Hata Obama alisema "Africa needs strong institutions" akimaanisha ina taasisi dhaifu

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Kwa mujibu wa Spika Ndugai usemi huo wa Obama ni matusi kwa Africa nzima?

Na je ule wa Donald Trump kwamba nchi za Africa ni s'holes ulimaanisha nini kama sio mizengwe kama hii, isiyo ya lazima?
Na usemi " biting the hand that feeds you" una maana CAG analishwa na mkono wa aliyemteua au kodi za wananchi?

Ni ajabu kwa Bunge kufumba "jicho" lake au kuzima taa yake badala ya kupambana na jambazi aliyetinga chumbani kwao!
Mbaya zaidi inapoonekana Spika anajaribu ku-preempt kamati zake za PAC na LAAC kuhusu audit queries!
 

Kama taasisi zote za serikali zilizo huru kisheria zingeamka na kuamua kuwa na wivu na uhuru wao kama hivi anavyofanya mzalendo wetu Prof Assad, nchi ingepona hii.

Tumekuwa tukijadanganya na kudanganywa eti mtu mmoja anaweza kuibadilisha nchi,huu ni uongo unaoaminiwa na wajinga peke yao.

Tuna taasisi huru kisheria lakini zinaongozwa na watu wasio huru. CAG ameonyesha mfano bora sana.

Binafsi naomba aendelee kushikilia msimamo wake wa kuendelea kuchapa kazi na kutekeleza majukumu yake ya kikatiba. Historia itakuja kuhukumu ni yupi alifanya anachofanya kwa maslahi ya taifa.
 
Back
Top Bottom