Hata Mugabe alijifanya kichwa ngumu

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,801
Mugabe alijifanya kichwa ngumu, hakujali maonyo wala ushauri. Alidhani Waafrika wenzake wangemsapoti kwa wazo lake zuri kabisa la kuwarudishia wazawa mali yao ya ardhi.

Lakini mambo yalivyomuendea kombo nchi zote za Afrika ziliingia mitini. Leo Mugabe kaenda zake lakini mateso na dhiki zilizotokana na vikwazo vya mabeberu kawaachia wana Zimbabwe.

Sasa wako hoi wamejichokea. Hili la Makonda kuzuiwa kuingia Marekani ni warning light na Rais Magufuli akijifanya nunda yatatukuta ya Zimbabwe.

Rais Magufuli ataondoka tutabaki tunalia na kuomboleza peke yetu.

Watu wanawaambia ukweli hamsikiii mmekalia kushabikia hata ya ovyo. Shauri yenu msije kusema hatukuwaambia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom