Hata nyakati za ukoloni, ukoloni uliondolewa kwa nguvu ya chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata nyakati za ukoloni, ukoloni uliondolewa kwa nguvu ya chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPANDA Jr, Jan 26, 2012.

 1. MPANDA Jr

  MPANDA Jr JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,299
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Leo hii Watanzania wenzangu wengi bado hawajui kuwa nyakati za Ukoloni "Babu zetu" walikerwa sana na matendo mabaya yaliyotendwa na Wakoloni. Kwa zaidi ya miongo 7 yaani miaka sabini ya utawala wa kikoloni katika Tanganyika na Tanzania babu zetu walipitia vipindi mbalimbali vya kudai ukombozi, moja kati ya hivyo ni kupigana ama kupambana na wakoloni kwa Silaha: Mfano ni akina Mkwawa, Mirambo, Isike Mangi Sina, Kinjekitile, Bushiri na wengine, leo hii vita vya majimaji vimekuwa Historia isiyoakisi uhalisia wa kwanini wao walipambana
  Kumbe vicheko vyetu juu ya "Babu zetu" kwamba walikuwa wajinga hata wakakubali kutawaliwa ni sawa na kumcheka mtu kipofu aliyekanyaga dimbwi la maji machafu ilihali wewe mwenye macho mazimaa ukidumbukia katika karo la choo. Nayasema haya kwa sababu kigezo kikubwa kwa "Babu zetu" tunaambiwa "Hawakuwa na Elimu" ndio maana walikubali
  1. Kulipwa Ujira mdogo 9sio mshahara)
  2. kutozwa kodi kubwa
  3. Kuwekwa makambini viwandani
  4. Kufanyishwa kazi ngumu na kwa muda mrefu
  5. Kunyimwa elimu
  6. Rasilimali zao kama Arhi, Madini, Misitu nk ziliporwa na wakoloni
  7. Utawala ulikuwa wa kigeni
  8. Unyanyasaji wa raia na mengineyo
  Katika harakati hizo Watanganyika walikumbana na kikwazo cha vyama vya siasa vya wageni kama European Association, Indian Association, UTP na vingine ambavyo vilitawala kwa niaba ya nchi zao. Ndipo kati ya miaka ya 1948 hadi 1950's watanganyika waliamua nao kuunda vyama vyao kama kile cha African Association ambacho kilikatazwa kabisa na Gavana kijihusisha na "SIASA" lakini baadaye kufikia 1954 kilipatikana chama cha TANU.

  Sasa point ta msingi hapa ni hii: Aliyetuvusha katika mchakato wa kupata "UHURU" ni TANU kwa njia ya "KURA TATU" ambayo J.K.Nyerere kwa kuhamasisha Watanganyika kujitambua alifanikiwa kuwashinda "Wazungu" na akawa Waziri mkuu mwaka 1961. Hii ni njia BoRa ya kupata ukombozi ambayo wenzetu wa Zanzibar walishindwa kuitumia bali walifanya mapinduzi. Kama ilivyokuwa kwa TANU katika kuleta UHURU ni maoni yangu kuwa ni KAZI YA CHADEMA kuleta UKOMBOZI kwa njia ileile ya TANU....
  Itaendelea......................

  Asante kwa Kunisikiliza
   
 2. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu kwa hiyo nikweli kuwa dhana ya kupata uhuru kwa blaablaa ni ya uongo?
   
Loading...