Hata Waingereza walibadilisha sanamu ya Bismini, Rais Magufuli itoe hii kitu

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Kwa wasiofahamu ile sanamu ya bismini mwanzoni kabisa ilikuwa sanamu ya Askari ya Kijerumani aliyejulikana kama Hermann von Wissmann, yaani ilijengwa na Wakoloni Wajerumani kwa ajili ya kumuenzi Askari wao aliyewezesha ukoloni wao, baada ya Ujerumani kushindwa vita Waingereza wakamuondoa wakaweka ya kwao kwa ajili ya kumbukumbu ya askari wa Kihindi na Kikenya waliokufa kwa ajili ya kutetea ufalme wa Uingereza sasa ni kwa nini na sisi tusiiindoe na kuweka ya kwetu inayotutambulisha??

Kama Waingereza waliiondoa na kuweka ya kwao, Je ni kwa nini na sisi tusiiondoe nakujenga yetu?!

Tafadhali Raisi Magufuli wewe ndiye mtu pekee unayeza kuleta Mapinduzi ya KWELI na ya kifikra hapa kwetu ambayo hata Mlm.Nyerere ingawaje alijaribu lkn hakuwa na uthubutu wa kutosha na kushindwa hata AK wanaondoa masanamu yote ya Kikoloni huko kwao, hivyo tafadhali Raisi Magufuli tuondolee hii takataka!

Hii ndiyo Historia ya Sanamu ya Bismini!

Mwanzoni alikuwa ni Hermann von Wissmann

wissdar2.jpeg

denkmaldar.jpg

Ndugu zetu kwenye vita ambayo haiwakuwahusu!

askari-porters.jpg

Waingereza walipoingia Dar es salaam baada ya Ujerumani kushindwa vita jambo la kwanza waliipiga bomu sanamu ya Askari wa Kijerumani

wiss1945a1.jpeg

Waingereza wakaweka sananu ya kwao kwa ajili yao, yaani kumbukumbu kwa walikokufa kwa ajili ya kutetea Ufalme, na hatukuwa sisi bali ni Wahindi na Wakenya!

askari-monument-dar-archive-LQ.jpg

Waafrika Kusini wakiondoa masanamu yaliyowekwa na Wazungu kwa ajili ya Wazungu, hawa wenzetu wameshaamka!
9D3FFB66-1F80-4F39-924B-56DC71FDDD85_mw1024_s_n.jpg

00b85daf-5871-4d5b-b8ba-1fb48a946d52-2060x1236.jpeg

0d3a2389e.jpg

6Xey1HbJJ-HSK1-3031543-The_defaced_statue_of_British_colonialist_Cecil_Rhodes_is_tied_b-a-61_1428585430478.jpg
 
sijakuelewa, kwa hiyo unamuunga mkono huyu?

Kwangu mimi ni bora hata awekwe huyo Diamond klk hao waliopo sasa hivi angalau Diamond ni wa kwetu, ingawaje ukiniuliza nichaguwe wa kuwekwa hapo sitoweza kumtaja Diamond lkn ukiniambia nichague kati ya Diamond na huyo Askari wa Kikenya aliyewekwa kwa ajili ya kumbukumbu ya Askari wa Kihindi nitachagua sanamu ya Daimond!
 
Mkuu mara nyingi hua natofautiana sana na Mara zako, lakini kwa hilo LA sanamu, kwanza naomba nikushukuru kwa kuleta historia mujarab ya hii sanamu ya posta, kama maelezo yako ni sahihi na huyo askari ni wa kikenya na wahindi, hakuna namna inabidi itolewe kwanza hata kama bado tunafikiria tutaiweka ya nani lakini kuiondoa tu itakua jambo LA busara.
 
Si kila historia ni nzuri kwetu hii inafaa kubaki ili kuwakymbusha watu madgila tuliyopitia.Zanzibar pale kanusani kuna sanamu za watumwa wa kiafrika ambao zilitengenezwa kwa kutumia picha halisi za watumwa hao waliokombolewa.si wazanzibar wala watanganyika bali wanatokea congo(majority ya watumwa wa bagamoyo na zbar ndio asili yao).
Mpaka leo zile sanamu zipo kwa faida ya kihistoria tu si kujivunia
 
Nafikiri basi wala hauelewi historia yetu vizuri, unawezaje kusema kwamba Watumwa waliouzwa Zanzibar na Bagamoyo siyo wa kwetu yaani hawatuhusu??? Ulishawahi kusikia kusikia kuhusu Bantu Somali??? Hiyo Karavani ilikuwa inaanzia Kongo (leo) lkn haimaanishi kwamba ilikuwa haisomibi watu njiani na ndio maana inaitwa karavani ilichukuwa Kigoma, Tabora, Dodoma, morogoro kwa kifupi njia nzima hivyo waliouzwa Bagamoyo na Zanzibar ni watu wetu kwa 100%, na hivyo kumbukumbu inatuhusu lkn sanamu ya Askari haitusu hata chembe kwani ni kumbukumbu ya askari wa Kihindi na Wakenya waliopigana kwa niaba ya Ufalme wa Uingereza hivyo ilipaswa ikajengwe Kenya au India/Pakistani na siyo kwetu!
 
Kwangu mimi ni bora hata awekwe huyo Diamond klk hao waliopo sasa hivi angalau Diamond ni wa kwetu, ingawaje ukiniuliza nichaguwe wa kuwekwa hapo sitoweza kumtaja Diamond lkn ukiniambia nichague kati ya Diamond na huyo Askari wa Kikenya aliyewekwa kwa ajili ya kumbukumbu ya Askari wa Kihindi nitachagua sanamu ya Daimond!

Kulikko huyo mdharirishaji wa wanawake na mwanga asiye haya kiasi cha kujitangaza hadharani kwamba yeye anafuga mafuvu ya binadamu ofisini kwake, ni afadhali mara mia hiyo sanamu iliyopo kwa sababu haina madhara zaidi ya kumbukumbu ya historia yetu, wapi tumetoka!.

Huy Diamond ana kipi kikubwa hadi ajengewe mnara? Ninadhani ni vyema hawa wadau wake wa siri, mkamjengea na huku kashika mafuvu yake anayofuga.

Na kwanini hapo tu ndipo mnapataka pabadilishwe? Hakkuna maeneo mengine ya kuweka hicho mnachokitaka?

Kwa nini monument you mtu tu? Mbona msiwaze kuweke picha za tembo wetu ambao muda mfupi ujao watakuwa wamekwisha kwa maana ccm watakuwa wamewamaliza??

Mbona musibuni minara ya kuonyesha utajiri wetu kama misitu ya asili na mito yetu ambayo inatoweka kwa kasi kwa sababu ya failures za serikali ya ccm?

Mnaonaje mkiweka minara yenye wingi wa aina ya madini yetu kama Tanzanite, Almasi na ghasia nyingi ambayo kwa sasa inabakia kuwa historia tu, ila tunabadi na mashimo katika jangwa tasa?

Tunahitaji kumbumbukumu hizi ziwe wazi kwenye minara kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo ambavyo vinahujumiwa na serikali ya ccm pamoja na wachina, ili visifaidike kama sisi na zaidi visishuhudie neema ya asili ambayo Mungu aliiumbia Tanzania.

CCM ni mauti ya Tanzania
 
Sijasema kwamba awekwe Diamond ila nimesema kama ukiniuliza nichague kati ya diamond na hao walioko sasa nitachagua Diamond kwa maana ni wa kwetu na ana mchango mkubwa TZ klk hawo Askri wa Kenya na India!
 
Mchango gani kafanya? Huyo mwanga na mdharirishaji wa wanawake anafundisha nini katika historia ya kwetu, Africa ama hata dunia? kuna nini cha kujifunza kwake kuliko hiyo sanamu iliyopo hapo? Wa kwenu anakusaidia nini katika ujinga endelevu wa ccm, umaskini unaoshamieishwa na ccm ma magonjwa mengi yalinayoua Watanzania bila tiba kwa sababu y akushindwa kwa serikali ya ccm kuwatumikia Wananchi? Tafadhali bwana!.

Huwezi kunishawishi kwa upuuzi wa huyu jamaa. Afadhali uweke breed mpya ya kuku wakubwa!.

TENA HILO SANAMU LISIONDOLEWE SANA SANA KUWEKWE PLATE KUBWA KULIZUNGUKA YENYE MAELEZO KWA UFUPI JUU YA VITA MWANZO NA MWISHO KUWA ANGLAIZO KWA KILA KIZAZI JUU YA KUTUNZA AMANI.

Siyo hii mihumi na michawi eti ndiyo mnajadili hapa!.
 
Mchango gani kafanya? Huyo mwanga na mdharirishaji wa wanawake anafundisha nini katika historia ya kwetu, Africa ama hata dunia? kuna nini cha kujifunza kwake kuliko hiyo sanamu iliyopo hapo? Wa kwenu anakusaidia nini katika ujinga endelevu wa ccm, umaskini unaoshamieishwa na ccm ma magonjwa mengi yalinayoua Watanzania bila tiba kwa sababu y akushindwa kwa serikali ya ccm kuwatumikia Wananchi? Tafadhali bwana!.

Huwezi kunishawishi kwa upuuzi wa huyu jamaa. Afadhali uweke breed mpya ya kuku wakubwa!.

Labda kama unataka kulazimisha kutokunielewa kwa sababu unazozijua wewe, hakuna mahali nilipojaribu kukushawishi chochote kile, na wala hakuna niliposema kwamba Diamond awekwe, mada yangu nzima imejikita kwenye historia ya sanamu na wala siyo Diamond hivyo kama una ishu na Diamond ni bora utafute uzi unaomuhusu na ziko nyingi sana hapa JF wee peruzi tu utaziona!
 
SAWA SAWA!
hivo hivo masanamu hadi sukari isaulike, taratiiiiiiiiibu nanza kuelewa issue za masanamu hivi, lakini hatuna watu wa kuwaenzi mpaka tumweke huyo diamond? mbona huyu mtoto anatupeleka pabaya, kwani ametufanyeje hadi tunamtukuza zaidi ya nyerere na mwinyi?(wasio na madoa mengi) jamani eeeeh!
 
Diamond ametokea wapi hapa?? Unaweza kuniambia?!
 
Labda kama unataka kulazimisha kutokunielewa kwa sababu unazozijua wewe, hakuna mahali nilipojaribu kukushawishi chochote kile, na wala hakuna niliposema kwamba Diamond awekwe, mada yangu nzima imejikita kwenye historia ya sanamu na wala siyo Diamond hivyo kama una ishu na Diamond ni bora utafute uzi unaomuhusu na ziko nyingi sana hapa JF wee peruzi tu utaziona!

Wewe mbona mzito hivyo kuelewa? Kama anakashifa nyingi hapa JF wewe unaujasirini gani kama siyo ujuha kutokutaka kuelewa tunavyosema? Kweli afadhali uwe maskini kuliko juha!. Tafadhali bwana. Jitambue!.
 
Back
Top Bottom