Hata Spika wa Bunge awe nani, hawezi kutufaa kama taifa. Ufizi ukioza jino hata liwe zuri vipi litauma tu na huenda likang'olewa tena

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,095
4,059
Habarini za saa hizi ndugu, adui, rafiki na jamaa yangu wa humu JamiiForums.

Nataka kuzungumzia hili suala la watu wengi kufikiria (ponder] juu ya nani ajaye kama spika wa bunge. Kama wengi wetu wakitabiri kwa maoni na mitazamo yao Kabudi, Chenge au Lukuvu na hata Waitara sio mbaya.

Hawa wote wanaweza wakawa watendaji wazuri au wakawa wanataka kuiliinua bunge letu na likawa na nguvu.

Kipindi mkijikita katika kupendekeza majina ya nani anafaa,msisahau ule wembe alionyolewa nao Ndugai haujatupwa umehifadhiwa Dodoma hapo hapo. Yawezekana kabisa mihimili ikatofautiana kimtazamo au sera kwa maana kila mhimili unatazama kimtazamo wake.

Bunge linaaminika lipo jirani zaidi na maslahi ya walio wengi aka wanyonge na seeikali wapo jirani pia ila sio kwa ukaribu wa bunge.

SHINIKIZO KUBWA LA KUONDOLEWA SPIKA WA BUNGE LILITOKA CHAMANI NA KUPOKELEWA NA SERIKALI.

Hapa naomba tuelewane, isije nikanukuliwa vibaya na makomredi wenzangu au nikapata uungwaji mkubwa kutoka kundi fulani.

Nasisitiza mada hii ni kujaribu kuwafumbua watu macho kuwa hali bado sio nzuri ndani ya CCM na bunge na waache mara moja kuzungumzia ya Ndugai na spika mpya anaetarajiwa kupendekezwa.

1. BUNGE LOTE NI LA CHAMA KIMOJA
Kitendo cha bunge kuwa na aina ya wabunge wa aina au chama kimoja kwa 100% na kwa namna tamaduni za CCM zilivyo ni wazi kusema kuwa Makatibu na Wenyekiti wa CCM ndio bunge kwa sasa. Japo CCM ni chama changu ila Makatibu na Wenyeviti maazimio yao ndani ya kamati kuu ya CCM NEC na Halmashauri kuu ya CCM Taifa yanaathari moja kwa moja kwenye bunge letu. Angalia ku resign kwa Ndugai barua ilipitia wapi na nakala ilienda wapi na katibu wa bunge alikenua tu meno na kuthibitisha kupata taarifa kutoka kwa Katibu wa chama, how ridiculous is this?. Dhambi ina zaa dhambi nyingine.

JINA LA SPIKA WA BUNGE LINAPENDEKEZWA NA RAIS NA KISHA KUTHIBITISHWA NA BUNGE(SPIKA WA BUNGE ANACHAGULIWA NA RAIS]

Hapa ni moja ya uchafu wa katiba inayotumika kwa sasa, katiba hii ni kichekesho sana directly inatambua mihimili mitatu ila indirectly muhimili upo mmoja tu. Yaani sawa na kusema mti mmoja alafu useme ipo mitatu alafu unaorodhesha kuna mizizi,shina na matawi. Sawa hivyo vitatu vipo na vinategemeana ila tusisahau uiamara wa hivyo vyote ni mizizi. Mizizi ni Urais,shina ni mahakama na matawi ni bunge. Spika wa bunge na jaji nyuma ya kamera anawajibika kwa rais na ndio teuzi zake rais. Nachekaga watu kulalamika kuona rais anaingilia muhimili fulani na wakati anamwajobisha aliyemteua. Refer prof Musa Asad na Magufuri na leo Ndugai na Samia. Mihimili yote ni teuzi za rais.

NITAPAMBANA KUIPATA KATIBA MPYA YA WANANCHI NA SIO YA WANASIASA.

Kutokana na mbugi la kikatiba na kisheria nitasimama kidete kuhakikisha katiba iwe ya wananchi na sio kwa ajiri ya viongozi na wala sio kwa ajiri ya wanasiasa.

Tunahitaji katiba ambayo haina muingiliano hata ikitokea mpishano wa kisera basi kila mtu asimamie chake hadi pale watakapoyamaliza kwa kwa majadiliano,na sio kutunishiana misuri.

Sisi wananchi tupewe nafasi kwenye maamuzi hasa yenye maslahi kitaifa na kimataifa.

Katiba mpya kwanza kwa faida ya uma.
 
Back
Top Bottom