Hata Tume Huru ya Uchaguzi ikiwepo Tanzania, CCM hawawezi kuachia ngazi!

Kwa faida ya nani? Sisi Tume iliyopo inazingatia matakwa na maslahi ya Wananchi! Hatuoni kwa nini tupoteze muda kuunda Tume huru eti Wapinzani waende Ikulu! Wakafanye nini la maana? Kuonja tu kukaa Ikulu! Rubbish!

Kwa faida ya nani. Sisi wananchi tulio wengi tumeikubali CCM! Hao wababaishaji wa Upinzani waende zao huko!!
Uongozi wa nchi unapokuwa wa hila mafanikio yatabaki kwenye makaratasi na si realty. Ubinafsi unaoisumbua CCM kujiona wao wanastahili kutuamulia na si wengine haiwezi kuwafanya wafanikiwe

Kama wanajiamini tume iwe ya wote (huru)
 
Siyo ajaribu kuianzisha sisi wenyewe Watanzania tuindai ni haki yetu,tuondokane na fingisu tupate viongozi tunaowataka kiukweli.Hapa ndipo atakuwa na ujasili wa kusema "msema kweli ni mpenzi wa MUNGU".
kweli inapaswa tuidai
 
Ni kweli Tanzania ata 2015 tumechaguliwa viongozi wengi na tume, Ni wakati sasa tume iwe huru au iundwe na vyama vyote, ya sasa hivi ni maigizo tu ata wenyewe ccm wanajua bila tume madarakani hawabaki, tena uchaguzi ukiitishwa sasa hivi Magufuli atapata below 10% kama tume itakua huru. Wengi humu ni wanafiki hawasemi ukweli kwa uoga wa mafarisayo.
 
Ndio kazi ya chadema siku hizi kuombea kila aina ya maovu yatokee Tanzania.

Tume inakuwa nzuri na huru inapowatangaza washindi Mbowe, Lisu, Lema, Mdee etc

Lakini tume hiyo hiyo inakuwa siyo huru inapowatangaza Magufuli, Zungu, majaliwa, Nchemba etc
Acha maneno wacha iwe huru iendelee kuwatangaza akina majaliwa lakini kwa ushindi halali. Mimi binafsi sina tatizo na mgombea yoyote anayeshinda kihalali, au wapinzani kushinda hadi wakeshe sehem ya kuhesabia kura otherwise imekula kwako, ccm kwa nini wanaogopa tume huru, kwani ikiwepo ni dhambi?
 
Muundo wa Tume,

Base au Wajumbe wa Tume,

A) Wajumbe 9 Kutoka Chama Tawala
B) Wajumbe 9 kutoka Kambi ya Upinzani

Kamati ya Tume ya Sheria na Katiba

1) Wajumbe 5 Wanasheria Kutoka Chama Tawala
2) Wajumbe 5 Wanasheria Kutoka kambi ya Upinzani

Kamati ya Utaalamu na IT

3) Wajumbe 5 Kutoka Chama Tawala
4)Wajumbe 5 Kutoka Kambi ya Upinzani

Kamati ya Ushauri na Uhusiano

5) Wajumbe 3 dini/Taaluma etc Kutoka Chama Tawala
6) Wajumbe 3 dini/Taaluma etc Kutoka kambi ya Upinzani

Uongozi.

Mwenyekiti atokane na Kudi la wale Wajumbe Tisa Tisa. Automatically Mwenyekiti akitokea Chama Tawala Makamu awe Upinzani and Vice Versa. Maamuzi yote yahusianayo na Process nzima ya Uchaguzi na Kutangaza matokeo ni batili bila Kura za wajumbe 3/4 ya wale tisatisa.

Katibu atokane na Kundi la Wataalamu wa kundi la wale wajumbe watano watano. Katibu akitoka Upinzani automatically Naibu anatoka chama tawala n Vice Versa. Katibu anawajibika kwa Mwenyekiti na Kundi lile la Tisa Tisa.

Kundi la Mwisho Liwe Ni Kundi La watendaji na Waajiriwa wa Tume ambao Itikadi ya Kisiasa haitazingatiwa na Wataapishwa kuwa ni Kosa la jinai Ikiwa watajihusisha na Kuyumbisha au kuvuruga process ya Uchaguzi wowote kwa maslahi ya chama chao au chama fulani kwa maslahi ya binafsi. Idadi yao itakuwa kila Mkoa Kulingana na Mahitaji.

Iwe ni Marufuku Kwa Mteuliwa Yeyote wa Rais au Watendaji wake eg DED kujihusisha na Chaguzi zozote.

Tume Ikiwa mfano huu, Hata CCM wakishinda miaka 10,000 Mfululizo Nikifanikiwa kuwepo nitawapigia Mizinga 21. Ila bila kuwa na Tume huru CCM wakasema wameshinda Kihalali, wanatakiwa kupigwa Mizinga 21! Hasa huyu, huyo atakayesema kashinda!
Katika comments zote ambazo nimepata kusoma humu jf wewe umeandika kitu cha thamani sana bahati mbaya ni mwiba kwa watawala, hawawezi ruhusu ingawa ndio ingetupatia viongozi walioshinda kihalali sio hawa wa kuwekwa kwa ushindi fake, ukiona mtu humu anasifia ushindi wa ccm ujue ni mchumia tumbo ila ukweli huu anaujua.
 
Dah... Mzungu alituweza sana...Yaani bado miaka zaidi ya 3....tunawekeza kwenye kazi za midomo na perete perete... na bado tunalia njaa.... Hivi vyama vya siasa haviwezi kugeuka taasisi za uzalishaji baada ya Uchaguzi kupita? Kama kweli Nia yao kumsaidia wananchi... Kwanini wasifanye hivyo kwa kuelekeza ruzuku yote kwenye uwekezaji... Kuanzisha miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji na ufugaji...hapa ajira nyingi zingezaliwa. . Bila ya aibu wanajinadi hadharani kuwa lengo la Chama chochote cha siasa ni kuchukua dola (Makusanyo ya kodi) ....kama kweli wana Nia njema na wananchi kwanini wasituonyeshe angalau kwa hayo makusanyo kidogo ya kodi wanayopata(ruzuku)? Kweli mzungu muacheni aitwe mzungu.... Hivi Hatuwezi kuwa na mfumo mwingine wa kujiongoza tofauti na huu unaotutia ujinga?
 
Na muundo wa sasa ukoje???

Muundo wa sasa unawahusisha wakuu wa wilaya,mikoa na halmashauri za miji na Manispaa kama wasimamuzi wakuu na makamishna wa uchaguzi,wateule hawa wote ni wanachama wa ccm,kuendesha uchaguzi unaosimamiwa na makada wako kisha makada wako wakakutangaza mshindi na wewe ukajigamba kuwa umeshinda kwa kishindo waweza kuwa ni uthibitisho kuwa PhD ya maganda ya korosho haina mchango wowote katika Taifa linalozalisha korosho kwa wingi.
 
Dah... Mzungu alituweza sana...Yaani bado miaka zaidi ya 3....tunawekeza kwenye kazi za midomo na perete perete... na bado tunalia njaa.... Hivi vyama vya siasa haviwezi kugeuka taasisi za uzalishaji baada ya Uchaguzi kupita? Kama kweli Nia yao kumsaidia wananchi... Kwanini wasifanye hivyo kwa kuelekeza ruzuku yote kwenye uwekezaji... Kuanzisha miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji na ufugaji...hapa ajira nyingi zingezaliwa. . Bila ya aibu wanajinadi hadharani kuwa lengo la Chama chochote cha siasa ni kuchukua dola (Makusanyo ya kodi) ....kama kweli wana Nia njema na wananchi kwanini wasituonyeshe angalau kwa hayo makusanyo kidogo ya kodi wanayopata(ruzuku)? Kweli mzungu muacheni aitwe mzungu.... Hivi Hatuwezi kuwa na mfumo mwingine wa kujiongoza tofauti na huu unaotutia ujinga?

Nafikiri ungetumia bandiko lako kuihimiza serikali iwasilishe Rambirambi za Wanakagera ungekuwa umefanya jambo la maana sana,kuwaambia wapinzani watumie Ruzuku kuiendeleza jamii ni justification ya kitoto sana.Wanaokusanya kodi zetu kila mwezi wao wamefanya nini?Wao Ruzuku yao imefanya kitu gani?Au ni Ruzuku za wapinzani tu ambazo ni 1/3 ya Ruzuku inayochukuliwa na CCM ndiyo inayopaswa kutumika kuiendeleza jamii tu?
 
Dah.. .Chief hujanielewa.. Tuliza akili ..bila hasira.. ..kanisome upya.. mdogo mdogo
 
Mkuu Mokili Fumulauhi,
Nasoma post zako lakini mara nyingi nachangia kwa uangalifu mkubwa.Si mtabiri wala msoma nyota lakini inaelekea huwatakii mema binadamu wenzako.Katika hali hii ya leo una ujasiri gani wa kusema haya usemayo?
Twende kwenye mada-Magufuli atashinda kwa asilimia kubwa kwa sababu moja kubwa ambayo nayo ni kuwa watanzania hasa wa bara si watu wa kuweka mambo sana na ni watu wa kuridhika haraka.Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 utakuonyesha hali halisi na mambo yakayotokea 2019 na 2020 kabla ya uchaguzi hata kama ni kwa muda mfupi yatawafanya Watanzania wasahau mengine yote.
Watanzania wakilalamika waangalie kwa makini.
Yaani Kuomba Tume huru ni kuwatakia Binadamu wenzangu mabaya? Kuna ubaya katika Ukweli na Uwazi, Je Uhuru ni neno baya kweli. Unakumbuka enzi za Glasnost na Perestroika?
 
naunga mkono hoja yako

lakini tatizo kubwa la watanzania ni ujinga..hawaeezi ku reason..wapo wengi tu wanaoichagua CCM

Naunga mkono hoja yako na tumeshauri Mara nyingi sana hii iwe ajenda namba moja lakini watu wameweka pamba masikioni

CCM ikishinda katika mazingira ya tume huru it's well and fine
Mkuu inawezekana level ya wa Tz walio wengi bado wako chini katika kuelewa baadhi ya mambo, huwezi kuwalinganisha na baadhi ya nchi zilizopiga hatua LAKINI pia si wajinga kiasi hicho. Ati tu kwa vile CCM haifanyi vyema then utegemee wafanye uamuzi wa kipumbavu zaidi kwa kumchagua mwingine yeyote ili awaongoze. Itafika siku tutapata viongozi mbadala pale itakapoonekana inafaa. Tumewahi kuwa nao na bado baadhi tumewachagua chini ya tume hii hii (Lissu, Mbowe, Waitara, Mr.2, Prof. J, Kamanda Lema, Mbatia, Mdee, Bulaya, E. Matiku etc hata Edo tulimpa 40% siyo haba). Mkuu TZ ni nchi kubwa na ina watu wenye matamanio tofauti na kwa hivyo acha kujipumbaza kwa kuwaona ni wajinga eti tu kwa sababu hawakuchagua Upinzani chini ya Edo.
 
Dah... Mzungu alituweza sana...Yaani bado miaka zaidi ya 3....tunawekeza kwenye kazi za midomo na perete perete... na bado tunalia njaa.... Hivi vyama vya siasa haviwezi kugeuka taasisi za uzalishaji baada ya Uchaguzi kupita? Kama kweli Nia yao kumsaidia wananchi... Kwanini wasifanye hivyo kwa kuelekeza ruzuku yote kwenye uwekezaji... Kuanzisha miradi mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji na ufugaji...hapa ajira nyingi zingezaliwa. . Bila ya aibu wanajinadi hadharani kuwa lengo la Chama chochote cha siasa ni kuchukua dola (Makusanyo ya kodi) ....kama kweli wana Nia njema na wananchi kwanini wasituonyeshe angalau kwa hayo makusanyo kidogo ya kodi wanayopata(ruzuku)? Kweli mzungu muacheni aitwe mzungu.... Hivi Hatuwezi kuwa na mfumo mwingine wa kujiongoza tofauti na huu unaotutia ujinga?
Hapo nakuunga Mkono vingefanya hivyo Visingeishia Kupora pesa za Wahanga wa Tetemeko. Hasa vinapokuwa ni Chama tawala ongoza kwa mfano. Na pia mwenyekiti wake asingelazimika kutumia nafasi yake ya Urais Kukwapua 2.7 billion hazina na kuwagawia. Hapo umenena!
 
Mkuu inawezekana level ya wa Tz walio wengi bado wako chini katika kuelewa baadhi ya mambo, huwezi kuwalinganisha na baadhi ya nchi zilizopiga hatua LAKINI pia si wajinga kiasi hicho. Ati tu kwa vile CCM haifanyi vyema then utegemee wafanye uamuzi wa kipumbavu zaidi kwa kumchagua mwingine yeyote ili awaongoze. Itafika siku tutapata viongozi mbadala pale itakapoonekana inafaa. Tumewahi kuwa nao na bado baadhi tumewachagua chini ya tume hii hii (Lissu, Mbowe, Waitara, Mr.2, Prof. J, Kamanda Lema, Mbatia, Mdee, Bulaya, E. Matiku etc hata Edo tulimpa 40% siyo haba). Mkuu TZ ni nchi kubwa na ina watu wenye matamanio tofauti na kwa hivyo acha kujipumbaza kwa kuwaona ni wajinga eti tu kwa sababu hawakuchagua Upinzani chini ya Edo.
Hizo ni Hadithi, Tunataka Tume Huru shida iko Wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom