Hata tuyazime, maswali yale yale kuhusu Muungano yanaturejea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata tuyazime, maswali yale yale kuhusu Muungano yanaturejea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHIBUU, May 25, 2012.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Ye yote anayetaka kujua jinsi masuala ya Muungano yalivyotusumbua katika historia yetu ya takriban nusu karne atakumbuka mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na tume na kamati mbalimbali zilizoundwa katika jitihada za kujaribu kurekebisha baadhi ya masuala yaliyoonekana kukera makundi ndani ya nchi, na jinsi ambavyo jitihada hizo zote na kamati na tume hizo hazikufanikiwa kuondoa malalamiko kuhusu Muungano.
  Sasa itakuwa ni jambo la ajabu iwapo, wakati tunasema tunataka kuandika katiba mpya, tutajinyima wasaa wa kuujadili Muungano kwa kuwauliza wananchi wa pande mbili (Tanganyika na Zanzibar) ni nini wanachotaka, iwapo wanataka Muungano au hawautaki.


  Swali hilo la msingi likiiisha kupatikana, na jibu likawa kwamba wanautaka Muungano, ndipo sasa itawezekana kuangalia kwa undani ni mambo gani ndani ya mfumo na taratibu za Muungano yafanyiwe marekebisho ili kuyaweka sawa na kukidhi matarajio ya pande mbili zilizoungana.


  Binafsi nakataa dhana ya kuwaambia watu kwamba kuujadili Muungano ni sharti tujadili namna ya kuuboresha. Mtu huboresha jambo analotaka kuendelea nalo, na kama hataki kundelea nalo ni upuuzi kuanza kuliboresha. Haina maana hata kidogo. Na si kweli kwamba hatujasikia sauti za watu wanosema kwamba hawautaki Muungano, na wala pia si kweli kwamba hawana haki ya kuwa na mawazo kama hayo.


  Njia pekee kwa wale wanaopenda Muungano uendelee kuwapo (pamoja na marekebisho yatakayokubaliwa) ni kuwaacha wana-Muungano wenyewe waseme kwamba wanataka kuuendeleza kwa kuuboresha. Iwapo watasema kwamba hawautaki, na tujue kwamba hiyo ndiyo kauli yao, huo ndio utashi wao. Kujidai kwamba tutauendeleza Muungano bila ridhaa ya Watanganyika na Wazanzibari ni ndoto za Alinacha.
   
 2. M

  Masabaja Senior Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naaunga mkono hoja aslilimia milioni moja pasipo na shaka lolote bila watanganyika na wazanzibari kukubali namna ya kuendesha muungano na ikawa watu wachache wanataka kuamua kila kitu ni hatari. Sijui ni kwa nini hawa wachache hawataki jambo hili wenye nalo (yaani watanganyika na wazanzibari) walijadiri isipokuwa mawazo yao tu ndiyo sahihi (yaani Kikwete na wachache tu wantuambia katika kuundwa kwa katiba mpya hakuna kujadili muungano) nafanisha mawazo haya na mlevi ambaye anakuja baa mara akilewa anamdharau kila mtu. Wenye mamlaka acheni dharau kwa mnaowaongoza muungano na muundo wake lazima uhamuliwe na wenye muungano wenyewe na si viongozi.
   
Loading...