Hata kama tumeachana/tumetengana sipo tayari kuona mabaya yanakupata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata kama tumeachana/tumetengana sipo tayari kuona mabaya yanakupata

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mary Chuwa, Feb 27, 2011.

 1. M

  Mary Chuwa Senior Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Imekuwa ni kawaida matukio mabaya kama ya kujeruhi,kuua yanawapata wale ambao wametengana baada ya kuwa aidha wapenzi au wana ndoa.
  Je ipo siku itafika waliotengana/kuachana wakafikia kusema hawapo tayari kuona mabaya yanawapata waliokuwa wapenzi wao na kupunguza kama siyo kufuta kabisa haya matukio mabaya ya kusikitisha tunayosikia kila kukicha baina ya wapenzi walioachana?
   
 2. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Mary wapo watu wanaoachana na kutakiana mema pale tu sababu za kuachana zinapokuwa zinaeleweka.wapo watu wanaokubali hali zilizowafanya waachane,wanasamehe na kujisamehe wenyewe.Kweli sababu nyingine zinazowaachanisha watu ni kubwa na zenye uchungu mkubwa,ila watu wakijifunza kumtumaini Mungu na kumtegemea hata kwenye breakups na kusamehe ipo siku watu watakuwa wanatakiana mema.Tatizo tunataka kubeba kila kitu kwenye vifua vyetu,mtu anakusanya hasira,mateso miaka mingi na pengine kuhatarisha hata maisha yake,laiti tungekuwa tunakubali alama za nyakati mapema tungeepuka mengi.Tutue mizigo kwa Mungu na tuvumilie kadri ya uwezo wetu na si kujilazimisha mwishoni yanashindikana unakimbilia kuua.
  ipo hata sasa ila tu namna ya kukabiliana na mitihani binadamu tumetofautiana,wapo wenye uwezo mkubwa,wapo wanaokimbia mapema na wapo wanaovumilia hadi mwisho wa safari yao.
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Inategemea na sababu za kuachana.
  Inawezekana nisitamke neno ila chozi langu likawaa ni laana kubwa kwa maisha utakayoenda kuyaface.
  Unajua hata wazazi sio wote wanaotoa maneno makali.
  Akishasononeka tu unaweza ukashaa hiyo minuksi itakayofumuka.
   
 4. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35

  Hata kama sababu ya kuachana ilikua kubwa vipi, je akiwa na shida na uko in position kumsaidia hutofanya hivyo? na je ukigoma kumsaidia akifa utaudhuria mazishi na kulia? Mimi na ndhani shida huwa zinatokea kwa njia nyingi, ikiwa unaweza kumsiadia mwenzio fanya hivyo and forget.
   
 5. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkiachana unamfatilia wa nini ili iweje? Mpaka uyajue yale yanayomsibu au yasiyomsibu.

  Kaza buti endelea na mambo yako achana na yaliyopita yampate mazuri/mabaya wewe yanakuhusu nini?
   
Loading...