Hata kama unamiliki pesa isiwe sababu ya kumdharau mwenye kipato kidogo

MR MLAWA

JF-Expert Member
Apr 29, 2020
282
428
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza hapo juu. Leo hii nimeona sio vibaya kufikisha ujumbe au tukabadilishana mawazo jambo lenyewe ni:

Katika pita pita zangu ilikua mida ya mchana kuna sehemu nilienda kupata huduma ya kununua maji ya kunywa maana nilishikwa na kiu maana jua lilikua kali mno nikawa nimepumzika pembeni kidogo.

Mara akaja bodaboda akiwa na abiria wake akashuka akaenda kufanya huduma mazungumzo yalikua hivii maana niliyasikia yote.

Mteja: Habari yako

Mfanya biashara: Salama karibu boss

Mteja: Asante vipi ninaweza nikapata kiasi cha pesa kama Milioni moja na laki mbili 1.2 Mil mteja akiwa ametoa kadi yake ya bank na kumpatia mfanya biashara.

Mfaya biashara: Akamwambia ndio boss unaweza ukapata.Mfanya biashara akaanza proccess za kuanza kumtolea kwa kadi lkn kabla hajafika popote mara ghafla;

Mteja: Unayo mashine ya kuhesabia pesa?

Mfanya biashara: Hapana sina ninahesabu kwa mkono tu boss wangu.

Mteja: Hapana wacha niondoke nachelewa.

Mfanya biashara : Kama unaona utachelewa sawa hamna shida mteja akachukua kadi yake na kupanda boda akaondoka.

Nikaona hili suala limenigusa mno na kila nikijiuliza maswali bado nashindwa kuelewa hivi kweli yule mteja alishindwa kuhesabu milion moja na laki mbili kwa mkono au shida nini.Kwanini tunapenda kua na haraka zaidi kuliko kufanya mahitaji kama jamaa lengo lake lilikua ni kupata pesa kwa nini alishindwa kua na subira?
Machache ni hayo tu shere nawe kwa uelewa wako kuhusu uzi huu.

Mteja:
 
Dharau iko wapi hapo? Watoa huduma wengi wanashindwa kujiongeza, kuna mahali nilikuwa nadeposit 5m alaf mtu anahesabu kwa mkono, sema tu nilikuwa namlipa mtu na yeye ndo alinipeleka hapo, vinginevyo ningeachana naye.
 
Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile Nilichofikiri mimi huenda mtoa huduma mtaji wake bado mdogo ndio mana hana mashine ya kuhesabia pesa
 
Katoa sababu lakini kua atakua nje ya muda wakati Bwana Mfanyabiashara akihesabu Pesa kwa kutumia Mikono..... sijaona dharau bado
Milioni moja ina ugumu gani kuhesabu ina maana hata kama angepewa zile pesa aisingeweza kuhakiki na angetumia nini?
 
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza hapo juu. Leo hii nimeona sio vibaya kufikisha ujumbe au tukabadilishana mawazo jambo lenyewe ni:

Katika pita pita zangu ilikua mida ya mchana kuna sehemu nilienda kupata huduma ya kununua maji ya kunywa maana nilishikwa na kiu maana jua lilikua kali mno nikawa nimepumzika pembeni kidogo.

Mara akaja bodaboda akiwa na abiria wake akashuka akaenda kufanya huduma mazungumzo yalikua hivii maana niliyasikia yote.

Mteja: Habari yako

Mfanya biashara: Salama karibu boss

Mteja: Asante vipi ninaweza nikapata kiasi cha pesa kama Milioni moja na laki mbili 1.2 Mil mteja akiwa ametoa kadi yake ya bank na kumpatia mfanya biashara.

Mfaya biashara: Akamwambia ndio boss unaweza ukapata.Mfanya biashara akaanza proccess za kuanza kumtolea kwa kadi lkn kabla hajafika popote mara ghafla;

Mteja: Unayo mashine ya kuhesabia pesa?

Mfanya biashara: Hapana sina ninahesabu kwa mkono tu boss wangu.

Mteja: Hapana wacha niondoke nachelewa.

Mfanya biashara : Kama unaona utachelewa sawa hamna shida mteja akachukua kadi yake na kupanda boda akaondoka.

Nikaona hili suala limenigusa mno na kila nikijiuliza maswali bado nashindwa kuelewa hivi kweli yule mteja alishindwa kuhesabu milion moja na laki mbili kwa mkono au shida nini.Kwanini tunapenda kua na haraka zaidi kuliko kufanya mahitaji kama jamaa lengo lake lilikua ni kupata pesa kwa nini alishindwa kua na subira?
Machache ni hayo tu shere nawe kwa uelewa wako kuhusu uzi huu.

Mteja:
Muache mwenzio.
 
Dharau iko wapi hapo? Watoa huduma wengi wanashindwa kujiongeza, kuna mahali nilikuwa nadeposit 5m alaf mtu anahesabu kwa mkono, sema tu nilikuwa namlipa mtu na yeye ndo alinipeleka hapo, vinginevyo ningeachana naye.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Kuna mazingira aliyokuja nayo na maneno aliyokua akitamka alionyesha na sio uungwana.
 
Sababu ni kuwa aliona anaweza bambikiwa hela feki. Huu mchezo unafanyika sana huko uswazi
 
Huwa wanahesabu mara ya kwanza na ya pili kuhakikisha ,wanachelewesha hao kama una haraka zako
 
Back
Top Bottom