Hata Rais akiwa kanisani hawezi kuchangamana na waumini wengine?

Ni kweli kua rais anapaswa kulindwa na kuhakikishiwa ulinzi masaa 24 7.

Naomba kuuliza, je rais anapokua kanidani haruhusiwi kuchagamana na waumini wengine?

Kwa mfano katika hii picha walinzi wa rais wamemzunguka na kumtenga rais na watu wengine. Je hii haiondoi dhana nzima ya kua ibadani? Hakuna namna nyingine ya kuharmonize ulinzi wa rais katika mazingira kama haya maana kwa hii inaondoa kabisa ile ari ya kusali.

Nimeuliza tu.View attachment 1018569
Hata bila ya rais kanisani hukai popote unapopataka wewe. Ubaguzi mtupu.
 
Labda anahofia wakurugenzi, maana siku hizi hata kanisani ni pyuu pyuu...

Hizo ngudu ni dalili za imani mdogo za watu..
Bora kuamua kuwa mpagani kuliko, mcha Mungu..
 
Mimi nimeswali Mara kadhaa Na Jakaya Msikiti wa Mtoro Kariakoo Na Ulinzi ulikuwepo Kama kawaida acheni kumsakama Ndugu Magufuli Hata kwa yake ambayo hana control nayo

Rais hajiamulii namna ya kulindwa wanaoamua Ni watu wenye weledi Na kazi hiyo
Nani kasema JK hakuwa na ulinzi?
 
Privacy

°°ᴶᵉᵃˡᵒᵘˢˢʸ ⁱˢ ᵖʳᵒᶜᵉˢˢ ʸᵒᵘ ᵍᵒ ᵗʰʳᵒᵘᵍʰ ᵇᵉᶠᵒʳᵉ ᵇᵉᶜᵒᵐⁱⁿᵍ ᵃ ʷⁱᵗᶜʰ°°
Mzee analindwa popote pale alipo. Haitakiwi kuacha upenyo wowote ule! Hahahaaaaa, Mzee baba huwezi amini vitu vinashuka na huku ulinzi umeimarishwa!!
 
Mi najua raisi sehemu zote analindwa ila naskia chooni tu ndio anakuwa mwenyewe

°°ᴶᵉᵃˡᵒᵘˢˢʸ ⁱˢ ᵖʳᵒᶜᵉˢˢ ʸᵒᵘ ᵍᵒ ᵗʰʳᵒᵘᵍʰ ᵇᵉᶠᵒʳᵉ ᵇᵉᶜᵒᵐⁱⁿᵍ ᵃ ʷⁱᵗᶜʰ°°
Wengine mpka toi lazima awepo mtu pembeni ya mlango kuskilizia majambo
 
Kama kanisani ni hatari hivyo kwanini huko Ikulu kusiwe na jengo maalum la kufanyia ibada za kiongozi mkubwa wa nchi? Huko kanisani wote tuko chini ya Mungu, inapotokea binadamu akawa zaidi ya Mungu hiyo ibada haina maana.
Umenena vema. Hii ibada inakuwa imebatilishwa.. Lengo la kuhudhuria ibada haliwezi kutimia.. cz attention na concentration yote inahamia kwa presida. Ni vema mkuu akawa na nyumba ya ibada kule pembezoni mwa bahari.
 
Ni kweli kua rais anapaswa kulindwa na kuhakikishiwa ulinzi masaa 24 7.

Naomba kuuliza, je rais anapokua kanidani haruhusiwi kuchagamana na waumini wengine?

Kwa mfano katika hii picha walinzi wa rais wamemzunguka na kumtenga rais na watu wengine. Je hii haiondoi dhana nzima ya kua ibadani? Hakuna namna nyingine ya kuharmonize ulinzi wa rais katika mazingira kama haya maana kwa hii inaondoa kabisa ile ari ya kusali.

Nimeuliza tu.View attachment 1018569

Kwa hiyo amezungukwa na sanamu? Badilisha hiyo miwani ya mbao.
 
Mbona huyu hazongwiiii sana
IMG_20190125_193650.jpeg
IMG_20190125_193713.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kua rais anapaswa kulindwa na kuhakikishiwa ulinzi masaa 24 7.

Naomba kuuliza, je rais anapokua kanidani haruhusiwi kuchagamana na waumini wengine?

Kwa mfano katika hii picha walinzi wa rais wamemzunguka na kumtenga rais na watu wengine. Je hii haiondoi dhana nzima ya kua ibadani? Hakuna namna nyingine ya kuharmonize ulinzi wa rais katika mazingira kama haya maana kwa hii inaondoa kabisa ile ari ya kusali.

Nimeuliza tu.View attachment 1018569
Achangamane nanyi ili mfanikishe Nia zenu Ovu sio!?
Kwani hao masista/watawa hapo mbele ya Mh. Rais nao ni watu wa Usalama sio?
Upunyunyu umewajaa mpaka mnakosa Hoja.
 
Ni kweli kua rais anapaswa kulindwa na kuhakikishiwa ulinzi masaa 24 7.

Naomba kuuliza, je rais anapokua kanidani haruhusiwi kuchagamana na waumini wengine?

Kwa mfano katika hii picha walinzi wa rais wamemzunguka na kumtenga rais na watu wengine. Je hii haiondoi dhana nzima ya kua ibadani? Hakuna namna nyingine ya kuharmonize ulinzi wa rais katika mazingira kama haya maana kwa hii inaondoa kabisa ile ari ya kusali.

Nimeuliza tu.View attachment 1018569
Mkuu rais wa nchi sio kama rais wa wasafi au rais wa chama cha wapenda taarabu. Huyo ni nembo ya Taifa, huwezi kumchanganya hovyo na watu, ikiwa mtu kaingia na bomu ili ammalize?.

Rajiv Gandhi aliuwawa na dada aliyevaa bomu kifuani mwake, alipomkaribia akajifanya kama anainama kama vile kumpa salamu ya heshima, bomu likalipuka kiunoni mwake.
 
Mi najua raisi sehemu zote analindwa ila naskia chooni tu ndio anakuwa mwenyewe

°°ᴶᵉᵃˡᵒᵘˢˢʸ ⁱˢ ᵖʳᵒᶜᵉˢˢ ʸᵒᵘ ᵍᵒ ᵗʰʳᵒᵘᵍʰ ᵇᵉᶠᵒʳᵉ ᵇᵉᶜᵒᵐⁱⁿᵍ ᵃ ʷⁱᵗᶜʰ°°
Hadi akichepuka mlinzi anabaki mlangoni kusikilizia vilio vya mgegedo chumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere alikuwa anasali kila siku pale St Peters lakini mbwembwe zilikuwa zinaachwa nje ya kanisa. Mwinyi msikitini alienda, Mkapa naye na hata JK alienda sio msikitini tuu bali hata mazishini alienda na mbwembwe hatukuziona.
Huyu wa kwetu sasa haya ndio anapenda, kwanza alipenda hata asindikizwe na ndege za kivita na vifaru ni basi tuu inakuwa ngumu. Ni mpenda sifa sana
Mkuu Chakaza, nyakati zimebadilika. Nyerere na Sokoine pale Saint Joseph walitengenewa mabenchi yao, benchi lao lilikuwa linakaliwa na watu watatu, mlinzi mmoja kulia, mwingine kushoto na katikati ndio wanakaa wao. Hawakujiachia kihivyo.
 
Hili jambo la Rais kwenda Kanisani na mbwembwe zote za dola, limetukwaza wengi.

Tunaosali St Peters, kila mmoja analalamika. Siku Rais akija kusali inakuwa ni kero kubwa.

Siku anayoenda kusali, hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia kabla ya walinzi kuingia na mbwa na kufanya ukaguzi kila mahali. Mbwa wanapelekwa mpaka madhabahuni kwenda kukagua.

Magari yote yanayoingia kwenye eneo la kanisa au hukaguliwa kwa vifaa maalum au yanazuiwa kuingia eneo la kanisa. Waumini wote kabla ya kuingia kanisani, hukaguliwa kwa metal detectors, mikoba yote ya akina mama inakaguliwa.

Wakati wa kutoa sadaka na kupokea ekaristi takatifu, walinzi wa Rais hujipanga mistari miwili, na waumini wote hulazimishwa kupita katikati ya hiyo mistari miwili ya walinzi wa Rais.

Kuna wakati Rais hukaa mstari wa mbele na mlinzi wake, nyuma yake hupangwa masisita. Wakati mwingine hukaa nyuma ya masista, na mistari inayofuata wanakaa walinzi wake.

Wakati ibada ikiendelea, baadhi ya walinzi wa Rais, husimama mbele na kuwaangalia waumini, huku wengi wakiwa wametapakaa maeneo mbalimbali.

Kwa ujumla, siku Rais akienda pale St Peters ni kama siku hiyo huwa hakuna ibada ila maonesho ya mbwembwe za walinzi wa Rais.

Tunashauri uongozi wa kanisa, Rais awe na ibada yake pekee yake na watu wake anaowaamini kuwa ni salama kwake. Maana kwa sasa ukienda halafu na Rais akawa anakuja siku hiyo kusali, unajilaumu kwa nini ulienda kwenye ibada hiyo.

Kama uongozi wa kanisa hauwezi kuzingatia maoni yetu haya, kuna siku watashangaa waumini wote wakitoka na kuwaacha na Rais na walinzi wake. Kwa ujumla siku Rais akienda Kanisani, hakuna ibada. Rais inaonekana haendi kwenye ibada bali kwenye maonesho. Kama kanisani ni hatari kiasi hicho, mapadre waweke utaratibu wa kwenda kumsalisha Rais Ikulu ambako, nina imani kuna usalama wa kutosha.

Na hawa viongozi wetu wa kanisa wanatukwaza kiasi cha kujiuliza kama kweli wapo na Roho ya Mungu. Itawezekana vipi, madhabahuni ambako sisi tunaamini ni eneo takatifu, leo wanapitishwa mbwa kila eneo, kama wanavyotaka?

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha Uzandiki Wewe! Hiyo St. Peters umeanza kusali juzi ulivyokuja mjini ndio imekuwa tabu. Watu wanasali hapo tokea enzi za Baba wa Taifa akiwa muumini wa hapo na taratibu zilikuwa ni hizo hizo na hakukuwa na malalamiko ya kipuuzi kama haya. Rais anakukwazaje anapoenda kanisani kufanya Ibada!? Kwani amekuja nyumbani Kwako!? Kuna misa Tatu pale...misa ya kwanza, ya pili na ya Jioni. Chagua moja kati ya hapo ambayo hakutakuwepo na Kero za Mh. Rais akiwepo Ibadani.
Kila la kheri ewe mkatoliki zandiki.
 
Aseee kumbe kunakuwa na seleka kubwa kiasi hicho? siku akiingia madarakani musilamu mwenye mbwembwe mbwa wataingia msikitini kukagua? haya mengine mbwembwe zinazidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha Uzandiki Wewe! Hiyo St. Peters umeanza kusali juzi ulivyokuja mjini ndio imekuwa tabu. Watu wanasali hapo tokea enzi za Baba wa Taifa akiwa muumini wa hapo na taratibu zilikuwa ni hizo hizo na hakukuwa na malalamiko ya kipuuzi kama haya. Rais anakukwazaje anapoenda kanisani kufanya Ibada!? Kwani amekuja nyumbani Kwako!? Kuna misa Tatu pale...misa ya kwanza, ya pili na ya Jioni. Chagua moja kati ya hapo ambayo hakutakuwepo na Kero za Mh. Rais akiwepo Ibadani.
Kila la kheri ewe mkatoliki zandiki.
Anataka watu wajue kwamba anasali Saint Peters, ndio yale yale ya mtu kupanda Airbus halafu akaposti picha kwenye kundi la whatsapp.

Hajui watu wamekuwa wakisali pale pengine kabla hata hajazaliwa.
 
Mkuu Chakaza, nyakati zimebadilika. Nyerere na Sokoine pale Saint Joseph walitengenewa mabenchi yao, benchi lao lilikuwa linakaliwa na watu watatu, mlinzi mmoja kulia, mwingine kushoto na katikati ndio wanakaa wao. Hawakujiachia kihivyo.
Tatizo la hawa makamanda Uchwara haya mengi walihadithiwa na hawajui ukweli ulivyokuwa mkuu.
Enzi za Baba wa Taifa alipokuwa akienda kufanya Ibada pale St. Peters taratibu na hatua za kiusalama wa Kiongozi wa Nchi zilikuwa ni zile zile. Tena kuna nyakati ilikuwa hata lile benchi linalofuata kwa nyuma lilikuwa tupu kabisa. Inashangaza leo hii hili suala linazua mjadala! Au kwa vile ni Mh. Rais Dr John P. Magufuli!?
 
Walinzi pia si ni watu pia aliokuja nao kanisani..Rais anapaswa kulindwa na kuakikishiwa ulinzi mda wote hili haweze kutimiza majukumu yake yote kwa kipindi atakachokuwa madarakani kwa sababu hana sikukuu wala wikendi..
 
Back
Top Bottom