Hata Mwinyi amshangaa Kikwete, Serikali lazima ilinde ajira za wananchi wake ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata Mwinyi amshangaa Kikwete, Serikali lazima ilinde ajira za wananchi wake !

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, May 7, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mwinyi: Serikali ilinde ajira za wananchi wake

  Na Fredy Azzah - Mwananchi

  SIKU mbili baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa hotuba kali na maagizo ya kutimua wafanyakazi wote ambao wangeitikia tangazo la mgomo lililotolewa na Tucta, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema serikali inatakiwa kulinda ajira za wananchi wake ili kudumisha amani.

  Rais Kikwete, akizungumza na wazee wa Dar es salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jumatatu iliyopita, alisema mgomo huo ulioandaliwa na Tucta ni batili na kwamba, yeyote ambaye angehusika, angechukuliwa hatua za kisheria; ikiwa ni pamoja na nguvu ya polisi kutumika kuwazuia watakaoingia mitaani kuandamana.

  Katika hotupa yake Kikwete alisema viongozi wa Tucta kuwa ni wazandiki, waongo, wanafiki na wafitini kwa kuwa wanakwenda kinyume na makubaliano yao na serikali.

  Lakini jana Mzee Mwinyi alionyesha mtazamo tofauti jana katika hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Shule ya Kimataifa ya Wavulana ya Feza, ambako alitoa somo fupi la dhima ya utu.

  "Taasisi au nchi yoyote ambayo itakuwa haiheshimu utu wa wananchi wake, itakuwa inajichimbia kaburi," alisema Mwinyi kwenye hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na mtoto wa mfalme wa Norway, Haakon Magnus na baadhi ya viongozi wa nchi mbalimbali.

  "Ni lazima kwa serikali yoyote ile kuwalinda watu wake na si kufanya uadui kati yake na wananchi. Serikali yoyote duniani ni lazima ilinde ajira za wananchi wake ili iweze kudumisha amani na kuheshimu utu wa raia wake."

  Hotuba ya Rais Kikwete ilitafsiriwa kuwa ni ya vitisho na ambayo ilitolewa bila ya ushahidi wa kutosha kutoka pande zote mbili kuhusu maendeleo ya mazungumzo baina ya serikali na Tucta, ambayo ilieleza baadaye kuwa rais alipaswa kwanza kusikiliza viongozi wa shirikisho hilo badala ya kusikiliza watendaji wa serikali pekee.

  Mgomo huo ambao ulipangwa kuanza Mei 5, umesogezwa mbele hadi baada ya Mei 8, siku ambayo serikali na Tucta watakutana kujadili suala la kima cha chini cha mshahara wa sekta ya umma, suala ambalo hadi sasa pande zote hazijafikia muafaka.

  Mbali na haki ya ajira, Mwinyi pia alisema haki ya kuishi lazima ilindwe na serikali ili kuweza kudumisha amani na kuheshimu utu wa watu wake.

  “Vitu kama uhuru wa kujieleza, kusali, mawasiliano lazima vipewe ruksa, lakini pia ajira na kuishi, haki hizi lazima zilindwe na serikali,” alisema Mwinyi.

  Kauli hiyo ya Mwinyi imekuja wakati kukiwa bado na kutoelewana baina ya serikali na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) lililositisha mgomo uliopangwa kuanza Mei tano mwaka huu, baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa hotuba kali ambayo wadau mbalimbali walisema ilikuwa imejaa vitisho.

  Mbali na hayo Mwinyi alisema: “Shule ya Feza ni nzuri sana, ni nzuri kwa sababu ina walimu wazuri na hata wanafunzi wake ni wazuri, hata katika matokeo yake imekuwa ikifanya vizuri na kuwa ndani ya shule tano bora.”

  Kabla ya kutoa hotuba yake, baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo walieleza kwa nyakati tofauti juu ya maana ya utu kutokana na mafunzo waliyopata kutoka kwa viongozi hao wa vijana wa dunia.

  Watu mbalimbali, akiwemo mtoto huyo wa mfalme wa Norway walikuwa wakihamasika na kuwashangilia wanafunzi hao walipookuwa wanaeleza maana ya utu, umuhimu wa kuheshimu utu wa mtu na athari zake endapo hautaheshimiwa.

  Prince Haakon aliwaambia vijana hao ni muhimu kuheshimu utu na kujiamini kwa kuwa wao ndiyo watakaoweza kuifanya Afrika na dunia kwa ujula kuwa mahala pazuri na salama pakuishi.

  Baadhi ya wanafunzi hao wakizungumza mbele ya Mzee Mwinyi walisema "utu ni kuheshimiana baina ya mtu na mtu; kusema ni sisi na si ni mimi, kujiuliza nimetoa nini na siyo nimepokea nini".

  Wengine pia walisema, kujilimbikizia mali nyingi si utu na kuwa hata mtu huyo aliyejilimbikizia mali wakati anazungukwa na watu masikini haishi maisha ya amani kwa kuwa wale wasio nacho nao watakuwa wakifanya kila liwezekanalo kupata mali za mtu huyo tajiri.

  Yaani hata Mwinyi amshtukia Mkwere, serikali gani inafanya uadui na wananchi wake ? "Uhuru wa kujieleza, kusali, mawasiliano lazima vipewe ruksa, lakini pia ajira na kuishi, haki hizi lazima zilindwe na serikali," asema Mwinyi.

  Na mimi Mag3 nauliza, Serikali gani inawaogopa mafisadi lakini iko tayari kuwapa vilema wafanya kazi wake ? Nawaomba wazalendo wazidi tu kukusanya data, safari hii mkuu wa kayahaponi akitoka madarakani !
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Raisi mwenyewe anajua dhahiri kuwa alikuwa anavurunda, lakini akaona bora afe na tai shingoni.
   
 3. masharubu

  masharubu Senior Member

  #3
  May 7, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani mwinyi ni mzee wa wapi? Na fikiri anakaa dsm na si kule mchambawima, mwembe mimba, kibanda maiti ,au makundu uchu. Mbona hatukumuona pale diamond?inabidi jamaa ajiweke sawa huu ni wakati mwengine si enzi zile za zama za mawe
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Sasa shangaa wale wanaoandamana kuunga mkono hotuba basi!
   
 5. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kikwete ameshauriwa vibaya, ana washauri wa kisiasa pia wanaotakiwa kumpa mwelekeo wa hotuba, mambo ya kusisitiza, achilia mbali waliompa hotuba ile
   
 6. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Safi ruksa, mpe ukweli huyo mkwere yeye anakurupuka tu bila kuchuja la kusema au kufanya.
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  May 7, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kikwete yeye mwenyewe ni mwepesi mno, ndo maana wanamdanganya na anaganganyika kirahisi....
  wanamdanganya hata muda wa vikao , wanamwambia TUCTA waligoma kwenda asubuhi wakati kikao kilikua ni saa 8 Alasiri.
  Yeye mwenyewe, anajirundikia wasaidizi wahovyo, ni kimeo huyu Mkwere.
   
 8. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Tatizo ubabe ndio kawaida ya maraisi wengi waliopitia jeshini.kwa kifupi ccm haijali wananchi na wanaona kwamba wamejenga kingdom yao ndio maana wajeuri na wana kiburi.
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Labda anataka aende Ze Hague kula pilau la kizungu.
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Jamani jamani, JK kalikoroga kweli, jana nilikuwa sehemu bibi mmoja naamini atakuwa na myaka zaidi ya 65, kwani ni bibi kweli, nilishangaa alipo toa maoni yake kwamba sasa raisi gani anataka kuua watoto wetu? Nikamuuliza kwanini bibi? akajibu si kasea polisi watawipiga risasi watoto wetu wakigoma?

  Nilitoka pale taaratibu kichwa chini kwani sikutegemea maelezo kama hayo ayasee bibi wa aina ile!
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  May 7, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamani tumpongeze Rais, kwa mara ya kwanza kaamua kutotoa ahadi - au mlitaka awaahidi tena?
   
 12. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Hayo mliyayasema wanajamii nimeyaelewa na nimeyaheshimu.
  Mimi ninatamani ugeni ule ungekuwa umekwenda kwenye shule ya sekondari ama msingi ya Umma. Lakini unajua nini, hawathubutu kuwakaribisha kule kwakuwa kwanza mazingira ya shule za umma ni mabovu na waalimu wenyewe ndio hao wafanyakazi wa serikali wanaonyanyaswa na kudharauliwa na serikali yao kila kukicha.
  Rais na wenzake wanasahau kwamba: Mwalimu mnyonge hawezi kumuandaa mwanafunzi jasiri, bali mwalimu mnyonge huzalisha mwanafunzi mnyonge na mwanafunzi mnyonge huzalisha Taifa nyonge na Taifa nyonge hutawaliwa Daima hapa duniani na kunyanyaswa katika kila nyanja.
  Mfano ni huu wa watanzania kudhaniwa kuwa ni wakarimu ilhali ni wanyonge, na ninasema wanyonge kwakuwa hakuna binadamu mkarimu anayeweza kuwa muuaji wa binadamu mwenzake kwa kisingizio cha kupata utajiri.
  Akili kichwani mwenu ndugu zanguni.
  Mungu Ibariki Tanzania na Watu Wake!
   
 13. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hao wanaounga mkono si wa kuwashangaa, bali ndo wale wale wanaounga mkono ilimradi tu mtu yupo madarakani. na kimsingi ndo hao wanaotutesa kwas kutuweka hapa. Japo si wa kuwalaumu maana kwa kifupi hawajitambui. Ha hii Tanzania ndo wengi zaidi. Ndo maana tutawatukana na tutashinda kwa kishindo hata kama kura zenu hamtatupa
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2010
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kuongea na wananchi kwa JK kulikuwa na ulazima gani wa kuwepo kwa RO, Mwamunyange na Said Mwema ? What was the message ukiangalia ile hotuba kwa undani ?

  Msaada wenu tafadhali
   
 15. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona kaahidi kuwaadabisha wafanyakazi watakaogoma.
   
 16. g

  godybn2005 Member

  #16
  May 7, 2010
  Joined: Apr 20, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani..Rais hajui analotenda...! Dira yake iko wapi? Vipaumbele ni vipi? Maslahi ya taifa anayatafsiri vipi? October is around the corner...! " Come..go and chant down the babylon one more time" Mi nadhani..ifikie mahali Wafanyakazi na wakulima watengeneze alliance ya kulinda maslahi yao katika nchi...! Wao ndo wengi na ndio wanaojenga uchumi wa nchi nyingi (Especially wakulima). Chama kinachijidai ni cha wakulima na wafanyakazi kwa kuweka jembe na Nyundo kwenye bendera sio cha kwao..Ni cha wafanyabiashara na wanasiasa....! Amkeni...We are gonna chant down the babylon system this October..!
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ahh...ile ilikuwa ni show-off tu hana lolote. Alitaka kuonyesha tu kwamba ni rais na aliyoyasema ni mawazo ya wote aliokuwa nao lakini uzuri ni kwamba kifo anachowatakia wananchi hohe hahe na yeye hatakikwepa.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,611
  Likes Received: 82,195
  Trophy Points: 280
  Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani Send to a friend Thursday, 06 May 2010 22:46
  Na Fredy Azzah:
  Mwananchi

  SIKU mbili baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa hotuba kali na maagizo ya kutimua wafanyakazi wote ambao wangeitikia tangazo la mgomo lililotolewa na Tucta, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amesema serikali inatakiwa kulinda ajira za wananchi wake ili kudumisha amani.Rais Kikwete, akizungumza na wazee wa Dar es salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jumatatu iliyopita, alisema mgomo huo ulioandaliwa na Tucta ni batili na kwamba, yeyote ambaye angehusika, angechukuliwa hatua za kisheria; ikiwa ni pamoja na nguvu ya polisi kutumika kuwazuia watakaoingia mitaani kuandamana.

  Katika hotupa yake Kikwete alisema viongozi wa Tucta kuwa ni wazandiki, waongo, wanafiki na wafitini kwa kuwa wanakwenda kinyume na makubaliano yao na serikali.

  Lakini jana Mzee Mwinyi alionyesha mtazamo tofauti jana katika hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Shule ya Kimataifa ya Wavulana ya Feza, ambako alitoa somo fupi la dhima ya utu.

  "Taasisi au nchi yoyote ambayo itakuwa haiheshimu utu wa wananchi wake, itakuwa inajichimbia kaburi," alisema Mwinyi kwenye hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na mtoto wa mfalme wa Norway, Haakon Magnus na baadhi ya viongozi wa nchi mbalimbali.

  "Ni lazima kwa serikali yoyote ile kuwalinda watu wake na si kufanya uadui kati yake na wananchi. Serikali yoyote duniani ni lazima ilinde ajira za wananchi wake ili iweze kudumisha amani na kuheshimu utu wa raia wake."

  Hotuba ya Rais Kikwete ilitafsiriwa kuwa ni ya vitisho na ambayo ilitolewa bila ya ushahidi wa kutosha kutoka pande zote mbili kuhusu maendeleo ya mazungumzo baina ya serikali na Tucta, ambayo ilieleza baadaye kuwa rais alipaswa kwanza kusikiliza viongozi wa shirikisho hilo badala ya kusikiliza watendaji wa serikali pekee.

  Mgomo huo ambao ulipangwa kuanza Mei 5, umesogezwa mbele hadi baada ya Mei 8, siku ambayo serikali na Tucta watakutana kujadili suala la kima cha chini cha mshahara wa sekta ya umma, suala ambalo hadi sasa pande zote hazijafikia muafaka.

  Mbali na haki ya ajira, Mwinyi pia alisema haki ya kuishi lazima ilindwe na serikali ili kuweza kudumisha amani na kuheshimu utu wa watu wake.

  “Vitu kama uhuru wa kujieleza, kusali, mawasiliano lazima vipewe ruksa, lakini pia ajira na kuishi, haki hizi lazima zilindwe na serikali,” alisema Mwinyi.

  Kauli hiyo ya Mwinyi imekuja wakati kukiwa bado na kutoelewana baina ya serikali na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) lililositisha mgomo uliopangwa kuanza Mei tano mwaka huu, baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa hotuba kali ambayo wadau mbalimbali walisema ilikuwa imejaa vitisho.

  Mbali na hayo Mwinyi alisema: “Shule ya Feza ni nzuri sana, ni nzuri kwa sababu ina walimu wazuri na hata wanafunzi wake ni wazuri, hata katika matokeo yake imekuwa ikifanya vizuri na kuwa ndani ya shule tano bora.”

  Kabla ya kutoa hotuba yake, baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo walieleza kwa nyakati tofauti juu ya maana ya utu kutokana na mafunzo waliyopata kutoka kwa viongozi hao wa vijana wa dunia.

  Watu mbalimbali, akiwemo mtoto huyo wa mfalme wa Norway walikuwa wakihamasika na kuwashangilia wanafunzi hao walipookuwa wanaeleza maana ya utu, umuhimu wa kuheshimu utu wa mtu na athari zake endapo hautaheshimiwa.

  Prince Haakon aliwaambia vijana hao ni muhimu kuheshimu utu na kujiamini kwa kuwa wao ndiyo watakaoweza kuifanya Afrika na dunia kwa ujula kuwa mahala pazuri na salama pakuishi.

  Baadhi ya wanafunzi hao wakizungumza mbele ya Mzee Mwinyi walisema "utu ni kuheshimiana baina ya mtu na mtu; kusema ni sisi na si ni mimi, kujiuliza nimetoa nini na siyo nimepokea nini".

  Wengine pia walisema, kujilimbikizia mali nyingi si utu na kuwa hata mtu huyo aliyejilimbikizia mali wakati anazungukwa na watu masikini haishi maisha ya amani kwa kuwa wale wasio nacho nao watakuwa wakifanya kila liwezekanalo kupata mali za mtu huyo tajiri.
   
 19. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu umenikumbusha, kimsingi CCM inabidi waondoe hiyo alama ya nyundo ya wafanyakazi, watafute alama nyingine ya mafisadi waiweke hapo, kwani M/kiti wao kaisha sema wafanyakazi kura zenu hazimtishi na hana shida nazo! sasa alama yao ya nini? weka ya mafisadi ambao kimsingi ndio chama kina walinda kwa nguvu zote.
   
 20. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Nawapongeza wote wana jf kwa mawazo makini. Keep it up.
   
Loading...