigania chama kishinde na sio mgombea.
   
 11. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  jk anaelewa nini kilichopo kwa kifupi anajifariji kuwa ccm itapona ndani ya wimbi la udini na ufisadi kumbe ndio kwanza wananchi wanazidi kuichoka na kupandisha hasira
   
 12. d

  dotto JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sisi tumetabiri kufa kwa ccm yeye anatabiria watu wafe kabla ya ccm . basi aanze yeye ili sisi tuishuhudie ccm ikifa na rais wa ukweli akiapishwa.
   
 13. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,890
  Likes Received: 1,647
  Trophy Points: 280
  umetumwa, tunakujuwa. Polee!
   
 14. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 2,890
  Likes Received: 1,647
  Trophy Points: 280
  amejitabiria.
   
 15. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CCM hata kama iki-survive kifo, itakuwa severely paralysed. Whether huu nao ni utabiri au la ni suala la muda tu.
   
 16. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  CCM itanusurika 2015 kwa mtizamo wangu ingwa inawezakuwa kwa gharama kubwa hata ya kumwaga damu. Kinachofanyika sasa ni kugawanya watu katika makuc^ndi na dini tofauti na hili CCM ilifanikiwa kwa CUF na inaelekea kufanikiwa katika baadhiya sehemu fulani za nchi hii hasa mikoa ya Pwani na palipokuwa na waisalmu wengi. CCM haikemei ukabila wala udini as long unaishambulia CDM na kwa namna fulani 2015 nchi itakuwa imegawanyika na CCM itakuwa na faida. Hofu yangu ni kuwa baada ya 2015 inawezekana kabisa nchi ikawa haitawaliki tena kwani udini na ukabila ulipoandikizwa na CCM utakuwa unaanza kujitafuna na tusishangae watu wakitiana mapanga. Mtizamo wangu wa pili na uasi ndani ya CDM.Tayari kuna viongozi tegemeonadani ya CDM ambao wametangaza kutogombea cheo chochote katika chama hicho ingawa umri na sifa vina waruhusu,wanataka kuelekea wapi,wana nia gani? Tatu ni nguvu ya makampuni ya nje na mataifa mengine yenye maslahihapa nchini,wana hofu na kundi la vijana walio nyuma ya CDM.CDM ikikamata madaraka itaweza kuwadhibiti kina Malema wa Tanzania? Tujadiliane.
   
 17. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,232
  Likes Received: 817
  Trophy Points: 280
  Statement aliyoitoa JK is very rude........ Hakutakiwa kuongea vile,amekuwa ni mtu wa mipasho mipasho kama mhuni wa mitaani tuu. Thats very low of him.
   
 18. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  CCM and Kikwete deserve each other! Thanks
   
 19. M

  Mindi JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Naingalia hiyo kauli ya JK kwa tahadhari kubwa. Ni mtu ambaye hajaonesha kushtushwa na mwelekeo mbaya katika nchi yetu: ukatili kwa Dr. Ulimboka, Mauaji ya Mwangosi. kabla ya hapo kulikuwa na mauaji ya Arusha na kwingineko. hivi mtu wa namna hii anapotamka kwamba WAPINZANI WAKE WATAKUFA KABLA YA CHAMA CHAKE, haujafika wakati wa kumtafakari kwa makini zaidi mtu huyu? amekwisha onja damu na anaonekana yuko tayari kuendelea kunywa damu, ali mradi kuendeleza utawala wa chama chake, kwa gharama zozote. Enter JK the VAMPIRE
   
Loading...