Hata Nyerere alikataa, Rais Magufuli usikubali, shikilia msimamo. Tanzania tusikubali misaada na mikopo yenye masharti kuingilia sovereignty yetu

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,582
Wanabodi

Leo naendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa". Sisi watu sekta binafsi, tunaotegemea tenders, kuna siku unaamka asubuhi, huna tenda, huna kazi, huna hili wala lile, uko kitandani, ndipo unaamua kuamka na Jf, wakati ukisubiri saa 12:00 asubuhi uanze kusikiliza morning news.

Kuna msemo "beggars cannot be choosers" kumaanisha ukiwa omba omba, huwezi kuchagua usaidiwe na nani na usaidiwe nini, wewe kazi yako ni kutembeza tuu bakuli kuomba tuu, chochote utakachopewa au kusaidiwa unapokea na kazi yako ni kusema tuu "hewala*, " asante". Hivyo Tanzania as beggars as we were, we had no choice but to bow down to IMF and World Bank and beg for mercy.

That was then, Nyerere aliwahi kuwakatalia Waingereza kutuingilia, wakati wa mgogoro wa Jimbo la Biafra nchini Nigeria, na akarejesha misaada yao, na kuvunja uhusiano wetu na wao wa kibalozi.

Pia Nyerere aliwahi kuwakatalia Wajerumani walipotaka kutuchagulia marafiki. Kabla ya Muungano, Tanzania ilikuwa na Ubalozi wa Ujerumani Magharibi, na Zanzibar ilikuwa na ubalozi wa Ujerumani Mashariki. Kutokana na ugomvi wao, hadi kujenga ukuta jiji la Berlin, kila watu na upande wao, nchi ikiwa na ubalozi wa nchi moja nyingine inajitoa. Hiyo tulipoungana na Zanzibar, Tanzania tukawa na balozi zote mbili, Ujerumani Magharibu wakatulazimisha kuwafukuza Ujerumani Mashariki, Nyerere aliwagomea, akawarudishia misaada yao na kuwaambia kama hawataki wao ndio waondoke.

Hata mashirika ya kibeberu ya IMF na WB, aliwakatalia kutokana na masharti yao, ila kibano kilipozidi akaamua, kuliko kugeuka nyuma akageuka jiwe la chumvi, bora ang'atuke na kupisha wengine, Mwinyi alipoingia, Ali bow down kwa kufungulia ruhsa zote.

Mambo ya Nyerere na Mashirika ya kimataifa kama World Bank, sasa yanataka kurejeshwa kiaina. Rais Magufuli tangu ameingia, amebana mianya yote ya upigaji hadi vyuma vimekaza, sasa haya mashirika kwa kuanzia na WB wanataka kuleta za kuleta kwa kutishia nyau watu wazima. Baada ya kukosa mahali popote pa kumshikia bango rais Magufuli, sasa wanataka kuzitumia baadhi ya kauli zake kama bangusilo la kutunyima mikopo.
Kama hii taarifa ya CNN eti World Bank wanatunyima mkopo wa dola Milioni 300 kuboresha elimu, kwa sababu Rais Magufuli alisema mwanafunzi atakaeshika ujauzito akiwa shule, masomo basi. Serikali yake haitasomesha.
Baadhi ya kauli za rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli zimeanza kutu cost kama taifa, kwa baadhi ya kauli hizo kutumika kama bangusilo la kutunyima mikopo, hivyo kuti cost na kulicost taifa. moja vya cost hizo ni hii
CNN: Tanzania loses $300m World Bank loan amid crackdown concerns - JamiiForums
Ya Mkuu Tang Zhou,

Hawa WB kama wana yao, nao ikibidi, waende zao tuu, hawawezi kutunyima mkopo wa elimu kwa kisingizio cha kauli ya Rais Magufuli kukataa mimba za utotoni. Tanzania tangu tumepata uhuru, hatujawahi kuruhusu pregnant girls kuendelea na masomo shule zile zile, alichokisema rais Magufuli sio kitu kipya, ni kuusisitiza tuu kitu kile kile kilichokuwepo miaka yote, sasa iweje hawa WB, wazuie mkopo huo muhimu sana wa elimu kwa kisingizio cha sababu hizo?!, hawa nao wana yao, kama wana yao waseme tuu, vinginevyo nao tuwafungulie tuu milango, kuwaonyesha njia ya kutokea na ikibidi kuondoka, nao waondoke tuu, kama Nyerere aliweza nchi ikiwa with nothing, Magufuli atashindwaje sasa nchi ina everything?.

Mwalimu Nyerere aliwahi kuwagomea mabeberu hawa na Mashirika yao ya kimataifa, IMF na WB, japo tuliteseka, bora tuteseke huru kuliko kulishwa tukashibishwa utumwani.

Watanzania tusimame na rais wetu, kamwe tusikubali, nchi yetu na
rais wetu kupangiwa nini aseme na nini asiseme kisa kuogopa kunyimwa mikopo na misaada yenye masharti.

Japo katika hili la pregnant girls kunyimwa fursa za kuendelea na masomo, mimi siliungi mkono kauli ya Rais Magufuli, naiunga mkono ilani ya uchaguzi ya CCM na niliuliza hapa
Jee Kitendo Cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta?. - JamiiForums

Lakini pamoja na kutomuunga mkono rais Magufuli kwenye hili, ila ninamwelewa ana maanisha nini, hivyo kupinga media za nje zinazo shadadia sana mimba za utotoni na hapa nimewapinga,
Huku sio kudhalilishwa kwa Rais wetu na Media za Nje? Je, watanzania tukubali, Tukae kimya? - JamiiForums

Lakini hili la rais wetu kupangiwa nini cha kusema ili asiwaudhi wakubwa hawa, nasimama na rais Magufuli.

Mwalimu Nyerere alipowagomea IMF na World Bank, enzi zile, Tanzania tuliteseka kwa sababu tulikuwa nchi changa, nchi masikini with nothing, lakini sasa Tanzania sio changa tena, sasa Tanzania ni nchi tajiri with everything, madini, gesi asili, ardhi yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, maliasli za kutosha, watu tunao etc, hivyo hatuwezi kutishwa na yeyote kwa rais wetu kupangiwa cha kuongea.
Tena hizo $ Milioni 300 ambazo WB wanataka kutunyanyasia, sisi tunazipata kwa siku moja tuu, kwa rais Magufuli kumkumbusha tuu Prof Richard Thornton atimize ile ahadi yake.

Kwa mambo kama haya ya nchi yetu kuadhibiwa kwa kauli za ukweli za rais wetu, jee kuna haja ya washauri wa rais, wamshauri rais wetu kutafakari baadhi ya kauli zake, ili kuepusha hizi sintofahamu za kimataifa ambazo baadhi zinaanza kutugharimu kama hivi, au kwa vile Tanzania ni nchi huru, a sovereign state, kulinda uhuru wetu na heshima ya nchi yetu, tusikubali nchi yetu inyanyaswe kwa kunyimwa mikopo na misaada yenye masharti magumu ya kuingilia uhuru wetu na uhuru wa rais wetu ambaye ni mkweli daima, aendelee kuwa huru kusema chochote popote regardless of the consequences?.

Hili rais Magufuli kusema chochote popote, pia niliwahi kushauri
Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!. - JamiiForums

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . - JamiiForums

Jumatano Njema.
Paskali
 
Tutakuwa ni watu wa ajabu sana kutomuunga mkono RAISI MAGUFULI kwenye hili maana so far tunaona kabsa POSITIVE IMPACT kwenye hili suala la kuzuia wanafunzi wanaopata UJAUZITO kuendelea na MASOMO maana rate ya mimba kwa wanafunzi imepungua mno awamu hii huwezi fananisha awamu zilizo pita.....
Sisi kunyimwa misaada kuna sababu nyingi tu za KIPUUZI ikiwemo baadhi ya WASALITI wa nchi hii kushinikiza mataifa yenye UHUSIANO nao wa karibu kutunyima misaada hivyo NA HAYA MATAIFA AU TAASISI mbali mbali wanatumia vigezo vya MIMBA KWA WANAFUNZI kama ngao yao ya KUJIFICHA ila nyuma ya PAZIA wanaujua UKWELI....
Pia ulinzi wa RSILIMALI ZETU hili nalo ni sababu nyingine inayowaumiza sana hawa MABWANA WAKUBWA hivyo lazima watafute sababu za KIPUUZI kutupiga indirect kwa kisingizio cha Mimba kwa wanafunzi..mara demokrasia mara Uhuru wa HABARI...
Kama kweli wanania ya DHATI kusaidia hawa mabinti wanaopata UJAUZITO wawachukue na kuwasomesha mahali ambapo WANARUHUSU HUU UPUUZI.....
 
Nafikiri wengi labda hamuelewi World Bank ni nini, ni Benki kama vile tu CRDB ilivyo ni Benki na in Wamiliki.
Pia labda hamuelewi jinsi mfumo wa Brettton woods unavyofanya kazi, Benki ya Dunia haiwezi kuinyima TZ mkopo hata siku moja kwanza ni kinyume chake ni lazima Tanzania ichukue huo mkopo, kwa maana nyingine ni lazima TZ iwe na Deni ndiyo mfumo wa Dunia ulivyo.

Sasa kilichopo ni kuishinikiza Serikali ili ikubali masharti yao ambayo mengi yamejificha na wala hayana uhusiano wowote na ushoga hiyo ni false flag tu, inawezekana ikawa ishu ni Mikataba ya Madini na Gesi iliyobadilishwa na Serikali yetu, au fiscal policy za Serikali ambapo zinawaathiri banksters ikumbukwe kwamba wadau au wamiliki wa Benki ya Dunia ndio hao hao wanufaika wa Madini yetu, hivyo msidanganyike, the devil is always in the details, kuna kikubwa nyuma yake.

Lkn mkopo wa Benki ya Dunia ni lazima tuchukuwe iwe tunataka au hatutaki kwani ni lazima tuwe na deni ambalo tutalilipa kwa interest, na hiyo interest ndiyo Muzungu au finance World na banksters wanaoitegemea.

Vita vyoote Duniani huanzishwa na Banksters, na sababu ni hiyo interest, Gadafi aliuliwa shauli alikataa kutumia US dollar, Vita vyoote vya Dunia kuanzia Napoleon mpaka Vita kuu ya pili vilianzishwa na finance World na vilihusu fedha.

Isitoshe unaongelea sovereignty, hakuna sovereignty Tanzania tena kwani tumeshasaini kama vipofu international agreements nyingi sana kama kama ICC ambapo foreigners wana uwezo wa kuarrest Mtanzania na kumfunga Hague, tumesaini Mikataba mingi ya climate, sisi tuko African Union tumesaini free trades agreements za African Union hizi zote zinaondoa sovreignty na kuikabidhi nchi kwa international na globalist ambao ndio wanamiliki World Bank, na ndo maana Trump amegoma na kuiondoa USA.

Wengi mnamdharau Trump lkn ukimfwatilia atawafundisha mengi sana jinsi Dunia inavyofanya kazi, ...
 
Come on Mayalla,
Hakuna taifa linalofikiri linaweza kukubali kununua sera mpya isiyotekelezeka katika mazingira na hali ya ndani ya kiuchumi, kisiasa na kijamii/kiutamadani. Tanzania ingekubaliana na sera tafsiri yake ni kuendelea kuomba misaada na/au mikopo kutoka kwa hao IMF, WB na mabeberu wengine ili kuendelea kuwatunza wanafunzi wazazi, na pengine watoto na waume zao. Hizo dola million 300 zinafahamika kuwa gharama ya ku-introduce policy mpya (hovyo) hapa nchini. Ni metego wa kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa maskini. Ni kuongeza mzigo katika sekta ya elimu katika mazingira ambayo tayari serikali inalemewa mzigo uliopo tayari. Kwa hiyo, kukubaliana na sera hii inabainisha kuwa miaka yote ya siku za usoni sharti Tanzania iendelee kutegemea WB, IMF, na mataifa ya kibeberu. Huwezi kuwa na sera inayolengo watoto wa kike kuolewa na kupata uja uzito, na kuzaliana huku wakiwa mashuleni halafu utarajie kupata taifa imara na linalowajibika. Tunaweza kujiuliza: kama hivyo ndivyo kuna haja gani ya kuwa na sheria ya kuwalinda watoto wa kike wasipate ujauzito?

Huko tulikotoka, enzi za Kikwete, kulikuwa na tatizo kubwa la 'uswahili'. Wataalam wa serikali [wengi wao wakiwa na vyeti fake] walikuwa wakianza kufkiri kuhusu sera yoyote kwa kuangalia pesa iliyopo/watakayopata (rushwa). Ukiwa na civil service ya manma hiyo huwezi kujenga taifa imara hata kidogo. Taifa haliwezi kujengwa kwa sera za kipoyoyo namna hiyo. Pesa haipswi kuongoza uamuzi wa sera bali kinyime chake. Wataalam wa serikali wanapaswa kuchambua na kujua madhara ya sera yoyote kabla ya kuruhusu pesa iliyopo/inayotolewa iamue juu ya sera za umma zinazopaswa kutekelezwa. Sera hii ya seikali kusomesha wali na kutunza watoto wao ni kitanzi kingine dhidi ya maendeleo yetu. Sisi bado ni taifa change hatupaswi kukubaliana na sera za kipuuzi namna hii. Ukiona Benki ya Dunia wanataka ununue sera na wao wako tayari kulipa pesa unapaswa kutilia mashaka. Kwamba WB watupatie tzs. billion 600 kisha tukikubali tupokea sera ya kuruhusu watoto wa kike waliojifungua kuendelea na masomo ya shule za msingi na sekondari ni kuliingiza taifa kwenye mtego wa miaka yote. Kwamba kila mwaka Tanzania itaendelea kubeba bakuli la kuomba misaada na mikopo nje ya nchi kwa ajii ya kutunza mama, watoto na pengine waume zao!

Njia ora ya kuhakikishia watoto wa kike wanapata elimu bora sawia na watoto wa kiume ni wajibu wa wazazi, na kwa kiasi fulani waliimu. Wazazi wanawajibika kulea watoto wao, wa kike na kuime sawia kwa kuzingatia maadili. Serikali haipaswi kulea mtoto mmoja mmoja akiwa nyumbani kwa wazazi wake. Mabweni ya shule za wasichana yanatakiwa kusimamiwa ipaswavyo. Hatuwezi kuzawadia mzazi ambaye ni lousy akiwaacha watoto lousily akitarajia serikali ku-step-in nyumbani kwake kumlelea watoto wake. Serikali inapaswa kushushughuika na usimamizi wa utekelezaji wa sera za maendeleo siyo masuala binafsi ya familia ya mtanzania mmoja mmoja. Kulea watoto ni parental duty siyo government obligation. Ukiwa mzazi lousy na watoto ukawaacha kuwa lousily wasisome kwa mujibu wa disciplinary code ya shule za msingi na sekondari usitarajie serikali kuja nyumbani kwako kukulelea watoto. Ikitokea hivyo, basi ujue suala la watoto kupelekwa polisi, mahakamani na kisha gerezani.

Kwa kisingizio chochote kile, kuruhusu watoto wa kike waliopata ujauzito kuendelea na masomo katika mfumo rasmi wa elimu tulionao sasa ni kuendeleza the obvious colonial nonsenses za wazungu; kwa mfano wanaume kwa wanaume [juzi tumeona kwenye mitandao ya kijamii, Waziri Mkuu wa Luxembourg ameoa mwanaume mwenzake] au wanawake kwa wanawake kuoana wao kwa wao.
 
Tutakuwa ni watu wa ajabu sana kutomuunga mkono RAISI MAGUFULI kwenye hili maana so far tunaona kabsa POSITIVE IMPACT kwenye hili suala la kuzuia wanafunzi wanaopata UJAUZITO kuendelea na MASOMO maana rate ya mimba kwa wanafunzi imepungua mno awamu hii huwezi fananisha awamu zilizo pita.....
Sisi kunyimwa misaada kuna sababu nyingi tu za KIPUUZI ikiwemo baadhi ya WASALITI wa nchi hii kushinikiza mataifa yenye UHUSIANO nao wa karibu kutunyima misaada hivyo NA HAYA MATAIFA AU TAASISI mbali mbali wanatumia vigezo vya MIMBA KWA WANAFUNZI kama ngao yao ya KUJIFICHA ila nyuma ya PAZIA wanaujua UKWELI....
Pia ulinzi wa RSILIMALI ZETU hili nalo ni sababu nyingine inayowaumiza sana hawa MABWANA WAKUBWA hivyo lazima watafute sababu za KIPUUZI kutupiga indirect kwa kisingizio cha JAMBO lingine kabsa
Kama kweli wanania ya DHATI kusaidia hawa mabinti wanaopata UJAUZITO wawachukue na kuwasomesha mahali ambapo WANARUHUSU HUU UPUUZI.....
Hebu lete takwimu za sasa na awamu iliyopita ili tujiridhishe unachokisema!
 
Kuhusu mimba kwa wanafunzi, serikali ijikite kwenye ilani ya chama tawala ili isionekani nchi inaongozwa na mtu mmoja.

Kwa upande wa IMF na World Bank, napendekeza mfumo wa kuliokoa taifa na hali ya ombaomba ungewekwa ili kila rais ajaye afuate mfumo huo.
Mfumo ulinde raslimali zetu dhidi ya "wachukuaji" wanaojiita wawekezaji wa kigeni.
Mfumo ulete mgawanyo sawa wa pato la taifa kulingana na mahitaji na mazingira.

Tukifankiwa ktk hilo tutaondokana na "one man show" na madhara yake tutaumia kama taifa.

Ni mtazamo tu
 
Tutakuwa ni watu wa ajabu sana kutomuunga mkono RAISI MAGUFULI kwenye hili maana so far tunaona kabsa POSITIVE IMPACT kwenye hili suala la kuzuia wanafunzi wanaopata UJAUZITO kuendelea na MASOMO maana rate ya mimba kwa wanafunzi imepungua mno awamu hii huwezi fananisha awamu zilizo pita.....
Sisi kunyimwa misaada kuna sababu nyingi tu za KIPUUZI ikiwemo baadhi ya WASALITI wa nchi hii kushinikiza mataifa yenye UHUSIANO nao wa karibu kutunyima misaada hivyo NA HAYA MATAIFA AU TAASISI mbali mbali wanatumia vigezo vya MIMBA KWA WANAFUNZI kama ngao yao ya KUJIFICHA ila nyuma ya PAZIA wanaujua UKWELI....
Pia ulinzi wa RSILIMALI ZETU hili nalo ni sababu nyingine inayowaumiza sana hawa MABWANA WAKUBWA hivyo lazima watafute sababu za KIPUUZI kutupiga indirect kwa kisingizio cha Mimba kwa wanafunzi..mara demokrasia mara Uhuru wa HABARI...
Kama kweli wanania ya DHATI kusaidia hawa mabinti wanaopata UJAUZITO wawachukue na kuwasomesha mahali ambapo WANARUHUSU HUU UPUUZI.....
Unaweza kutuambia hao wasaliti ni akina nani na mmewafanya nini kwa kulisaliti taifa?
Hays ndo madhara ya kukurupuka kwenye mambo yanayohitaji busara, hekima na weledi
 
Tanzania haijanyimwa mkopo bali masharti ya mkopo unaifanya Tanzania isiweze kukopa.

Kwani huu ni mkopo wa kwanza kutoka World Bank?

Je, hatulipi hiyo mikopo mingine waliyotukopesha?

Unaweza tu kunyimwa mkopo kama huwezi kulipa na sio vinginevyo.

Tatizo la hii mikopo ni fimbo ya kukuchapia pale unapokataa baadhi ya masharti yaliyoko kwenye small print.

Kama suala ni wanafunzi waliozaa kutorudi shuleni, mbona hii sheria imekuwepo nchini kabla hata ya Rais Magufuli kuingia madarakani? Kwa nini hawakutunyima mkopo huko nyuma kama suala la hili ni muhimu sana katika vigezo vya mkopo?

Utawasikia wanakuambia tatizo ni utawala bora wakati huo huo nchi kama Rwanda zenye zero utawala bora ndizo wanazifanya kama mfano wa kuigwa Africa kiutawala.

Tatizo ni Raslimali za taifa ambazo zimetungiwa sheria ya kuzilinda kwa faida ya taifa na vizazi vijavyo.
 
Mama Kamou alianzisha hostel Weruweru ya mabinti waliopata mimba. Baada ya kujifungua walirudi lakini waliishi kwenye hostel yao.
Suala la msingi ni je, wangapi walifanikiwa? Je, kipi bora kati ya kuzuia mtoto wa kike kupata mimba au kuchochea wapate mimba na baadaye tuwatengee hostel za wazazi! Sijazungumzia walobakwa ambao nina uhakika walowabaka wapo Segerea ambapo wakitoka hao watoto wao watakuwa na wajukuu. Njia anayotumia JPM ni mojawapo ya njia za kuzuia mimba za utotoni. Tatizo kubwa hapa kwetu tunakosa watafasiri wa maagizo ya Rais tu nadhani Pasco unanipata
 
Hivi kwanini watu mnafikiria hasa kuwawekea watu kikomo cha KUSOMA ?

Hili taifa la ajabu kweli.

Inaonekana Nyerere alikuwa kiumbe wa "pekee" sana nchi hii, maana mitazamo yake na yetu ni tofauti kabisa.

Moja ya ahadi za mwanaTANU zilikuwa ni "Nitajielemisha mimi kwa nguvu zangu zote kwa ajili yangu na taifa langu"

Kwasasa naona hakuna hata anaeihitaji, kinachotumika ni "kidumedume cha mila za kizamani huko karne ya 9, kudidimizana"

Taifa linaloruhusu msichana mwenye umri wa miaka 14 kuolewa kisheria na wakati huo huo linaamini ni mtoto, then tena linapinga watoto kuolewa. Ni taifa lisiloeleweka na lisilo na dira.

Kwanza kuzaa siyo kosa kisheria, pili kurudi shule ni haki ya msingi na haiwezi kunyang'anywa mtu kwa sababu yoyote.

Mtu yeyote, awe Mzee, kijana, mbibi, ana watoto 200, hana mtoto, malaya, mtoto mdogo, Mjamzito, baba wa familia n.k kama anataka KURUDI SHULE - ARUDI. Tena serikali ihamasishe kila mtu kusoma kadri awezavyo. Ndio maana huko nyuma tulikuwa na UPE, MEMKWA n.k
 
Suala la msingi ni je, wangapi walifanikiwa? Je, kipi bora kati ya kuzuia mtoto wa kike kupata mimba au kuchochea wapate mimba na baadaye tuwatengee hostel za wazazi! Sijazungumzia walobakwa ambao nina uhakika walowabaka wapo Segerea ambapo wakitoka hao watoto wao watakuwa na wajukuu. Njia anayotumia JPM ni mojawapo ya njia za kuzuia mimba za utotoni. Tatizo kubwa hapa kwetu tunakosa watafasiri wa maagizo ya Rais tu nadhani Pasco unanipata
Kwani rais anatumia lugha gani tusiyoielewa? Kwa uzowefu wa kufanya kazi na watoto nimejifunza kuwa elimu na uwelewa kunasaidia sana watoto. Watoto wseleweshwe athari za mimba na ikiwezekana waonyeshwe video za kero ya kulea vichanga ambavyo huletwa kwa njia ya ngono zembe.
 
This Aid business is killing us...hawa tunaowaita development partners wanakupa kamkopo then they make noise as they gave birth to you. Hakuna kitu kilikuwa kina kera nchi hii kama kuomba omba mikopo wakati tuna rasilimali za kutosha. Ifike mahali tujitegemee..tuwe na budget surplus
 
Back
Top Bottom