Hata sasa Mungu amenisaidia. Hakuna lililopo chini ya jua litakaloshindikana

elyamuia

Senior Member
Aug 21, 2020
113
225
Ndugu Habari.
Namshukuru Mungu amenisaidia sana katika wakati mgumu niliopitia wakurushiwa roho chafu za ndoto. Kipindi cha nyuma nilileta mada ya ndoto nilizokuwa naziota na za kunitesa nafsi Yangu.

- Nimeota napambana na paka mwitu Jeusi la kutisha kwa kupigana nalo kwa muda mrefu. Naomba tafsiri ya hii Ndoto

Sasa Basi Baada ya Maombi ya mazito kwa muda mrefu na kumkabidhi Mungu apambane na mtesi wangu,ambapo kwa siku nilikuwa nikiomba kama masaa mawili hivi.

Ndugu zanguni nikiri kuwa Juzi nimeoteshwa ndoto nikiwa ninamkimbiza Mbwa na fimbo akapanda juu ya bati na baada ya hapo gafla akatokea mtu ambae sikumfahamu nikamuomba apande juu ya bati ampige mbwa yule. Kwa kweli alipanda na akampiga yule mbwa na rungu na baadae rungu ikadondoka akaumana na yule mbwa,uzuri yule mtu akamuuma yule mbwa akakimbia.

Nimepewa tafsiri yake kuwa naelekea kuishinda vita. Hivyo nisipunguze maombi.Nitakuwa shuhuda wa Mungu milele ne milele Asante Bwana Yesu.
 

sala na kazi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,884
2,000
Sitaacha Ndugu,Namshukuru Mungu
Safi sana,Usiwe mvivu..sasa hivi piga double double.....
.. asubuhi,mchana na jioni

Na huyo mtesi mkabidhi kwa Mungu ampige moto wa Mungu + makombora.Lia na Mungu hadi koo likauke

Nahisi hilo jamaa kama lipo mitaa ya hapo litahama au lianzishe urafiki na wewe akuzingue tena.

Kemea hadi kieleweke.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom