Hata uingereza wanatumia utaratibu huu ndugu Spika, (Sauti za Bungeni) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata uingereza wanatumia utaratibu huu ndugu Spika, (Sauti za Bungeni)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mess, Apr 22, 2010.

 1. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wana JF mimi nilikuwa nataka tu discuss kwa nini viongozi wetu hasa waliopo madarakani Tanzania huwa wanakataa wasikae na wale contestants wao kutoka vyama vingine wakati wa kampeni ili kila mtu auze sela? nimefurahia tarehe 15april akina gorden brown, david cameron na clegg walipokutana na kuanza kuulizwa maswali kila mtu anajibu na wenyewe pia kujiuliza maswali na kujibishana, ambao tena leo unaendelea huko kwa mara ya pili. Je Tanzania kwa nini isifanyike kitu kama hicho? kwanza inawezekana?
   
 2. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  hiyo kitu ilifanyika 1995 tu,baada ya hapo kila mtu lwake.
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,115
  Trophy Points: 280
  unataka kujua jinsi walivyo shalow??????????????
  waache bana sisi wadanganyika kwa hiyo kudanganywa kwetui freshi tu.......................
  ndio maana jk akija tena na maisha bora kwa kila mtz tutamchagua tu kwa kuwa sisi ni wadanganyika...............HII NI AHADI AMBAYO MUNGU PEKEEE ANAWEZA KUAHIDI LAKINI PAMOJA NA KUJUA HIVYO WATU WANAZIBA MASIKIO...............................
  bhandugu!!!!!!!!
   
 4. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  CCM walikubali 1995 kwasababu walijua Ben ni kichwa ila wanaogopa sasa hivi maana Vasco da gama atakuwa kichekesho kwenye mdaalo.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sasa hivi watu wa sisiem wanakataa..wanajua maswali yatakuwa mabaya, na watadhalilika!...hutasikia tena hiyo kitu, labda waulizaji waitwe ikulu, wachezwe, ndo waje kwenye ukumbi kuuliza sasa.period!
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nia ya mdahalo (debate) ni kwa ajili ya wananchi kusikia sera za chama na kumjua zaidi mgombea. Je tuna system au format itakayo fikia watu wengi? Ukiangalia t.v. nyingi ziko mjini(siyo kusema hakuna t.v. vijijini) au labda na radio. Tatizo naona huo mdahalo hauta fikia watu wengi na utamu wa mdahalo ni kuuona au kuusikia live siyo kuandikwa kweye magazeti. Tuki weza kupata format itakayo fikia asilimia kubwa ya wananchi then tuna weza kufikiria hilo swala.
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka ilipangwa kufanyika 2005, lakini JK 'alimgwaya' Mbowe na kipindi kuahirishwa!
   
 8. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Format nzuri na system huwa inakuja baada ya kujaribu na kuona matatizo then mnaanzia hapo kuboresha. Mimi napenda sana hiyo itokee kwa presidential candidates sio kutumia pesa tu. Tuone nani ana mawazo mazuri na nani yupo tu kwa sababu chama chake kina uwakilishi mkubwa bungeni. Kwanza ukiuangalia mdahalo hata ule wa Barack na Mcain utaona kuwa kila unachokiahidi unataonesha ni kwa jinsi gani utakifanya hicho kitu, io kukurupuka tu na kusema maisha bora kwa kila mtanzania, je utayafikiaje hayo maisha bora na indicator yako kuwa sasa maisha bora ni ipi? na inabidi uitaje wakati unafanya kampeni na sio vitu vinaishiahewani. Hatuwezi kumbana kikwete kwa sababu hakusema kiashiria cha maisha bora nini kipi, anaweza kusema kiashiria chake ni university of dodoma hatuwezi kukataa kwa sababu hakusema wakati wa kampeni. Nawaomba wana JF tu push hiki kitu kitokeee najua tunaweza.
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu. Nakubaliana na yote uliyo sema.
   
Loading...