Hata Kusimamisha Mradi wa Bandari ya Bagamoyo Rais Magufuli aliokoa Taifa

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,081
2,000
Mradi wa kujenga Bandari ya Bagamoyo ambao ulikuwa ugharimu dola bilioni 10 ulikuwa ni mzigo mkubwa sana kwa Watanzania.

Watanzania tunatakiwa tumshukuru sana Rais Magufuli kusimamisha mradi huo la sivyo ingechukua miaka mingi sana kuilipa China mkopo wa ujenzi wa bandari hiyo ambayo isingekuwa na manufaa kiuchumi kwa Tanzania. Upanuzi wa bandari ya Dar kwa gharama nafuu ni hatua nzuri aliyochukua Rais Magufuli.

Kwa kipindi cha miaka miwili cha utawala wa serikali ya awamu ya 5 imeonyesha dira na mwelekeo mzuri katika kuwekesha kwenye miradi yenye manufaa kwa taifa.
 
Jua usiyoyajua

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
1,129
2,000
Tusiyaseme tusiyoyajua. Plan to construct Bagamoyo Port is still underway. Hatuwezi kutegemea bandari moja kila siku, tunapoongeza nyingine ni maendelae. Akili ni nywele kila mtu ana zake.
 
Zanzibar-Nyamwezi

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
812
500
Mtoto wa mjini hana hata aibu kwa alivojipendelea yeye, eneo lake, dini yake. Yaani kama sio muda wake kuisha ilibaki kidogo nchi nzima tusilimu tu kama kina lugumi ili na wewe uonekane mtanzania
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,081
2,000
Tusiyaseme tusiyoyajua. Plan to construct Bagamoyo Port is still underway. Hatuwezi kutegemea bandari moja kila siku, tunapoongeza nyingine ni maendelae. Akili ni nywele kila mtu ana zake.
kama bandari ya Dar imekosa mizigo ya kutosha kuna umuhimu gani kujenga bandari nyingine tena kwa bei kubwa.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
206,589
2,000
Mradi wa kujenga Bandari ya Bagamoyo ambao ulikuwa ugharimu dola bilioni 10 ulikuwa ni mzigo mkubwa sana kwa watanzania.

Watanzania tunatakiwa tumshukuru sana Rais Magufuli kusimamisha mradi huo la sivyo ingechukua miaka mingi sana kuilipa China mkopo wa ujenzi wa bandari hiyo ambayo isingekuwa na manufaa kiuchumi kwa Tanzania. Upanuzi wa bandari ya Dar kwa gharama nafuu ni hatua nzuri aliyochukua Rais Magufuli.

Kwa kipindi cha miaka miwili cha utawala wa serikali ya awamu ya 5 imeonyesha dira na mwelekeo mzuri katika kuwekesha kwenye miradi yenye manufaa kwa taifa.
Mzigo kwa mkopo wa masharti nafuu? Faida zake mbona hukuainisha na hasara za kutokuwa nayo?
 
Jua usiyoyajua

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
1,129
2,000
kama bandari ya Dar imekosa mizigo ya kutosha kuna umuhimu gani kujenga bandari nyingine tena kwa bei kubwa.

Question of time. Mahitaji yanaongezeka siku zinavyosonga na ndiyo sababu tunahitaji maandalizi ya muda mfupi na mrefu. Kufikiria ya kwamba mahitaji yako ya kesho yatakuwa sawa na ya Leo ni fikira mgando ambazo hazitufikishi kwenye maendeleo. Unapokuwa na degree moja Leo lazima uwe na mipango ya masters kesho.
 
lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,474
2,000
Kwani umesimamishwa!? ...maana mara ya mwisho nilimuona Prof. Mbarawa akitoa maelezo ya 'mchakato'.
Kinachonishangaza ni kuona matangazo yakitoka kila upande na kwa nguvu kubwa kuwa walioasisi hizi hasara tena kwa makusudi mazima ili wafaidike wao na familia zao eti wasiguswe wala kutajwa!
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,081
2,000
Question of time. Mahitaji yanaongezeka siku zinavyosonga na ndiyo sababu tunahitaji maandalizi ya muda mfupi na mrefu. Kufikiria ya kwamba mahitaji yako ya kesho yatakuwa sawa na ya Leo ni fikira mgando ambazo hazitufikishi kwenye maendeleo. Unapokuwa na degree moja Leo lazima uwe na mipango ya masters kesho.
Tuna bandari mbili zaidi Mtwara na Tanga tukiziboresha hizo tayari tutakuwa na uwezo mkubwa.
 
Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,199
2,000
Mradi wa kujenga Bandari ya Bagamoyo ambao ulikuwa ugharimu dola bilioni 10 ulikuwa ni mzigo mkubwa sana kwa watanzania.

Watanzania tunatakiwa tumshukuru sana Rais Magufuli kusimamisha mradi huo la sivyo ingechukua miaka mingi sana kuilipa China mkopo wa ujenzi wa bandari hiyo ambayo isingekuwa na manufaa kiuchumi kwa Tanzania. Upanuzi wa bandari ya Dar kwa gharama nafuu ni hatua nzuri aliyochukua Rais Magufuli.

Kwa kipindi cha miaka miwili cha utawala wa serikali ya awamu ya 5 imeonyesha dira na mwelekeo mzuri katika kuwekesha kwenye miradi yenye manufaa kwa taifa.
Wachina wangegeuza ndio navy base yao kama wasingelipwa.
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,081
2,000
Mzigo kwa mkopo wa masharti nafuu? Faida zake mbona hukuainisha na hasara za kutokuwa nayo?
China imejenga reli kati ya Mombasa na Nairobi kwa gharama ya dola bilioni 3. 8 na kulipa huo mkopo pamoja na riba yake kwa mradi huo kujilipa wenyewe wataalamu wa uchumi kenya wamesema itachukua miaka 600 kulipa huo mkopo. Tunapozungumzia mradi wa bagamoyo ni bilioni 10 bila riba kwahiyo serikali badala ya kulipa mkopo tutakuwa tunalipa riba tu kwahiyo bandari hiyo itaendelea kuwa mali ya China.
Mzigo kwa mkopo wa masharti nafuu? Faida zake mbona hukuainisha na hasara za kutokuwa nayo?
China imejenga reli kati ya Mombasa na Nairobi kwa gharama ya dola bilioni 3. 8 na kulipa huo mkopo pamoja na riba yake kwa mradi huo kujilipa wenyewe wataalamu wa uxhu
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,412
2,000
Hao hao ccm wanaitekenya na kucheka.
Hizo pesa alizookoa ziko wapi?
Ajira zenyewe hakuna.
Afu kuna waziri wa ajira
Kwahiyo nyie mlioko CDM ni kwamba kila linaloendelea na kufanya na viongozi wenu mnakubaliana nalo 100%, huwa hakuna pahala nguvu ya wengi inawaacha wachache ama kwenu demokrasia ni vazi tu? Na kama mna demokrasia kweli basi naamini si wote katika chama chenu huwa mnakubaliana na kama nyote mnakubaliana kwa kila jambo basi ni wazi pia, hamna demokrasia. Demokrasia kwa maana nyingine ni lazima kuwepo na mawazo tofauti lakini siku zote mawazo ya wengi ndio ushinda na ndo ubeba maamuzi.

Vivyo hivyo, CCM nako walikuwa na yao. Naamini wengi wao walishakaa ki upigaji pigaji lakini naamini wale wachache pia (akina Magufuli) nao walikuwepo ila kwa vile wanaokuwa wengi wanaruhusiwa kuungwa mkono hata kwa kuhusisha njia haramu za kulaghai na ndo walioko madarakani (bosi) basi nyie wachache mawazo yenu hayawezi kupenya. Kuna mambo JPM simwelewi lakini kumtizama JPM kwa macho ya wana CCM walio wengi nafikiri itakuwa ni kutokumwelewa vizuri ama kujianya msanii. JPM ni CCM lakini JPM ni JPM katika yeye, waulize CCM wenyewe watakusaidia kumfahamu vizuri zaidi.
 
Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
6,202
2,000
Dah ila Kikwete kaiba siyo mchezo. Dart kamega mamia ya mabilioni. Hazina kafyeka. Richmond kala. Iptl kila siku anapata mgao wake. Huko bandarini home shopping na makonteina kalamba. Cha kukasirisha anamuita lowasa fisadi. Gesi asilia kasafisha. Hii ya bandari ya bagamoyo alidhani Membe atakuwa rais hili waendelee kuifilisi nchi. Halafu anaomba wamuache apumzike.

Devil
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,826
2,000
Mbona inajengwa jamani, imesimamishwa waaapi?

Hata mimi nashangaa, kwani sisi tulikuwa tugharimie nini?? Watu wanazungumzia Bandari tu wamesahau viwanda ambavyo vingejengwa sambaba na Bandari ili kuongeza ajira kwa nguvu kazi, watu wanaopinga mradi huu sijui wana maana gani - someni machapisho kuhusu Silk Road Project ambayo itaunganisha reli za Asia, Continetal Europe, Uingereza na Africa - majaribio yamekwisha fanyika train imesafirisha mizigo kutoka China mpaka Uingereza, Wachina wamekwisha jenga reli Djibuti, Ethiopia na Kenya zitaungana na Tanzania, Zambia, Msumbiji mpaka South Africa - hii inamaanisha mizigo/containers zinaweza kusafirisha fasta kutoka/kwenda Uchina na Mataifa mengine kwa kupitia nchi kavu/reli bila ya kutumia usafiri wa Baharini.

Niliwahi kusoma sehemu fulani Wachina wanasema walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe kama Hub ya kusambaza bidhaa/mizingo kwenye landlocked Countries, wengine hilo hawalioni tunajifanya wajeuri tu na kusingizia watu - kwani sisi tuna nini cha ziada kuliko majirani zetu, mkiwazengua Wachina Nchi nyingine za Africa zitawakaribisha kwa mikono miwili, mfano Wakenya watawambia waende kuwekeza Bandari ya LAMU sisis tuendelee kula jeuri yetu.
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,081
2,000
Hata mimi nashangaa, kwani sisi tulikuwa tugharimie nini?? Watu wanazungumzia Bandari tu wamesahau viwanda ambavyo vingejengwa sambaba na Bandari wanaopinga mradi huu sijui wana maana gani - someni kuhusu Silk Road Project ambayo itaunganisha reli za Asia, Continetal Europe, Uingereza na Africa - majaribio yamekwisha fanyika train imesafirisha mizigo kutoka China mpaka Uingereza, Wachina wamekwisha jenga reli Djibuti, Ethiopia na Kenya zitaungana na Tanzania, Zambia, Msumbiji mpaka South Africa - hii inamaanisha mizigo/containers zinaweza kusafirisha fasta kutoka/kwenda Uchina na Mataifa mengine kwa kupitia nchi kavu/reli bila ya kutumia usafiri wa Baharini. Nilisoma sehemu fulani Wachina wanasema walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe kama Hub ya kusambaza bidhaa/mizingo kwenye landlocked Countries, wengine hilo hawalioni tunajisanya wajeuri tu na kusingizia watu - kwani tsisi tuna nini cha ziada, mkiwazengua Wachina Nchi nyingine za Africa zitawakaribisha kwa mikono miwili, mfano Wakenya watawambia waende kuwekeza bandari ya LAMU.
Hakuna kitu hii silk road project ni njia ya wachina kuzifanya nchi hizo kuwa koloni lake. Mbaya zaidi China inapiga vita sana corruption nchini mwao lakini ni wazuri sana katika ku export corruption kwende third world countries tujichunge sana na mikopo yao. Ndio maana Rais Magufuli amewaweka pembeni wachina kwenye mradi wa reli ya kati.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom