Elections 2010 Hata kama rais akitoka kwao...tumepata ushidi wa demokrasia!

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
385
Kwanza napenda Kuwashukuru watu wote waliokuja na Wazo la Kuanzisha Chama cha CHADEMA. Nasema hivyo kwa sababu katika Historia ya siasa za Tanzania,Ni Chadema pekee iliyoleta Mapinduzi Makubwa ya Kidemokrasia nchini. Kwanza Madiwani wengi zaidi wa upinzani wameshinda,Wabunge wengi zaidi wa upinzani wanaingia Bungeni.Sijali kama Rais katoka katika Kambi ya Kijani lakini Kwangu MSHINDI WA DEMOKRASIA ni Dr. Slaa,shujaa pekee aliyeleta mabadiliko katika sura ya siasa za Tanzania na kuzima Ngonjera za CCM za ushindi katika Udiwani na Ubunge

KIKWETE AJIFUNZE NINI KUTOKANA NA MATOKEO YA UBUNGE?
Kwanza Kikwete atambue kuwa hadi Vijijini watu wameamka sasa,nani alifikirikia Wasukuma wanetoa Channgamoto kwa CCM huko Maswa na MEATU? Nani alifikiria Wakara na Wakerewe huko Visiwani wangetoa Chanamoto? Kikwete anapaswa Kujifunza kuwa:
  1. Watanzania Wameichoka CCM- Dr.Slaa Kuvuna Kura Vijijini (Japo hazitoshi) ni dalili kuwa hata watu wa vijijini wameichoka CCM
  2. Watanzania Wamewachoka WatAwala-Kuangushwa kwa Dialo,Masha, Batilda na watawala wenine wengi ni dalili tosha kuwa Wananchi wameacha sasa Kuangalia KIJANI na sana wanataka Mabadiliko
  3. Watanzania wanataka Mabadiliko- Mabadiliko ya Kiuchumi yameanza kwa kuwabadilisha Viongozi
Jambo ninalowaomba Wanajeshi wetu wa UPINZANI Wanaoelekea Bungeni (Wakiongozwa na wa CHADEMA) kuwa Msilale, Mpachimbe Bungeni Pachimbike Haswa.....Mpachakachue pachakachulike Haswaaaa.. Msisinzie kama akina Komba ambao hawasemi Chochote.
Kumbukeni Kuwa hata Kama Rais Katoka Kwao,Nguvu tuliyonayo katika Bunge na Mabaraza ya Madiwani inatosha kabisa kuleta Mabadiliko katika Nchi hiii.
Na kama CCM Ikikosea mwaka 2015 ikamleta Ole Ed Lowassa kama ambavyo source zangu zinanijulisha.. Basi Historia ya nchi itageuka kabisa.
Na pia Utulivu ndani ya Vyama ni jambo la Msingi Adui wa Chadema ni CCM na umaskini siyo Wanachadema...Tusiombane..Tusirumbane.
Nawatakieni uwakilishi mwema katika Bunge na Mabaraza ya Madiwani
Najua Dr. Slaa atakuwa Source Nzuri sana ya Data za ufisadi akiwa nje ya Bunge ili wapambanaji waliomo wapachimbe.

Mungu Ibariki CHADEMA...Mungu mbariki Dr.Slaa...Mungu Ibariki Tanzania
 
2015 kuna haja tukisimamishe chama kimoja tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
Na asiyetaka atakuwa mwana CCM
Joining hands is the only way to uproot CCM
 
Kura za urais lazima nazo wameiba. Tutajipanga tu mpaka kieleweke hata kwenye nafasi ya urais. Tusikubali kijingajinga tu Dr. Slaa ashindwe kwa umbali kiasi hicho.
 
MBONA HUMU JAMVINI PROPOGANDA NI KUKUBLI DR SLAA KASHINDWA WAKATI CHANNEL 10 WAMEZUIWA KUTANGAZA MOJA KWA MOJA KAMA WALIVYOANZA KUFANYA MWANZO NA TREND IKAANZA KULETA MATUMAINI CHADEMA? MBONA TUME IMEKATAZA MAJIMBONI YASITANGAZWE MATOKEO YA URAIS? MBONA WATU WAMEANZA KUKAMATWA NA KURA ZA WIZI HUKO MITAANI? kURA HIZI ZA WIZI ZIMETOKA WAPI? MBONA KATIKA MAENEO MENGI YA UPINZANI VING'AMUZI VINAKUWA NA KIGUGUMIZI NA SEHEMU WANAZOSHINDA CCM MITANDAO INAWAHI? KUNA MENGI YA KUJIULIZA KABLA YA KUKIMBILIA CONCLUSION. KATIKA SCIENCE CONCLUSION NI HATUA YA MWISHO SIO YA MWANZO AU KATIKATI. UNLESS MNATAKA NASI TUCHAKACHUE KAMA REDET NA SYNONOVET
 
Itafikia wakati watu uvumulivu utawashinda na hapataeleweka kabisa hapa nchini. Watu wanacezea sana hii amani tuliyonayo. Sisi tutawatoa tu madarakani hata wafanye vipi
 
tutaingia msituni 2015....lazima mafisadi watoke madarakani
 
Naona humu Jamvini kuna watu waliojichomeka kuendeleza Propaganda kuwa DR Silaa Atashindwa!!!. This is another Psychological warfare from CCM Preparing people to accept cooked Results.....Hatudanganyiki Ng'oooooooooooo!!

Hatukubali Mpaka Kieleweke!!

Nanaedhani JK atashinda amepata wapi data wakati matokeo hayajatangazwa???
 
Hatudanganyiki, tynajua walivyochakachua A-Z... kinachofuata ni movement ya kuwang'oa kote waliko chakachua... hakuna kungoja 2015.
 
MBONA HUMU JAMVINI PROPOGANDA NI KUKUBLI DR SLAA KASHINDWA WAKATI CHANNEL 10 WAMEZUIWA KUTANGAZA MOJA KWA MOJA KAMA WALIVYOANZA KUFANYA MWANZO NA TREND IKAANZA KULETA MATUMAINI CHADEMA? MBONA TUME IMEKATAZA MAJIMBONI YASITANGAZWE MATOKEO YA URAIS? MBONA WATU WAMEANZA KUKAMATWA NA KURA ZA WIZI HUKO MITAANI? kURA HIZI ZA WIZI ZIMETOKA WAPI? MBONA KATIKA MAENEO MENGI YA UPINZANI VING'AMUZI VINAKUWA NA KIGUGUMIZI NA SEHEMU WANAZOSHINDA CCM MITANDAO INAWAHI? KUNA MENGI YA KUJIULIZA KABLA YA KUKIMBILIA CONCLUSION. KATIKA SCIENCE CONCLUSION NI HATUA YA MWISHO SIO YA MWANZO AU KATIKATI. UNLESS MNATAKA NASI TUCHAKACHUE KAMA REDET NA SYNONOVET

Haya yanathibitisha uchaguzi huu siyo wa huru, haki na wa kweli.................DHULUMA ZA CCM ZIMETANDA KILA MAHALI............
 
Naona humu Jamvini kuna watu waliojichomeka kuendeleza Propaganda kuwa DR Silaa Atashindwa!!!. This is another Psychological warfare from CCM Preparing people to accept cooked Results.....Hatudanganyiki Ng'oooooooooooo!!

Hatukubali Mpaka Kieleweke!!

Nanaedhani JK atashinda amepata wapi data wakati matokeo hayajatangazwa???

Kwani ataesema Dr Slaa kashinda atakuwa kapata wapi data wakati matokeo hayajatangazwa?
 
Basi waache Propaganda. Waendelea kushiriki katika kulinda Matokeo yasichakachuliwe vituoni na kuendelea kuishinikiza Tume Itangaze matokeo sehemu ambazo haijatanaza.
 
Lakini nafikiri mtoa hoja ameangalia kwenye maeneo yote kabla hajatoa hoja yake. Mie nasema, tukubali tu kuwa Slaa ameshinda. Ameshinda, sio kwa kuwa rais lakini kwa kuleta mabadiliko makubwa ambayo hayajapata kutokea katika historia ya nchi hii tokea ipate uhuru wake miaka hamsini na ushee iliyopita. Wananchi wamefunguliwa macho na masikio na wameuona uovu wa CCM. Watanzania wanahitaji muda wa kusoma sura ya mchezo kabla hawajafanya a complete change of regime. Wengi wetu huwa tunaogopa mabadiliko. Lakini kama kuna kundi litaleta mabadiliko, na mabadiliko hayo yakaonekana yana maana, basi wengi watahamia kwenye kundi la mabadiliko. Kama wabunge wetu wapya wa Chadema watafanya kazi yao ipasavyo, basi Tanzania ya mwaka 2015 itakuwa ni Tanzania tofauti.
 
Kaka Mdogo Unaona Mbali sana mkuu
 
Kabisa
Kikubwa pamoja na yote we need to build CHADEMA from the roots, itakuwa raha sana ukiwa kijijini Mtwara unakuta branch ya CHADEMA, hapo kwa kweli 2015 njia itakuwa nyeupe!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom