mcrounmj
JF-Expert Member
- Feb 26, 2016
- 380
- 885
Poleni na pilikapilika za kuumalizia mwaka twenty twenty.
Jana nilikuwa kwenye usafili wa basi, kutoka mbeya kwenda mwanza. Ni safari ndefu na inachosha maana ni zaidi ya msaa 18.
Kabla sijaenda kwenye maada husika labda niseme, kuna usumbufu mkubwa mno yanaupata mabasi haya ya mikoani. Ndani ya mkoa mmoja unakuta basi linasimamishwa na traffic wa barabarani zaidi ya saba. Hii inachosha na kukera abiria. Inapelekea kuchelewa kufika safari. Miaka ya nyuma tulipata shida sababu ya miundombinu ilikuwa mibovu, barabara zilikuwa za vumbi.
Leo tumeboresha barabara tatizo limejitokeza kwenye usimamizi wa usalama wetu barabarani. Naomba mamlaka zinazohusika mtoe gag order kwa mabasi ya mikoani yakaguliwe mkoa to mkoa, itasaidia sana kuokoa mda wa abiria na mabasi hayo.
Nirudi kwenye maada. Usalama wa taifa ni idara nyeti ambayo kwa kawaida watumishi wake wamefichwa makusudi kwa ajiri ya kutekeleza majukumu yao ya ushushushu katika hali ya kuliweka taifa salama. Matumaini yangu kuwa hata wanapopatiwa mafunzo, hufundwa namna ya kuishi kwenye jamii wakiwa maafisa vificho, wakitumia cover za kazi zingine ili wasigundulike kuwa ni maafisa usalama na waweze kutekeleza majukumu yao ya ukusanyaji intelijensia.
Sasa wapo maafisa uchwara, ambao pengine wamekosa weledi wa matakwa ya idara yao, kwa makusudi wanataka wajulikane na watu kwenye jamii kuwa wao ni maafisa vificho.
Jana katika safari niliyosema, konda katika route zake za kukagua tiketi, mida ya saa tatu usiku akamugumia mzee furani ivi wa makamo ya kama late forty hivi, akiwa siti ya pembeni yangu, yule mzee alikataa kutoa tiketi akidai ni usumbufu. Kondo akaachana naye akakagua kwa abiria mpaka akamaliza wote ndiyo akamurudia. Mzee amekataa kutoa tiketi anadai ampeleke polisi. Konda kuona hivyo akamvaa, we! Yule mzee alitoa maneno, akasema "ivi unanifahamu mimi ni nani, nitapiga simu hili basi ata lisifike linakokwenda, usicheze na mimi hunijui"
Yule konda naye akaunga nukta na kuelewa, ikabidi amchane "mzee kwani kuna ulazima wa kujulikana wewe ni nani, suala la kutoa tiketi tu unataka basi lote abiria wafahamu kuwa wewe ni nani. Kwanza nyie mara nyingi mnakuwaga ni wale vitengo vya chini, afisa wa juu anakuwa na busara na anaheshimu kazi za wengine".
Konda aliongea ukweli ila mchungu kwa afsa kificho uchwara huyu. Hata kama hakuwa afisa usalama ila mazingira aliyoyajenga ni kama yuko kwenye mkondo huo.
Konda alisema kweli. Kwa afisa usalama anyejielewa, kwanza anakuwa mstaarabu kwa kuheshimu majukumu ya wengine lakini pili anatumia weledi kuishi kadri kazi yake inavyomtaka hivyo hawezi kujionyesha kiboya hivyo.
Usalama wa taifa ni idara nyeti, mnao wajibu wa kuhakikisha taifa liko salama. Tumieni cover zenu kuficha identity zenu kwa maslahi mapana ya taifa letu.